Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela

Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela

Tupambane 2tafute pesa! inamaana hata dem wako akikuomba buku ya kununulia SMS zakuchat nawewe hapa tayal atakuwa akupend or??
 
Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela ila yeye ndiye atakupa wewe. Atafanya kila awezavyo akutafutie vizawadi ili ujue anakupenda. Atatumia gharama zake mwenyewe.

Mwanamke anayekupenda anakutaka wewe tu kama ulivyo anakuhitaji tu wewe. uwepo wako kwake unatosha, hahitaji pesa yako. Ukiona mwanamke anataka sana pesa zako mpaka analalamika ujue huyo hakupendi ni mwanamke wa mtu mwingine huyo.

Tena hizo pesa ukimpatia anaenda kumgawia yule anayempenda kikweli.

Katafute wakwako, huyo sio wako.

Mwanzisha mada unaonekana upo katika mahusiano mapya na umeshidwa kutambua Siri ya mtungi kuhusu wanawake sasa mi naomba nikuibie Siri hii mapema

1.mwanamke asiekuomba hela mara zote yupo katika kipindi cha kukusoma wewe kiuchumi na kitabia katika uhusiano wenu

2.mwanamke asikuomba hela anakuwa ametokea kwenye mahusiano ambayo kaachwa sababu ya kuomba hela hivyo anajaribu kulinda mahusiano yake mapya

3.mwanamke asiekuomba hela huwa anajaribu kucheza akiri yako kwanza taratibu sana

Mwisho kabisa siku zinavyosonga mbele huwa anaanza kubadilika taratibu sana akifikia point anataka kuleft mahusiano hapo ndipo vijana wengi tunaanza kulalamika mpenzi wangu kabadilika kumbe mwenzio Kampata mtu bora zaidi yako
 
Mapenzi ya kwenye tamthilia hayo ila ukija kwenye maisha halisi ni sizani kama wanazidi watatu ktk 10.

Siku hizi hata mazali ya mentali hamna cha msingi tafuta hela.
 
Tupambane 2tafute pesa! inamaana hata dem wako akikuomba buku ya kununulia SMS zakuchat nawewe hapa tayal atakuwa akupend or??
Nadhani mtoa mada hazungumzii mizinga ya buku! Anazungumzia vizinga vya hela ndefu visivyo na idadi.
 
Mapenzi ya kwenye tamthilia hayo ila ukija kwenye maisha halisi ni sizani kama wanazidi watatu ktk 10.

Siku hizi hata mazali ya mentali hamna cha msingi tafuta hela.
Ratio ni mmoja katika hamsini kwanza hata haipendezi na midevu yangu hii halafu nigharamiwe na mwanamke!!




MAGUFULI4LIFE
 
Mwanzisha mada unaonekana upo katika mahusiano mapya na umeshidwa kutambua Siri ya mtungi kuhusu wanawake sasa mi naomba nikuibie Siri hii mapema

1.mwanamke asiekuomba hela mara zote yupo katika kipindi cha kukusoma wewe kiuchumi na kitabia katika uhusiano wenu

2.mwanamke asikuomba hela anakuwa ametokea kwenye mahusiano ambayo kaachwa sababu ya kuomba hela hivyo anajaribu kulinda mahusiano yake mapya

3.mwanamke asiekuomba hela huwa anajaribu kucheza akiri yako kwanza taratibu sana

Mwisho kabisa siku zinavyosonga mbele huwa anaanza kubadilika taratibu sana akifikia point anataka kuleft mahusiano hapo ndipo vijana wengi tunaanza kulalamika mpenzi wangu kabadilika kumbe mwenzio Kampata mtu bora zaidi yako
Hili ulilosema liko wazi na kimsingi wanawake wengi hutaka kuhudumiwa ila kuna exceptions. Ambacho kimetokea ni kuwa mtoa mada ameshindwa kulieleza hilo jambo vizuri ameegama upande mmoja kiasi watu wamemtafsiri tofauti.

