Mwanamke anayejilipia mahari ndoa yake haiwezi kudumu

Je, mwanaume akilipa mahari ndo itafanya ndoa idumu?
na tukisema ndoa "imedumu" Je inatakiwa ifike miaka mingapi?

Pia, naongezea,
Je vipi sisi watu wa Asia ambao baadhi yetu kwa mila zetu, mahari analipa mwanamke?
Au sisi hii kanuni haituhusu.
 
Sema kuna age flan mwanamke alifika hajaolewa waga anaingia wenge sana, hakawii kilipa mahali na kugharamia harusi. Wanawake wanapitia mengi sana kwenye maisha yao. 😁
 
Mahari mi naona ni kama utapeli tu just imagining unaambiwa;
koti la babu 1M
blanket la bibi 500k
kanga za mam 300k
suti ya baba 2M
Hali Halisi: Ingawa mila zina uzito, ndoa nyingi siku hizi zinafunga kwa makubaliano ya wanandoa, na mahari inaweza kuwa ishara tu badala ya sharti gumu la kisheria/kiroho la ndoa kubaki imara.
 
Je, mwanaume akilipa mahari ndo itafanya ndoa idumu?
na tukisema ndoa "imedumu" Je inatakiwa ifike miaka mingapi?

Pia, naongezea, Je vipi sisi baadhi ya watu wa Asia wale ambao mahari analipa mwanamke?
Au sisi hii kanuni haituhusu.
Nimeandika hivi mwanzoni kabisa mwa mada..
Pamoja na wimbi kubwa la talaka na watu kutengana ama kuachana kabisa lakini hii ni special case kwa muktadha wa mada hii

Ishu ya huko Asia ndio inaweza kukuthibitishia nguvu ya mahari. Always mlipaji ndio mwenye mamlaka .. Fuatilia mpaka China utaona
Mwanaume aliyelipiwa mahari anatakiwa kuishi nyumbani kwa wakwe yeye na mkewe at least mwaka mmoja
Huko atafanya kazi zote za nyumbani iwe kilimo, ufugaji biashara ama hata kazi za ndani hasa kupika na kupeleka watoto shule
Na watakapohama wakaenda kuanzisha biashara zao mwanamke ndio mwenye mamlaka na pesa zote! Fuatilia utaona
 
Hali Halisi: Ingawa mila zina uzito, ndoa nyingi siku hizi zinafunga kwa makubaliano ya wanandoa, na mahari inaweza kuwa ishara tu badala ya sharti gumu la kisheria/kiroho la ndoa kubaki imara.
Sema kuna age flan mwanamke alifika hajaolewa waga anaingia wenge sana, hakawii kilipa mahali na kugharamia harusi. Wanawake wanapitia mengi sana kwenye maisha yao. 😁
 
Tatizo lililopo ni tafsiri tofauti tofauti ya neno Mahari kwa makabila mengi hapa Tanzania. Kuna makabila kanda ya Ziwa mfano usukumani, Mahari si anayeolewa ila anayeoza (anayetoa mtoto wake wa kike). Hii inageuka na kuwa kama fidia kwa kumtoa binti yake. Hivyo tukiwa tunajadili hili suala, tuwe waangalifu Mshana Jr
 
Kwa upande wa masuala ya kiroho mahari na bikira ni two way traffic. Wakati mwanaume anabebeshwa jukumu la kutoa mahari, mwanamke anabebeshwa jukumu la kutunza usichana wake kwa ajiri ya mumewe. Hivyo basi mwanamke bikira ndie mwenye uhalali wa kutolewa mahari. Mwanamke kujitolea mahari na mwanaume kumtolea mahari mwanamke asiye bikira ni vitendo viwili ambavyo vyote ni batili
 
🤔
 
Hili la 'mahari ni mali ya mwanamke' ni tamaduni za kabila gani au dini gani na uhalisia wa jamii ya Tz upoje kwenye issue hii?
 
Mahari ni utaratibu wa zawadi kutoka kwa muoaji kwenda kwa wazazi wa binti, kama shukrani ya kumstiri vyema.

Lakini mjomba Mshana Jr, hatuoni hili suala limesha najisiwa kitambo?

sasa hivi kila binti ni tiktok, fb, ig, kurusha kalio, ulevi, kuswali mpaka nabii asikike.

wame geuka wajuvi wa style zote za kujunjana, guest hii sio nzuri twende ile, watoto kibao, sigara bhangi aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…