Mwanamke niliyemsaidia na kumpenda ametoroka na mtoto wangu

Mwanamke niliyemsaidia na kumpenda ametoroka na mtoto wangu

Alikuwa agent of devil /Satan at work.rudi tu kwa yesu ndio mkombozi wako right now.
 
We jamaa nae wa wapi ww?.
Yaan hujui nyumban kwa mwanamke wako kuanzia siku ya kwanza,preg hatimaye kakid kanazaliwa HUPAJUI KWAO?.
Ur not serious,
NJOO NA UZI MWINGINE hii inaboa!.
 
kunaulakini...ukiunganisha dots unaishia kuona hii ni chai isiyo viungo. Nenda poster saa tano usiku utamkumkuta.
 
Hiki kitu kidogo sana, karipoti polisi upate mpelelezi then mtaenda kwene kampuni ya simu na kutrace top five yake then mtawakuta hao na kuhoji wawili prefarable women watatoa no yake ya sasa utampata. Yesu anashughulikia mambo mazito zaidi kama watu wanaoteswa bila kuwa na hatia eg ukatili wanaofanyiwa albino
 
Habari za Jioni Wakuu
Kuna
Vitu Ambavyo Unaweza Kukutana Navyo Katika Maisha Yako ya Kila Siku na Ukavihifadhi Katika Moyo Wako Na Kufanya Siri Kubwa Ambayo Kamwe Hutataka Kumwambia Mtu Yoyote Yule. Katika Maisha Ambayo Nimeishi Hapo Kabla ikiwa Bado Sijakutana na Huyu Mpenzi Niliyenae Sasa Nilibahatika Kuzaa Na Msichana Mmoja Aitwaye Sheila. Alikuwa Ni Msichana Ambaye Nilikutana nae Kibahati Mbaya Sana, Nasema Kibahati Mbaya Sana Kwa Kuwa Mazingira Tuliokutana Yalikuwa ni Mazingira Ya Msaada Zaidi Baada Ya Kumkuta Maeneo Ya Posta Mpya Saa Tano Za Usiku Akiwa Amejiinamia. Sikujua Nikitu Gani Ambacho Kilinisogeza Pale Lakini Nilijikuta Tayari Nikiwa Mbele Yake Huku Nikionyesha Roho Ya Ubinadamu Ikiwa ni Pamoja na Kuuliza ni lipi Tatizo Ambalo Linamsibu. Binti Yule Hakutaka Kunijibu Wala Kunisikiliza Alichokuwa Anakifanya Ilikuwa ni Kunitazama tu na Kunibinulia Mdomo Kwa Dharau Kubwa. Kusema Kweli binti Alikuwa ni Mrembo Sana na Alikuwa Anavutia Sana.. Kijana Nikaona nitangaze Msaada Huku Moyoni Nikiwa na Mipango Yangu Mingine. Kweli Baada Ya Vuta Nikuvute Binti Akakubali Kuondoka na Mimi Kuelekea Kigamboni Ninakoishi Huku Akiweka Angalizo La Kutokumsumbua Tukifika Huko. Mdomoni Nikakubali Lakini Moyoni Nilikuwa Mbali Sana.... Kifupi Siku Hiyo Hiyo Ndio Siku Ambayo tulifungua Ukurasa Wa Penzi Letu Na Tukawa Kama Kumbikumbi Kila Wakati tuko Wote Huku nikiwa Sijui Chochote Kuhusu Alikotoka na Kwa Wazazi Wa Huyu Mwenzangu.