Ukweli lazima usemwe, iko hivi, mwanamke anayekupenda hatakuehenyesha kama yule ambaye hakupendi. Mwanamke akipenda anakuwa radhi kutoa support ya hali na mali inaweza isiwe pesa but ile emotional support itakuwa ya hali ya juu akikusihi kuwa usijali things will get better, atakusaidia connections za michongo kama yuko connected. Wengine wanafikia hata kukufungulia kitega uchumi kama biashara ili ikupush usifadhaike in case uko vibaya kiuchumi maana anachohitaji wote muwe na amani.

Kuhusu hela, hawezi kukulazimisha umtumie hela au umpe pesa ikiwa anajua hauko kwenye position ya kumpatia japo unaweza jitutumua ila neno lake kuu huwa usijali mpnz. Anakuwa na hali ya uvumilivu ndio ile kitu wanasema Upendo huvumilia na trust me anakuwa very loyal regardless ya status yako because she feels on you. Saingine ndio it goes beyond that, atataka muende out mkale bata with all bills on her cause she feels tamed

Shida iliopo kwa sasa wanaume wengi tumekuwa mistreated kwenye mahusiano na wanawake ambao ni self-centred ambao wako kimaslahi hasa wa hapa Dar ni uozo mtupu!!! Malaya bubu ni wengi sana kiasi kwamba tunaona ni ajabu pale mwanamke anapojitoa sababu ya mapenzi kwa jamaa yake.

Wanawake wa sasa hawana Upendo (Uvumilivu,Huruma na Uaminifu) wao wanaangalia maslahi yao na hasa pesa zako na imekuwa kama norm. Anakusoma kama hajavutiwa na wewe na huna dalili ya kuwa nazo hawezi ku engage kwenye mahusiano na wewe at all...anakutia vizinga hadi ukimbie mwenyewe! Na ndio maana kuna lindi la wanawake matapeli ila still ana kijamaa chake ambacho anakipenda na kinamla free of charge. Mapenzi ndio yako hivyo ila ukiwa on a disadvantaged side always utahisi kwamba mapenzi ni pesa tu maana kila unayekutana nae anakukamua tu.
 
Si ndio apo.. yan mtu akulalie na kilo zote hizo afu bado mimi ndio nimnunulie vizawadi eti.
siyo lazima mwanamme amlalie mwanamke....hata mwanamke anaweza kumlalia mwanamme...lakini majukumu ya mwanamme yapo pale pale
 
Mwanamke anayekupenda kikweli hawezi kukuomba hela ila yeye ndiye atakupa wewe. Atafanya kila awezavyo akutafutie vizawadi ili ujue anakupenda. Atatumia gharama zake mwenyewe.

Mwanamke anayekupenda anakutaka wewe tu kama ulivyo anakuhitaji tu wewe. uwepo wako kwake unatosha, hahitaji pesa yako. Ukiona mwanamke anataka sana pesa zako mpaka analalamika ujue huyo hakupendi ni mwanamke wa mtu mwingine huyo.

Tena hizo pesa ukimpatia anaenda kumgawia yule anayempenda kikweli.

Katafute wakwako, huyo sio wako.
Mwanamke akikupenda kweli atafanya kila kitu kwa upendo, atakupa chochote kilicho ndani ya uwezo wake, atakua msaada wa hali na mali kwako.
Ila anapofanya yote hayo hisia zake, akili zake, matamanio yake ni kupendwa na kutendewa kama mwanamke au mke.... Kutunzwa, kupewa kipaumbele, kupewa ulinzi na mengineyo.
Mwanaume ukiamua kupokea bila kufanya yanayompasa na najidanganya unapendwa ujue unajiingiza kwenye majanga. Kuna siku anachoka, atakuona mzigo, atakuambia unayotakiwa kufanya halafu utaona anakudharau kumbe ulianza mwenyewe. Hakunaga haki sawa kwenye asili, imani na uumbaji wa Mungu.

Halafu wanawake tunajijuaga wenyewe na akili zetu EllySkyWilly
 
Back
Top Bottom