Watu kuwa tofauti hakuyafanyi Kanuni za mapenzi kuwa Tofauti,
Mapenzi bila kujali Watu wapo tofauti yanahitaji, Kujali, kuthamini, kuvutiwa, kujitoa n.k. mapenzi yanaongozwa na Kanuni kinzani ya Wivu. Wanadamu wote wanawivu linapokuja suala la mapenzi licha ya kuwa Binadamu kuna baadhi ya ishu tunatofautiana.
Kuhusu hizo Kanuni za mapenzi, sasa itategemea na tamaduni husika jinsi ya kuzitekeleza.
Mfano, Mwanamke wa Kikurya ili ajue unamjali basi sharti umpige. Wakati Mwanamke wa jamii zingine ukimpiga atajua haumpendi.
Sasa wewe unajadili hiyo tofauti ya mchakato wa kujali badala kuangalia dhamira ya mchakato ni kuonyesha Kujali. Nafikiri wewe unajadili zaidi Reactions kuliko lengo au chanzo cha hiyo reaction.
Mfano mwingine, MTU anaweza akafumania Mkewe au mumewe lakini mmoja akaua na mwingine asiue. Lakini Wote Wataumia(Wivu) lakini reaction zao zitakuwa tofauti Kutokana na sababu zingine ambazo zipo katika vipengele vingine labda vya Afya ya Akili, vyakula MTU anavyopendekea Kula au unywaji ambavyo huathiri tezi na homoni zinazozalishwa mwilini.
Utofauti wa Watu hauvunji Kanuni au formula.
Ila unaweza kuathiri mchakato(reactions) wa kudhihirisha Kanuni au formula Fulani.
Kwa mfano, Ukichukua Watu Wawili ambao wanapenda Gari Aina ya V8 nyeusi kama wapendavyo au kama walivyochagua, ukawaletea Kwa pamoja, mmoja anaweza kushangilia huku akikukumbatia, mwingine anaweza akalia huku akiwa haamini. Wote wamefurahi lakini reactions ni tofauti.
Ukimfanyia MTU Jambo zuri na analolipenda lazima atafurahi. Lakini kwenye kuonyesha furaha ndipo Watu wanapishana, ndio hizo reactions unazozisema.
Ndio maana Sheria za nchi hutungwa Kwa kuangalia Kanuni za vitu mahususi na sio reactions za Watu Kutokana na utofauti wao.
Wataangalia zaidi intention, dhamiri kulingana na reactions MTU alizofanya.
Kwa mfano, Mtu ameua. Hapo watataka vithibitisho vya kuonyesha Fulani ameua, kisha wataangalia sababu ya yeye kuua, hapo ndio itakuja kaua bila kukusudia au kakusudia. Kote Huko wanaendeshwa na formula au Kanuni Fulani.
Chukua MKE au Mpenzi wa mtu uone nini kitatokea, jibu ni kuwa Wivu na maumivu ya mapenzi lazima yatokee, hiyo ni Kwa binadamu wote. Kuhusu reactions ndio huwa tofauti lakini Kanuni na formula ni Ileile.