Ndani Ya Kipindi Cha Uhusiano Wote mwenzangu Akapata Ujauzito Ambao Kila Mmoja Aliufurahia Sana Huku Mapenzi Yetu Yakiongezeka Maradufu. Sasa Kilichonifanya Kuja Hapa Kwenu Wanajamvi Wenzangu Ni Kwamba Licha Ya Kumhudumia Kwa Kila Kitu Kama Mwenza Wangu Lakini Baada Ya Kujifungua Binti Akanambia Alichokuwa Anakitaka Ameshakipata Hivyo Nisimjue na Nisimfuatilie Tena.... Mwanzo Niliona Ni Kama Utani Lakini Baada Ya Siku Chache Akatoroka na Mtoto Mimi Nikiwa Kazini na Hata Niliporudi na Kuwauliza Majirani Hawakuwa na Jibu La Maana. Na Hata Namba Zake Za Simu Kila Nikipiga Hazipatikani Tena Lakini kuna Siku NIlitumiwa Sms Kwa Namba Ngeni Akinipa Hongera Ya Kumpatia Mtoto... Lakini Nilipoipiga Haikupatikana na Mpaka Leo Haipatikani..... Ombi langu Kwenu Wanajamvi Wenzangu Nifanyeje Niweze Kuipata Damu Yangu? Imefikia Kipindi Nahitaji Kumuona Mwanangu Lakini Sijui Wapi Nitampata Huyu Mwanamke.

Msaada Wanajamvi Wenzangu
umezaa na jini duh......walai nakwambia yn ni jini
 
Duuh tamaa mbaya sn hiz, zimekuponza!! we umeokota tu mtu huko hujui story yake wala nn, wew tyr umeshawaza ngono juu yake!! aah sis hp hatuna cha kukusaidia labda nenda Bango TBC1 utoe taarifa hizo, labda unaweza kufanikiwa kumpata. Tofaut na hapo nenda kwa Mungu umlilie akuhurumie, akusamehee na akufanyie wepes kweny hilo basiiii. Hakuna lingine!!

Ahsante Mkuu
 
Umesema mtoto umemkuta posta kaJINInamia ??? Unamsemesha anakutazama na kubenua mdomo kwa dharau ?? Halafu anaitwa SHEILA ?? Haya bana pole na maswahibu

Soma Vizuri Uzi Mkuu... Au Ulitaka Niandike Kila Kitu... Hivi Mtu Uliyeishi Naye na Kuzaa naye Huwezi Kujua Jina lake? Siamini Kama Umeshindwa kuelewa kuwa nazungumzia Past tense mkuu
 
Hiki kitu kidogo sana, karipoti polisi upate mpelelezi then mtaenda kwene kampuni ya simu na kutrace top five yake then mtawakuta hao na kuhoji wawili prefarable women watatoa no yake ya sasa utampata. Yesu anashughulikia mambo mazito zaidi kama watu wanaoteswa bila kuwa na hatia eg ukatili wanaofanyiwa albino

Ahsante Mkuu Hakika Umenipa Nguvu na Imani ya Kuipigania Damu Yangu.... Ubarikiwe Sana
 
kunaulakini...ukiunganisha dots unaishia kuona hii ni chai isiyo viungo. Nenda poster saa tano usiku utamkumkuta.

Siamini Kama Hata Ww ni Great Thinkerz.. Lakini Naongea na Mungu Kwa Kuwa Ndiye Ajuae Sio Binadamu...
 
We jamaa nae wa wapi ww?.
Yaan hujui nyumban kwa mwanamke wako kuanzia siku ya kwanza,preg hatimaye kakid kanazaliwa HUPAJUI KWAO?.
Ur not serious,
NJOO NA UZI MWINGINE hii inaboa!.

Inaboa Ki vipi Mkuu... Labda Nikuulize Umesoma Majibu Yangu kwenye baadhi Ya Comment? Binti Alinikutanisha na Mama Mmoja Hivi Akanambia Huyo Ndiyo Anapajua Kwao na Hata Likitokea Tatizo Muone Huyo na Hata Binti Alipokuwa Mjamzito Yule Mama Alikua Anakuja Kwangu.... Tatizo Mmezoea Kupuuza Thread Za Watu... Great Thinkerz Hawezi Kuwa na Upeo wa Aina Hiyo
 
mama haibi mtoto...mwache atamrudisha au mtoto atakutafuta
 
Soma Vizuri Uzi Mkuu... Au Ulitaka Niandike Kila Kitu... Hivi Mtu Uliyeishi Naye na Kuzaa naye Huwezi Kujua Jina lake? Siamini Kama Umeshindwa kuelewa kuwa nazungumzia Past tense mkuu

Umeshindwa kunielewa ,anyway all the best
 
Back
Top Bottom