Mwanamke tegemezi asiye na Kazi huwezi sema anakuheshimu au kukutii. Heshima inatoka kwa mtu anayejitegemea Nje ya hapo tegemea Unafiki.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MWANAMKE TEGEMEZI ASIYE NA KAZI HUWEZI SEMA ANAKUHESHIMU AU KUKUTII. HESHIMA INATOKA KWA MTU ANAYEJITEGEMEA NJE YA HAPO TEGEMEA UNAFIKI

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwa Sisi tusiopenda unafiki na tunaojua hulka na akili ya binadamu. Kamwe hatutazamii heshima yoyote kutoka kwa mtu asiye na Kazi, mtu Maskini na mtu asiye na chochote.

Linapokuja suala la mahusiano, Sisi Watibeli tunapendelea kuingia kwenye mahusiano na wenza wanaojishughulisha na wenye uwezo WA kujitegemea. Binti au kijana hawezi kukubali kuingia kwenye uhusiano na mwenza tegemezi na asiye na Kazi Kwa sababu tunafahamu hakunaga mapenzi ya KWELI Wala heshima ya kweli kutoka kwa Watu wa dizaini hiyo.

Mtu asipojipenda au kujiheshimu unategemea akupende au akuheshimu wewe?
Kufanya Kazi ni Moja ya nguzo kuu inayoonyesha Fulani anajiheshimu na anajipenda.
Mtu kama hafanyi Kazi na hataki kujishughulisha ni wazi kuwa hajipendi na hajiheshimu.

Mwanamke ili akupende na akuheshimu lazima mwenyewe awe anajipenda na kujiheshimu.
Mwanamke kujipenda na kujiheshimu kwake sio kwa kujipamba pekee Bali kuweza kujisimamia, kujishughulisha na kujitegemea kwa Kazi halali zisizodhuru UTU wake.

Haiwezekaniki mwanamke atake umpende na kumheshimu kuliko anavyojipenda yeye.

Kijana usije ukajitesa ukidhani utapewa Tuzo kwa kuhangaika kumhudumia mtu asiyeweza kujihudumia. Kumpenda mtu asiyeweza kujipenda. Hayo ni matumizi mabaya ya Upendo. Ni dalili kuwa hukupata mafunzo mazuri kuhusu kuwa MWANAUME.

Hakunaga heshima au upendo utakaoupata kwa mwanamke asiyefanya Kazi na asiye jitegemea. Never ever. Hakunaga kitu Kama hicho.

Mtu anayeweza kukuheshimu na kukutii ni Yule ambaye anajiheshimu.
Mwanamke mwenye Kazi hata kama ni kuuza mandazi,mama Ntilie, kuuza Duka, saluni n.k.
Huyo mnaweza mkaa mkazungumza Jambo kama watu wazima.

Ukiona mwanamke anakazi na a ajitegemee na bado anakupenda na kukusikiliza elewa kuwa huyo haigizi.

Hawezi kukupa heshima za uongouongo.
Hawezi kukupa mapenzi ya kitapelitapeli.

Mwanamke asiyejitegemea akikupa Mapenzi yake ujue umeyanunua na malipo yake ni wewe umpe pesa. Hakunaga tofauti yake na wale wa pale kimboka wauza Nyapu.

Mwanamke ambaye Kulala naye anataka umpe pesa ya sabuni huyo mkimbie kama Ukoma. Labda kama upo naye kama wale madadapoa wa pale Buguruni. Hapo Sawa.

Lakini kujifanya unamchumba sijui Mwanamke unayemuita Mke lakini anatabia za kitapelitapeli, tegemezi na Umalaya wa kukuuzia Nyapu alafu kwako unaona ni kawaida ujue kichwani wewe nati zimelegea.

Unakaa na mwanamke mwaka mzima, wewe tuu ndiye unapeleka zawadi lenyewe Linatoa tuu meno. Halijawahi kukununulia zawadi nawe upo comfortable Kabisa my friend huna mwanamke HAPO!
Hakuna kitu hapo!
Bora ujiunge na Lile Genge la kina Liverpool VPN na Intelligent businessman la Kataa ndoa maana unapoteza Muda wako tuu.

