Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtafungwa 🤣Me nishaila kitambo🤣🤣 Utapambanaa
Kuazima nguo kwa mashosti zakeMWANAMKE ULIYEOLEWA, USIFANYE MAKOSA YAFUATAYO: (1)
Na. John- Baptist Ngatunga
___________________________
Kwa kawaida, kila binadamu anayafanya makosa. Lakini yapo makosa mengine ambayo pamoja na ubinadamu wetu hatupaswi kuyafanya. Tunatakiwa kuwa makini sana kuyaepuka ili tusikutwe na lawama. Ndivyo ilivyo pia kwa Mwanamke aliyeolewa kujiepusha sana na makosa yafuata:
1. KUOMBA HELA KWA MWANAUME MWINGINE
Kuna baadhi ya Wanawake wamekuwa la hulka ya kupenda kuombaomba Pesa kwa Wanaume tofauti na Waume zao. Akilini mwao wanaamini kuwa Mwanaume anaweza akawasaidia tu kama Msaada. Hii inatokana na Ukweli kwamba wengi wa Wanawake hao hawajui madhara yanayoweza kutokea kutokana na tabia hii.
Baadhi ya madhara yatokanayo na kufanya hivo ni haya yafuatayo:
Kwanza; unaiharibu sifa, utu na heshima ya Mume wako kwa kumdhalilisha kwamba ni Masikini asiyekuwa na uwezo wa kukuhudumia wewe na kukidhi au kukutimizia mahitaji yako. Kwa kufanya hivyo ni sawa sawa pia na kumtangaza Mume wako kwa Wanaume wengine kwamba yeye ni Dhaifu na hivyo umewasaidia Wanaume wengine kuyajua madhaifu ya Mume wako ya kushindwa kukuhudumia wewe.
Pili; unamdhalilisha Mumeo kwa kuoa Mwanamke 'Ombaomba' na automatically umejidhalilisha pia wewe Mwenyewe kwasababu huyu Ombaomba ninayemzungumzia hapa ni wewe Mwenyewe.
Tatu; Asilimia zaidi ya Sitini (60%+) ya Wanaume, hawawezi kumsaidia Mwanamke bila kutegemea kupata kitu kutoka kwao. Kumbuka huyo Mwanaume unayemwomba Pesa sio Ndugu yako. Ni Mwanaume tu ambaye hana kizuizi chochote cha kidamu kitakachoweza kumzuia pindi na yeye atakapoamua kukuomba Mwili wako.
Ni lazima tu na yeye atahitaji 'Marejesho' ya Mwili wako kwa Hela anazokupa. Wanaume ni wazuri sana katika Masuala ya biashara ya win win situation (yaani sote tunufaike).
Nne; utakuwa umewaambia Wanaume hao kwamba Mume wako anatakiwa asaidiwe Majukumu yake ya kukuhudumia wewe kwasababu hayajui ipasavyo Majukumu yake na wajibu wake kwako au ameshindwa kuyatimiza Mahitaji yako.
Na kitendo cha Wanaume au Mwanaume huyo mwingine kukupatia hela, kinafungua Rasmi ukurasa wa Mume wako kusaidiwa majukumu yake na Wanaume wenzie. Na akisaidiwa Majukumu ya Mahitaji yako ya kawaida, automatically anatakiwa asaidiwe pia na Majukumu ya kukutimizia Mahitaji yako ya kihisia.
Hii yote ni kwasababu haiwezekani "Ng'ombe alishwe na John, maziwa akamue Abdul". Hayo yote utakuwa umeyasema wewe kwa matendo yako ya kuwaomba Hela Wanaume hao wengine nje ya Mume wako.
Kama kuna shida yoyote ya Msingi, inayohitaji Msaada wa kifedha nje ya Familia yako, ni Heri Mume wako ndiye aende kuomba au kukopa hizo fedha kwa Wanaume wenzie.
2. KUTOKA 'OUT' NA MWANAUME MWINGINE
Usitoke out na Mwanaume yeyote nje ya Mume wako. Hata kama Mwanaume huyo ni Shemeji yako au Rafiki wa Karibu sana wa Mume wako. Unaweza ukakiona au kukichukulia kuwa ni kitu cha kawaida tu kwamba hamjaenda sehemu ya Faragha na mlikuwa mnaongea tu mambo ya kawaida au mbona ni Shemeji yako na hawezi kukuambia chochote 'kibaya'.
