NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Unaonekana wewe ni mchawi.Kila mtu na bahati yake na bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi.Soma vizuri habari yake usikurupuke.Amana hawakutangaza nafasi za kazi kilichotokea huyu mama alikwenda kumtembelea rafiki yake alizaa njiti ndio akaamua kumsaidia baada ya wiki mbili mtoto kaongezeka uzito wakati anataka kutoka akaona mtoto mwingine ametelekezwa kwa huruma ya kibinadamu akasaida na wa pili tena.Swali je wewe ukiona nyumba ya jirani yako inaungua moto na una ndoo ya maji utaacha kuchukua maji kuzima moto kama una uwezo kisa hadi wazima moto wenyewe waje?.1.kuna vijana wengi sana wamemaliza vyuo mtaani, wamepeleka barua za kujitolea pale Amana, wamenyiwa hiyo nafasi,inakuwaje mtu from no where asie na kazi Wala taaluma husika akaomba nafasi ya kujitolea na akapewa?
2.Huyu binti ana Mume,na watoto (family) how comes Mwanaume amruhusu Mkewe akiwa anajua Hana taaluma husika, akajitolee sehemu?
Note: najua watu wengi, mmepongeza Sana,Ila wasiwasi wangu upo palepale!
Kuna Jambo kubwa nyuma ya pazia linaloendelea.
Mfano hiyo namba mbili ndio umechemsha kabisa suala la mtu na mkewe mumewe kumruhusu wewe linakuhusu nini.Pilipili iko shambani wewe mdomo wako unawasha nini.
Nahisi utakuwa ni moja ya watu waliokosa ajira tafuta shughuli za kufanya ziko nyingi sana hata kama ni graduate fungua kijiwe piga viatu rangi.Jamaa mmoja Arusha kamaliza shahada ya sheria anang'arisha viatu amekuwa tajiri kiasi kwamba hataki hata kusikia neno kuajiriwa changamka dogo