Mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

Mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
Husika na mada hapo juu, swali kwenu enyi wanaume, mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

Hivi huwa mnajisikiaje kutudanganya na kutuharibia maisha, unakuta mwanaume anafanya juhudi zote kukutongoza unamkubali, una fall in love, anakwambia maneno mazuri, mna panga mipango mingi ya maisha ila ghafla kila kitu kinabadilika.


Unashangaa mbona mwenzangu kachange na hamtoi hata taarifa, ni kimya tu simu hazipokelewi meseji hazijibiwi, ukija kuchunguza kumbe ana mahusiano yake permanently💔 tena mwingine anaweza hata kukuacha na mimba kabisa na wala hajali.


Hivi, huwa mnafikiria mara mbili mnachokifanya? Just imagine dada yako au ndugu yako wa kike ndiyo anafanyiwa unyama kama huo, utajisikiaje eti, kumbukeni what goes around, comes around. Na baadae mwanaume kama huyu anakuja kupiga vita single mother 💔

Wanaume wa namna hii ndiyo mnaofanya baadhi ya wanawake tunakuwa wakatili.
 
IMG-20250725-WA0204.jpg
 
kwa sasa hivi wanawake ni wengi Sana mkuu hata ungekuwa wewe ndo mwanaume sifikirii Kama ungeweza kuvumilia kukaa na Mwanamke mmoja .

Kwahiyo Kama amekuacha ujue kaenda kwa mwingine unabidi usichukie ukitaka kila mwanaume akae na wewe tu unafikiri hawa wenzako itakuaje.
Mh! Kwahiyo wewe unaona ni sawa wanawake tukiendelea kudanganywa na kuharibiwa maisha?
 
Ingekuwa miaka ya zamani ingekuwa ni kweli wanawake mnadanganywa na kurubunika. Ila sio wanawake wa sasa.

Wengi wenu ndio wezi wa mapenzi na matapeli wa mahusiano mpo after money 💰. Mkikutana na wajanja wamewazidi mbinu na ujanja mnakuja kulia lia kuwa mnachezewa kumbe ukweli mnacholalamika ni kuwa wale mliowadhania kuwa ni mafala nowadays wanawazidi kete na ninyi mnaambulia patupu.

Kuna mdada juzi kati hapa kisa chake ukisikiliza unasema wanawake wa kizazi hiki wengi mtazeekea kwa wazazi au mtaishi maisha ya nje ya ndoa hadi uzeeni.

Dada ni mzuri kabisa pisi ya maana. Alipangishiwa nyumba kubwa na jamaa akalipia kodi miezi mitatu. Akawekewa baadhi ya vitu ndani na akapewa gari ya kutembelea.

Tukio halijachukua hata miezi miwili. Mwamba alikula sana mzigo halafu akapita hivi.

Gari ilikuwa ni ya watu iliwekwa bond alikuja kufuatwa na watu tofauti wamekuja chukua gari yao. Vitu vya ndani furniture zilikuwa zinadaiwa ni za mtu ziliwekwa bond pia zilikuwa bado mpya.

Nyumba ililipwa kodi miezi mitatu tu inatakiwa kulipiwa tena baada ya hapo na kodi ni 400K.

Mdada alikuwa kashajiweka comfortable. Ingawa ana kazi ila jamaa alimtengeneza kuwa atasimamia show kumbe ni wahuni tu wa mjini.

Kwa kifupi mlianzisha michezo ya uhuni kwenye mahusiano hadi wanaume serious wamepungua sana siku hizi mnapata matapeli wenzenu. Kuleni chuma hicho.
 
Back
Top Bottom