Alafu Kutafuta heshima kwa binadamu wasiohuru(tegemezi) ni dalili wewe sio Mwanaume unayejitambua. Ni Kutafuta viheshimu uchwara visivyo na kichwa Wala miguu.
Hivi mtu asiyejitegemea atakupa heshima inayostahili kweli au unafiki nafiki tuu. Atakuwa Huru kuliko kuendekeza njaa na shida zake?

Anyway! Mimi acha nimalizie Makande yangu.
Binti zangu fanyeni Kazi.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hii ni hiari, Mtume Paul anasema willingly submissive. Sio lazima atii
 
Hiyari ndio mapenzi yenyewe.
Kwenye mahusiano ya Mume na Mke. Kila siku nawaambia jukumu la kupendana ni la wote. Ingawaje Paulo( sio mtunga Sheria) anaposema mke Atii anarejelea uleule upendo ambao mwanaume anao kwa Mkewe

Mwanamke tegemezi Hana hiyo willingly submissive ila atalazimika kukutii(kukuogopa) kwa Sababu ya shida na Umaskini wake
 
Hivi inakuaje unakaa na mke bila ya yeye kushiriki miradi miwili ya msingi sana .

Mwanaume fuga kuku asubuhi unapoenda kazini lisha kuku zako 20 wawekee maji..mke mpe kazi ya kusafisha Banda na kuokota mayai ukirud kazini mchana unaweza kumwachia akauze genge la matunda ..easy very easy maisha utayaona marahisi tu .
Mtaji hapo ni km laki tano tu..

Pmj tujenge taifa letu
 
Hivi inakuaje unakata na mtu bila miradi miwili ya msingi sana .

Mwanaume fuga kuku asubuhi unapoenda kazini lisha kuku zako 20 wawekee maji..mke mpe kazi ya kusafisha Banda na kuokota mayai ukirud kazini mchana unaweza kumwachia akauze genge la matunda ..easy very easy maisha utayaona marahisi tu .
Mtaji hapo ni km laki tano tu..

Pmj tujenge taifa letu

Tatizo wanaume wanajua Kabisa wanawake hawawapendi ndio maana wanaogopa kuwawezesha
 
Hiyari ndio mapenzi yenyewe.
Kwenye mahusiano ya Mume na Mke. Kila siku nawaambia jukumu la kupendana ni la wote. Ingawaje Paulo( sio mtunga Sheria) anaposema mke Atii anarejelea uleule upendo ambao mwanaume anao kwa Mkewe

Mwanamke tegemezi Hana hiyo willingly submissive ila atalazimika kukutii(kukuogopa) kwa Sababu ya shida na Umaskini wake
Mwanamke alikuja kwa mahitaji ya mwanaume. Mwanamke hakuhitaji mwanaume, kwanini? Mwanamke hakuwepo hivyo asingeweza kuhitaji mwanaume. Alipokuja alitakiwa awe submissive ili aendane na mahitaji ya mhitaji. Akapewa uhuru wa kuchagua
 
MWANAMKE TEGEMEZI ASIYE NA KAZI HUWEZI SEMA ANAKUHESHIMU AU KUKUTII. HESHIMA INATOKA KWA MTU ANAYEJITEGEMEA NJE YA HAPO TEGEMEA UNAFIKI
Na tangiapo mwanamke anatakiwa ategemee toka kwa mume.

Siku mwanamke akianza kukuletea chakula ndani hesabu maumivu. Siku Adamu alipoletewa chakula na mke wake Hawa/Eva shida ilianza ndani ya nyumba yake.

Mwanamke anatakiwa awe tegemezi kwa mahitaji na busara toka kwa mume.

Ila vile tunajaribu kukwepa majukumu yetu wanaume tunaokoteza sababu kuwatumikisha wanawake. Mwanamke kazi yake kukuzalia watoto basi.
 
Unakaa na mwanamke mwaka mzima, wewe tuu ndiye unapeleka zawadi lenyewe Linatoa tuu meno. Halijawahi kukununulia zawadi nawe upo comfortable Kabisa my friend huna mwanamke HAPO!
Hakuna kitu hapo!

Robert Heriel
Taikon master
Kwa sasa Dar es salaam
Ngoja waje...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom