Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Wanawake ukipata fursa yoyote kwenye maisha yako usiiache eti kisa kuogopa mwanaume au kuwaza kuwa mbali na huyo mwanaume. Wanawake jifunzeni kujiweka wa kwanza kwenye kila kitu kwani hao wanaume hujiweka wao wa kwanza kabla yenu.

Ikitokea mwanaume kapata fursa labda ya kusoma au kazi mbali na mlipo na ikawa inawaweka mbali hawezi shindwa kwenda kisa kuwa mbali na wewe, hata kama anakupenda namna gani atajitahidi aende huku anakufikiria wewe ila kaenda.

Hapo kuna wanaume wa aina mbili, wakipata fursa kuna wanaokwenda na baadae kutafuta namna ya kukuweka kwenye hayo maisha yake mapya, na kundi hili si wengi. Kundi la pili ni wanaume ambao wakienda kweye fursa wanazopata ndio wameenda wewe unakuwa sio level zake tena anakusahau, sasa kwa nini wewe usijiweke wa kwanza pia kama wao wanavyofanya?

Wanawake huwa wana ujinga fulani, anaweza acha kwenda kazini alikopata kisa kuogopa kuvuruga mahusiano na mwanaume wake, na mara nyingi huwa anakuja kukumbuka bora angeenda kuliko hayo yanayomkuta kwa wakati huo lakini anakuta kashachelewa. Kama huyo mwanaume ni wako nenda na ukifanikiwa rudi muendelee.
Ushauri wako unapoteza. Huwezi kutoa ushauri wa jumla jumla namna hiyo kwa situation za watu wawili. Wiki iliyopita kuna dada mmoja wa kizungu ameacha kazi nzuri kweli kweli, na yenye mshahara mzuri. Alikuwa anafanya ubalozini. Nilipomuuliza kisa akaniambia wamefanya majadiliano na mumewe wakakubalina awe anabaki nyumbani kuangalia watoto! Wewe ushauri wako umeutoa huku upeo wako wa kuona mambo ukiwa umefungiwa ndani ya box!
 
Wanaume tumebaki wachache sana na kila siku tunapungua..ila fursa ni nyingi mno nakila siku zinatokea mpya ..sasa wanawake shauri yenu mtakuja kulia sana mkiacha mwanaume kisa fursa..
 
Back
Top Bottom