Mwanamke anayejilipia mahari ndoa yake haiwezi kudumu

Mwanamke anayejilipia mahari ndoa yake haiwezi kudumu

Pamoja na wimbi kubwa la talaka na watu kutengana ama kuachana kabisa lakini hii ni special case kwa muktadha wa mada hii

Mahari ninini?

1.Wajibu wa Mwanamume: Katika mafundisho ya kidini (kama Uislamu na Ukristo), mahari ni zawadi au "mahr" inayotolewa na bwana harusi kwa bibi harusi kama sehemu ya mkataba wa ndoa na ishara ya utayari wake wa kumtunza mke.

2.Haki ya Mwanamke: Mahari inachukuliwa kuwa haki ya mwanamke na ni mali yake binafsi, si ya wazazi wake wala mumewe.

3.Utambulisho wa Thamani: Kiroho, kitendo cha mwanamume kutoa mahari kinaashiria thamani na heshima anayopewa mwanamke katika kuingia kwenye agano la ndoa

Kwa maana hiyo basi mwanamke hawezi kujilipia mahari, kwa tafsiri nyepesi hawezi kujioa.. Anakosa ule muunganiko wa kiroho wa agano la ndoa! Kwamba agano limeanzia kwake na limeishia kwake
Wanawake wanaojipia mahari hawana tofauti na wale wanaojioa mitandaoni

Yaani kwa kukosa mwanaume (Sahihi ama la) eti anaamua kujioa mwenyewe😀 !!! Hivyo anatengeneza nguo yenye pande mbili, upande gauni harusi, upande suti
Anaamua kutengeneza nywele kichwani na make up usoni, upande kike upande kiume😀

Miguuni hivyo hivyo mguu mmoja kiatu cha kike mwingine cha kiume!

Sina hakika na nduo ya/za ndani😀

Mwanamke anayejilipia mahari hana tofauti na makuku ya mayai yasiyo na baba.. Yale mayai hayana kizazi kwakuwa hayana muunganiko wa kigenetic wa pande mbili..

Hivyo pamoja na wimbi kubwa la talaka humo ndani asilimia 99 ni talaka za ndoa za wanawake waliojipia mahari
Si mnawaonaga mitandaoni wale watu wanaotangaza kujizawadia vitu? Wote hao ni walewale
Mwanamke lipiwa mahali hats kama hutafanya sherehe kwakuwa hilo ndio tendo kuu la kiroho la agano la ndoa!

Mwisho
Mahari sio pesa ya kununua bidhaa! Hivyo huwa hailipwi yote! Wazazi na walezi wanaokomaa ilipwe yote tena kwa mamilioni hao ni wafanyabiashara wanaouza mali mbovu wenye uhakika itarudishwa muda si mrefu!
Baadhi ya tamaduni ambazo wanawake wamekuwa wakijilipia mahali, ndoo zao zimekuwa zikidumu zaidi kuliko wanao lipiwa mahali. Siku hizi wanawake wamekuwa wahuni wahuni na vijana nao wehu tu, sasa mchanganyiko huu hauwezi kaa pamoja ndani
 
Baadhi ya tamaduni ambazo wanawake wamekuwa wakijilipia mahali, ndoo zao zimekuwa zikidumu zaidi kuliko wanao lipiwa mahali. Siku hizi wanawake wamekuwa wahuni wahuni na vijana nao wehu tu, sasa mchanganyiko huu hauwezi kaa pamoja ndani
Makutano ya kwanza disco
Makuta ya pili gesti
Huko kote kuna maroho ya kila aina
Uchumba miezi mitatu
Hamjajuana vema mnaenda kuishi pamoja?! Lazima kiwake
 
Roho la ndoa lina nguvu sana

Suellen Carey, a 36-year-old Brazilian influencer based in London, married herself in a 2023 "sologamy" ceremony to celebrate self-love and independence. After one year, she filed for divorce from herself, citing that the pressure of being her own perfect!

Huu sasa ni uchizi
Kajioa
Kajiishi maisha ya ndoa
Kajishindwa
Kajitaliki😂
Imagine hata kujiishi mwenyewe kwenye ndoa aliyojioa mwenyewe kashindwa😂
c1db956d-f3cf-41dc-94e9-a378d5a8a00d.jpeg
 
Hivi kuna wanawake wanajilipia Mahary hilo kwa tamaduni zetu za kiswahili lipo kweli na kama lipo ni makosa
 
Seran , anakataa tuu, hajatokea kuelewa tuu sehemu. Mbona atakuwa wa kwanza kutoa pendekezo na kishika uchumba. 😁
Hizo ndoa ni kujiweka tu usionekane kiumbe cha ajabu lakini hasara ni nyingi kuliko faida! Mazuri machache kuliko mabaya! Duhh kwanza kumwambia mtu habari za kunioa sijui kishika uchumba hmm! Hapana mkuu..
 
Hizo ndoa ni kujiweka tu usionekane kiumbe cha ajabu lakini hasara ni nyingi kuliko faida! Mazuri machache kuliko mabaya! Duhh kwanza kumwambia mtu habari za kunioa sijui kishika uchumba hmm! Hapana mkuu..

Kwa iyo mtu akileta proposal kukuoa unaikataa? 😁
 
Back
Top Bottom