Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Okay kwahio unazungumzia mapenzi na ndoa ambayo yana Kanuni zake; Je hizo Kanuni ni universal, Sababu ndoa (sheria na mipangilio) ni tofauti kutokana na Jamii moja mpaka nyingine..., Tukija kwenye Mapenzi ni Mtu kupenda kwahio anaweza akafuata Jamii iliyomzunguka inataka afanye nini lakini sio necessarily hayo ni mapenzi yake...Tunazungumzia Mapenzi na mahusiano ya Ndoa. Wewe unazungumzia MAISHA.
Ni vitu viwili tofauti.
Mfano sio zamani kuna kina mama walitakiwa wawe wanakaa nyumbani na kulea watoto; ingawa kuna jamii za watu wa Ancient Celtic hadi kina mama walikuwa wanakwenda vitani...; kwahio utaona sheria na nafasi ya mtu na mtu katika ndoa katika jamii moja sio necessarily sawa na jamii nyingine, vilevile individually huenda mtu asipende ila akalazimishwa (refer arranged marriages) kwahio huenda ukafurahisha jamii lakini sio nafsi
Nadhani hapo juu nimejibu huwezi kuchukua formula ya gaelic women ukaipeleka kwa persian women katika mahusiano yao..., vilevile hata katika jamii husika tuseme wahindi na arranged marriages (ingawa jamii inataka hivyo na ndio utamaduni wao) lakini bado kuna individuals kutokana na shinikizo hizo na kutokuwa na upendo wanapelekea kujiua au kuishi maisha ya masikitiko na wengine kuchukiana hata kuwekeana sumu....Maisha ni neno la Jumla ambalo ndani yake kuna mambo mengi.
Alafu Mapenzi na ndoa ni neno mahususi.
Ni Sawa useme Matunda alafu useme Embe.
Maisha hayana Kanuni Kwa sababu ni neno la Jumla lakini vitu vilivyomo ndani ya Maisha ambavyo ni mahususi (specific) vina Kanuni na formula.
Siasa zina Kanuni zake,
Uchumi unakanuni zake
Dini zinakanuni zake
Akili na tabia ya Mwanadamu inakanuni zake.
Mapenzi na ndoa vinakanuni zake.
Maisha hayana Kanuni Kwa sababu yanahusu muunganiko wa specifications zote za yanayomzunguka Mwanadamu.
Like I say..., anything with too many variables can not be constant..., mambo hayo yote sio black or white (there is lot of grey areas and there is exception to the Rule to everything...., '
Life is not mathematics, and few things have only one correct answer' na hapo naweka (Siasa, Uchumi, Dini, Akili na Tabia, Mapenzi na Ndoa)