Mwanamke kumbuka yafuatayo unapotoka na mume wa mtu

Mwanamke kumbuka yafuatayo unapotoka na mume wa mtu

Mtoa mada hukumbuki ndoa zingine zinawaka moto wakumbushe na wanawake kwenye ndoa waache wenge halafu mbona mabinti wanafanyiwa mambo mabaya na hao wanaotakiwa kuwaoa kuliko hata hao waume zawatu sishauri wafanye hayo ila kunawatu wanajitambua wanamahusiano yaaina hiyo wanaishi vizuri tu ivi hao vijana wakuoa ndohawa
 
Suala la mtu kutoka na mume wa mtu halijaanza leo wala Jana na haliishi siku yoyote hivi karibuni. Kwenye bible Wakina Hajri wametoka na wazee wa zamani wa imani. Kubwa ni kuweka heshima na mipaka.
 
V
Dada yangu kipindi utakapokubali kutoka kimapenzi na mume wa mtu, utakuwa umekubaliana kuwa mwanamke wa daraja la pili. Na siku zote mtu wa daraja la pili ni mtu wa daraja la chini ukilinganisha na daraja la kwanza.

Angalia sasa, kama yupo na wewe na mke wake akapiga simu atamdanganya mkewe kwamba yupo ofisini au katika kikao na hautakuwa na ujasiri wa kuingilia mawasiliano yake. Pia anapokuwa nyumbani kwake kwa mkewe huwezi kumpigia au hata kumtumia text.

Dada yangu wewe ni mdoli? Anakuchukua kwenu na gari yake anakupeleka katika vyumba vya hotel lakini mke wake amemkabidhi nyumba nzima. Dada yangu, shtuka. Anakutembelea nyumbani kwako na unamtambulisha kwa rafiki zako na majirani kwamba ni boyfriend wako bila kujua unajizibia nafasi za kupata mtu sahihi wa kuweza kujenga nae maisha. Na mbaya zaidi hupajui hata yeye anapoishi.

Dada yangu mpaka lini utaendelea kujiharibia future yako? Anatoka na wewe out na anakununulia kila aina ya pombe na wakati huo huo hawezi kumruhusu mkewe kunywa pombe ya aina yoyote ile. Akili ya kawaida ikwambie kwamba anafanya hivyo ili ulewe vilivyo na apate wasaa wa kukukandamiza vizuri kitandani.

Dada yangu, je mwili wako ni wa majaribio? Anakupa mimba na anakupa pesa uende ukaitoe lakini mke wake akipata mimba nyumbani ni sherehe na anampa pesa za kuandaa martenity dress na vitu vya mtoto. Dada yangu kumbuka tayari anayo familia yake, kama ulikua hujui jamaa huwaelezea marafiki zake yote mnayofanya hotelini, lakini hata siku moja hawezi kuwalezea yale anayofanya na mkewe.

Hii inafanya marafiki zake wakuone kama mwanamke wa hadhi ya chini kabisa. Unazo picha zake katika simu yako na umesave namba yake kwa majina mazuri kama sweetheart, my love, etc lakini picha zako haziwezi kupatikana katika simu yake na namba yako ameisave kama fundi jenereta, fundi gari, mzibua chemba. Unatakiwa ukumbuke kwamba mwanamke asiye na akili sehemu zake za siri ndizo zitakazoumia zaidi. Amka dada yangu unatumika.

hivyo vi sentence vya mwisho vinauchungu zaido. Poleni wadada.
 
Back
Top Bottom