Lakini Mume wako akigundua au akiona ni mwendelezo au na ni Mazoea unatengeneza ya kufanya hivo, anaweza asiipende hiyo Tabia na ukawa unamkwaza na asikuambie kwasababu anaweza akaanza kuwa mdadisi juu yako.
Usitake mpaka siku Mumeo akukaripie au akuoneshe kuwa haipendi hiyo tabia. Ukisubiri mpaka afanye hivo, ni ishara tosha utakuwa umeionesha kwamba huwezi kujiongeza.
Wakati mwingine kitendo hicho kinaweza kikamtengenezea Maswali Mumeo na kutokana na Asili ya Wivu wa kila Mwaume kwa Mwanamke, Mume wako anaweza akaanza kutilia Mashaka ukaribu wenu na kutokana na Mashaka hayo kwako na kwa huyo Shemeji yako, Mumeo anaweza akaanza kukufuatilia kimya kimya bila kukuuliza au kumfuatilia huyo Ndugu yake au Rafiki yake kimya kimya.
Hata kama Mume wako hana 'wivu wa kihivo' epuka sana Mazoea ya kufanya hivo. Wanaume wote kwa Asili yao ni critical na reasoning. Mazoea yanaweza yakatengeneza tabia ambayo baadae ikamfanya Mumeo awe suspicious na akaanza kudevelop tabia ya kukufuatilia na kukuchunguza na vitu vingine ambavyo havikuwa Akili mwake.
Lakini pia, Mitoko Mitoko kama hii imewafikisha Wanandoa wengi sana katika mazingira ambayo hawakuwahi kuwaza kama yangeweza kujitokeza mambo mengine makubwa ambayo hawakuyawaza. Halafu mwishowe lawama anatupiwa Shetani au yanakuja maneno, "Ningejua nisinge......"
Itaendelea.......
Acheni kujificha kwenye mwamvuli wa "kuwachukia wanaume" mimi siwachukii wanaume bali nachukia mitazamo ya ajabu dhidi ya wanawake, lazima niseme ukweli tu hata kama hamtaki kuusikia tofautisha kati ya asili na mfumo kandamizi uliotengenezwa na wanaume, kiuhalisia misogynists ndio wako wengi na ndio wabaya na wa kuogopwa zaidi kuliko feminists tofauti na mnavyosema humuDada'angu una hasira sana na wanaume!
Huyo uliyegombana nae kwa sababu amekutaka uishi kadiri ya asili inavyotaka (mke kuwa chini ya mume) huku hutaki kwa sababu unazo sababu zako (kazi nzuri mshahara ect) jitenge nae kidogo utulize akili maana utawehuka.
Mmh mambo ya kiswazi kabisa haya..kule tandale kwa tumboKuazima nguo kwa mashosti zake
Kwa mwanaume kuna uzi wake ... tofauti. ila mengi ya hayo ana ruhusiwa tu.Waambie na mume wa mtu hatakiwi kufanya yapi?
Ama huku ni exemptions kote.
Kwann uyafanye sasa wakati mmeo anakutosheleza huoni una mpa shetani nafasiLakini cha ajabu utakuta mwanaume anaambiwa ni sawa yeye kufanya hayo na wanawake wengine, ukiuliza ni kwa misingi gani hutapewa jibu la maana zaidi ya kuambiwa usishindane na mwanaume na kuitwa majina ya ajabu ajabu sijui feminist sijui single mother, nonsense!!
kukubali kuchart PM .Noted...
Umeandika vema, ila usije ukaongezea kuwa hatutakiwi Ku log in jf.
Sasa kama kichwa cha familia tu kinafanya hayo imagine huyo anayeongozwa atafanya niniKwann uyafanye sasa wakati mmeo anakutosheleza huoni una mpa shetani nafasi
Naunga mkono[emoji1666]Dada'angu una hasira sana na wanaume!
Huyo uliyegombana nae kwa sababu amekutaka uishi kadiri ya asili inavyotaka (mke kuwa chini ya mume) huku hutaki kwa sababu unazo sababu zako (kazi nzuri mshahara ect) jitenge nae kidogo utulize akili maana utawehuka.
No. 1&5 zina nini mkuu?Namba 1&5