Mwanamke anayejitambua hawezi kuwa Mke wa Pili au mchepuko

Chief ni nani anae oa je kuoa ni nini?
 
Lakutisha linakuaje na sio la kutisha lainakuaje,hakika leo umeandika pumba.
 
Unatusagia kunguni tulio na chance ya kugombea majimbo manne

Siô Kosa Mwanaume Kuoa Wanawake kadiri awezavyo. Na itaendelea kuwa hivyo Mpaka mwisho wa Dunia

Kwa Sababu Wanawake wasiojitambua hawatakwisha, Wanawake wavivu hawataisha Duniani.

Alafu post hii inadhihirisha JINSI Watu Wengi walivyo wanafiki na wabinafsi.
Hapa wanaibisha na Kúpiga kelele wakiulizwa utakubali Binti yako akawa Mke WA pili au au mchepuko wa Mtu ndîo haohao wanakuwa wakwanza kukataa.

Ndîo shida ya Watu Wabinafsi
 
Mwanaume anao Mwanamke anaolewa.
Kuoa NI kitendo cha Mwanaume kuchukua Mwanamke na kumfanya Mkewe
Kuolewa na kitendo cha Mwanamke kumchukua Mwanaume na kumfanya kuwa Mumewe.

Wewe unatafsiri Ipi ya Kuoa?
Mwanaume kumchukua mwanamke kumuoa na sio mwanamke kumchukua mwanaume bali mwanamke huchukuliwa na mwaume na kua mke anae oa ndie anae chukuliwa sio anae olewa .

Kuoa ni kukubali pia majukumu yote ya mke kua chini ya mume kama kiongozi hivyo hata mwanaume akaoa mke zaid ya mmoja huyo anatambua majukumu yake kwa wake zake na akayafanyia kazi pasi na kujalisha mke ana mali au elimu ya kiasi gani.
 
Isaya 4 : 1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
 
Hii nakupinga mkuu. Kuwa mke wa pili sio laana wala kutokujitambua labda kwako tu hili ndo kutokujitambua!!

Kwa Mwanamke anayejitambua hawezi kuolewa Mke wa pili hata iweje. Pia Mwanamke anayejitambua Kisha anajitegemea ndîo haiwezeniki Kabisa kuwa mke wa pili au mchepuko.


Jamii za kifugaji ni kawaida sana na ni Baraka kabisa na mahali hutolewa sawasawa na Wa kwanza.

NI umaskini wa Wanawake ndîo unawafanya wakubali kishingo upande kuolewa wake wengi Huko kwèñye jamii za kifugaji.
Pili umeingilia dini za watu wenye Imani ya kuoa Hadi wake4 na nikawaida kabisaa.

Hizô Dini Wanawake Asilimia tisini na tisa hawakubali hicho kipengele. Alafu hicho kipengele kipô Kwa Matamanio ya Wanaume na waanzilishi wa hizô Dini.


Uzungu umekuingia sana usijione uko sawa Kila Wakati muda mwingine unapuyanga vibaya.

Hata wazungu wàpo weye mtazamo wa kuoa Wake wengi.

Ninachopinga NI Mila Potofu
 
Unakuwa unajitahidi sana kuandika kifalsafa ila huwezi na bado una safari ndefu mno kuweza kuandika ipasavyo ukakubalika. Fanya vitu vingine tu jamaa
Aliyekuambia nataka kukubalika NI Nani?
Au wewe unafanya vitu ili ukubalike?

Yàani niandike ili wewe unikubali ili Mimi nipate nini? Wewe kunikubali au kunikataa inaniongezea kitu gàni?
 
Hakuna kujitambua kwa mwanamke mbele ya mwanaume mwenye akili timamu, ni jambo la asili, ni mwanamke kwa ajili ya mwanaume na si mwanaume kwa ajili ya mwanamke.
 

Aliolewa akiwa Namba Moja?
Mwambie Sasa hivi kama atakubali.

NI Sawa na Christina Shusho unaweza ukamuoa Mwanamke akiwa hajajitambua au Kwa sababu ya umaskini wake Akakubali kuwa hata Mke WA Saba Huko lakini Siku akijitambua au kujipata Hawezi kukubali tenà huo ujinga
 
Aliyekuambia nataka kukubalika NI Nani?
Au wewe unafanya vitu ili ukubalike?

Yàani niandike ili wewe unikubali ili Mimi nipate nini? Wewe kunikubali au kunikataa inaniongezea kitu gàni?
Soma tena ulichokiandika na nilichoandika ulinganishe
 
Hakuna kujitambua kwa mwanamke mbele ya mwanaume mwenye akili timamu, ni jambo la asili, ni mwanamke kwa ajili ya mwanaume na si mwanaume kwa ajili ya mwanamke.

Ndivyo mnavyojidanganya?

Mwanamke aliumbwa kwaajili ya Mwanaume. Umesema kweli lakini siô Mwanamke anayejitambua aumbwe akawe Nyumba ndogo au mke wa pili ilhali Wanaume Wengine wàpo. Huko ni kutojitambua
 
Bible ina kila kitu, sijasema mm

Kwa sababu Siku za mwisho Upendo utapoa na wasiojitambua wataongezeka maradufu.
Na dhulma itakuwa Ipo juu.

Sasa wanawake saba wajitongozeshe Kwa Mwanaume mmoja huoni Hapo kuna tatizo.

Biblia inajua vyema matatizo ya jamii.

Siku za mwisho Upendo WA wengi utapoa lakini haijasema Upendo wa wôte au wfulani utapoa.

Vivyohivyo, Wanawake sababu watakaojidhalilisha ili kuondoa ya Kukosa Mume haitawahusu Binti za Tibeli
 
Mbona namba moja anaendelea na ndoa yake? Si atoke huko kama amejitambua. Watu wasipangiane maisha, kama wewe hupendi kitu it is fine , na wao pia . Kila mtu achague au afanye anachoona kinafaa.

Hapa duniani kila mtu ana ujinga wake. Kwa mfano, kwa wazungu , mitala hairuhusiwi lakini ushoga au ndoa za jinsi moja ni halali na zinalindwa na sheria .
 
Mbona namba moja anaendelea na ndoa yake? Si atoke huko kama amejitambua. Watu wasipangiane maisha, kama wewe hupendi kitu it is fine , na wao pia . Kila mtu achague au afanye anachoona kinafaa.

Hapa hamna aliyechaguliwa.
Kutojitambua nako NI uchaguzi Mkûu.
Kuhusu Namba Moja nimeshakuambia kuwa hata yeye ukimuuliza Sasa hivi hawezi kukubali.


Hapa duniani kila mtu ana ujinga wake. Kwa mfano, kwa wazungu , mitala hairuhusiwi lakini ushoga au ndoa za jinsi moja ni halali na zinalindwa na sheria .

Wazungu wanatoka Wapi?
Hata wazungu wàpo weñye mitazamo ya Ndoa za mitala.

Hapa Afrika zîpo familia nyingi Ambazo hawataki Ndoa za mitala

Huko arabuni zîpo familia pia Ambazo hazitaki Ndoa za mitala

Ushoga ni Dhambi
Kuoa wake wengi au kuolewa wake wengi Siô dhambi Ila NI kutojitambua.
 
Nimesema ulaya hawaruhusu mitala na haipo kisheria, sijakataa kama hakuna wazungu wanapenda mitala. Tunarudi pale pale, kila binadamu ana mtazamo wake kuhusu jambo fulani. Mitazamo ya watu na iheshimiwe. Hatuwezi kuwa na mitazamo inayofanana hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…