Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela

Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela

Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela ila yeye ndiye atakupa wewe.

Atafanya kila awezavyo akutafutie vizawadi ili ujue anakupenda.

Atatumia gharama zake mwenyewe.
Mwanamke anayekupenda anakutaka wewe tu kama ulivyo anakuhitaji tu wewe. uwepo wako kwake unatosha, hahitaji pesa yako.

Ukiona mwanamke anataka sana pesa zako mpaka analalamika ujue huyo hakupendi ni mwanamke wa mtu mwingine huyo.

Tena hizo pesa ukimpatia anaenda kumgawia yule anayempenda kikweli.

Katafute wakwako, huyo sio wako.
Basi ukute pengine mtoa mada kaombwa elfu 10,000..
Kaamua kufunguwa uzi,.
 
Mwanaume Rijali anaprovide kwakweli... Hatumaanishi Kwamba wanawake wasiwasaidie wanaume lahasha...kusaidiana kupo.

Lakini Wewe mleta mada hata kutoa hela y nauli TU ha bodaboda utaleta bandiko humu.. wanawake wanapenda pesa..

Nakuona Kama unatatizo either unatatizo la kifedha... Au unatatizo na mwanamke kupewa hela... Unaona Kama hatakiwi kupewa hiyo hela
Wewe naona hujamuelewa mleta uzi
 
Endelea kujidanganya mkuu sawa eenh eti unasemaaaaa
mkuu ndio hivyo huo ndio ukweli, nina mifano ya marafiki zangu Kabisa mkuu nimeshuhudia kwa macho yangu, rafiki yangu anaonyeshwa penzi na mwanadada mmoja alitokea kumwelewa mshikaji ile mbaya, dada alikua ndiye anamtoa out mshikaji,
 
Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela ila yeye ndiye atakupa wewe. Atafanya kila awezavyo akutafutie vizawadi ili ujue anakupenda. Atatumia gharama zake mwenyewe.

Mwanamke anayekupenda anakutaka wewe tu kama ulivyo anakuhitaji tu wewe. uwepo wako kwake unatosha, hahitaji pesa yako. Ukiona mwanamke anataka sana pesa zako mpaka analalamika ujue huyo hakupendi ni mwanamke wa mtu mwingine huyo.

Tena hizo pesa ukimpatia anaenda kumgawia yule anayempenda kikweli.

Katafute wakwako, huyo sio wako.
Dah... kijana tafuta pesa....acha kulialia....utajikuta wanawake wote unawaita shemeji [emoji2960]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom