Husika na mada hapo juu, swali kwenu enyi wanaume, mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?
Hivi huwa mnajisikiaje kutudanganya na kutuharibia maisha, unakuta mwanaume anafanya juhudi zote kukutongoza unamkubali, una fall in love, anakwambia maneno mazuri, mna panga mipango mingi ya maisha ila ghafla kila kitu kinabadilika.
Unashangaa mbona mwenzangu kachange na hamtoi hata taarifa, ni kimya tu simu hazipokelewi meseji hazijibiwi, ukija kuchunguza kumbe ana mahusiano yake permanently💔 tena mwingine anaweza hata kukuacha na mimba kabisa na wala hajali.
Hivi, huwa mnafikiria mara mbili mnachokifanya? Just imagine dada yako au ndugu yako wa kike ndiyo anafanyiwa unyama kama huo, utajisikiaje eti, kumbukeni what goes around, comes around. Na baadae mwanaume kama huyu anakuja kupiga vita single mother 💔
Wanaume wa namna hii ndiyo mnaofanya baadhi ya wanawake tunakuwa wakatili.