Mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

Mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

Husika na mada hapo juu, swali kwenu enyi wanaume, mwanamke kama haumpendi unaingia kwenye maisha yake kufanya nini?

Hivi huwa mnajisikiaje kutudanganya na kutuharibia maisha, unakuta mwanaume anafanya juhudi zote kukutongoza unamkubali, una fall in love, anakwambia maneno mazuri, mna panga mipango mingi ya maisha ila ghafla kila kitu kinabadilika.


Unashangaa mbona mwenzangu kachange na hamtoi hata taarifa, ni kimya tu simu hazipokelewi meseji hazijibiwi, ukija kuchunguza kumbe ana mahusiano yake permanently💔 tena mwingine anaweza hata kukuacha na mimba kabisa na wala hajali.


Hivi, huwa mnafikiria mara mbili mnachokifanya? Just imagine dada yako au ndugu yako wa kike ndiyo anafanyiwa unyama kama huo, utajisikiaje eti, kumbukeni what goes around, comes around. Na baadae mwanaume kama huyu anakuja kupiga vita single mother 💔

Wanaume wa namna hii ndiyo mnaofanya baadhi ya wanawake tunakuwa wakatili.
Ni kweli hili ni jambo baya,bora umwambie ukweli kuwa unataka papuchi tu
 
Mwaka juzi hapa nimekutana na pisi moja tukaelewana sana. Na yenyewe ndiyo ilifanya the next move. Katika maongezi yetu ya mwanzo tu blah blah kibao ooo we Jaws unajitambua na ni ndoto yangu kuwa siku moja nije nipate mume kama wewe. Mi nikaamua kusema ukweli kwamba kuna jambo nalifanya ndani ya hii miaka miwili - mitatu yaani sitaweza kabisa kuoa. Kama unaweza kunisubiri sawa lakini kama una haraka endelea tu kumtafuta Mr. Right wako. Tukacheka pale nikidhani kila kitu kiko sawa. Weh! Jioni ile nikapata bonge la gazeti miksa matusi na pin za uhakika + bloku juu. Nilikuwa sijaila na sikuwa nayo feeling kivile hivyo nikapotezea mazima na baadaye nikapata kisafari nje ya nchi.

Nimekuja kurudi juzi hapa nakutana nayo inalalamika vibaya sana kuwa niliipotezea. Oooh you ghosted me jaws. Kidogo niizabe vibao. Katika kuongea ndiyo ikasema kusema kwako ukweli kuliniumiza sana maana ilionekana kama vile hunitaki. Kwani ungekausha tu tukaingia kwenye mahusiano ingekugharimu nini? Ilikuwa lazima useme ukweli vile? Nilishangaa sana na ndiyo nikajifunza kwamba wanawake aisee wanapenda kudanganywa.

Kama wewe unapenda msema kweli basi zama P.M. tufanye mature convos. I am ready now to settle down and start a family. Karibu sana PM waifu material
Huyu atakuwa wa 10😅😅🏃🏃🏃
 
Mwanaume ni kichwa, na mwanamke ni shingo; kazi ya shingo ni kuzungusha kichwa upande wowote anaotaka, sasa kama shingo imeshindwa kazi yake, nani alaumiwe?
Mwanamke ana nafasi kubwa sana ya kumtengeneza mtu wake na kuwa mchumba sahihi kwake, kushindwa kwake huko, mwanamke anakuwa hajui wajibu wake; hajatumia nafasi yake kama mwanamke.​
 
Mwanamme rijali hakatai mimba!huwezi ongeza makosa wakati yajayo kukuhusu no giza!huwezi jua ni mtoto yupi atakufaa!

Kuna dogo Huwa anamzimia mama yake sim akiwa na hela!watoto wamepinda nyie!
Ninawashangaa sana hawa wanaume wanaofanya ukatili wa kukataa mimba
 
Back
Top Bottom