Mwanamke uliyeolewa, usifanye makosa haya

Mwanamke uliyeolewa, usifanye makosa haya

Sasa umeandika nini hapo cha kufanya nijadiliane na wewe zaidi ya kuleta shobo tu, acha matusi andika hoja tuanze mjadala uone kama nitaomba poo, nonsense
Foolish niandike hoja kwa hoja gani uliyoisema
 
Mamayer unaleta shobo kwa dume ? angalia utakosa rinder kyumer mmoja wewe
Kati ya mimi na wewe nani kaanza kumshobokea mwenzie, yani wewe ndio umeanza kuniquote pumba halafu unasema mimi ndio nakushobokea, hizo stress zako kazimalizie kwa mabwana zako acha shobo na mimi tutusa wewe
 
Hiyo namba 1 wanawake hawawezi kuzingatia, amini nakwambia mleta mada!
 
Nimtendeje Mungu dhambi kubwa namna hii? Ninaweza kumficha mke wangu wala asijue kama nilizini, na zamani hizo kabla sijamjua Mungu nilizini sana na wanawake wengi, wala hakugundua, unaweza kumficha mke wako au mume wako, ila huwezi kumficha Mungu, anakuona tangu unatongozana hadi unaenda kufanya uzinzi, anakuona, anakupenda na hataki ufanye uzinzi kwasababu anajua madhara ya uzinzi. Mungu anataka ushirika na sisi, tuishi maisha matakatifu, tumwabudu yeye, tufanye kazi yake ili na yeye afurahie kuwa na sisi kama watoto wake, anapoona tunakengeuka anakwazika na anakasirika. acheni dhambi, hata leo ukiona wazo la uzinzi linakuja kimbia, achana nalo.

ni kweli maisha wakati mwingine yanaweza kuwa magumu, hasa kwa wanawake, unakuwa hauna pesa, hauna kazi, hauna msaada, hauna njia ya kutatua tatizo fulani, hauna furaha, umeachwa na mume, haujaolewa, umefiwa na mume, upo katika mazingira mbalimbali. lakini jua kwamba mazingira yote hayo Mungu anayajua, na hiyo sio sababu ya wewe kufanya uzinzi. na kama upo katika kifungo cha uzinzi yaani kila ukijitahidi kuacha unashindwa, Mungu akusaidie, lipo tumaini, ukimkimbilia Mungu anaweza kubadilisha hali hiyo ukawa na solution, pengine ni kwasababu tu hujakabidhi maisha kwa Yesu, jaribu leo, bado wokovu upo, Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya hilo, kutusamehe dhambi na kutotoa kwenye vifungo vyote, kifungo cha dhambi ni kimojawapo, amebadilisha wengi. mpe maisha yake ili akukomboe, uwe mtoto wake na uishi kama mtoto wake.

Maana neema ya Mungu imefunuliwa kwa wanadamu nayo yatufundisha kukataa uovu na tamaa zote za dunia hii, tupate kuwa na kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa tukilitazamia tumaini lenye baraka (la ujio wa Yesu Kristo) na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu.

Yesu anakuja, wakati watu wasemapo kuna amani, uharibifu utawajia, hata kipindi cha Nuhu watu walioa na kuolewa, walikula bata, hata siku ile Nuhu anaingia kwenye safina, wakaangamia. Hata wakati wa Lutu kabla ya kuteketezwa sodoma na gomorah, watu walikula na kunywa, walioa na kuolewa, walizini mno hadi kulawitiana, hadi moto wa kiberiti ulivyowashwa. Ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Yesu Krsto. Mungu akusaidie msomaji utambue hili, YESU ANARUDI, YESU ANARUDI, YESU ANARUDI, yupo malangoni, dalili nyiiingi zimeshaonyesha kwamba tupo katika siku za mwisho, HERI WAZIFUAO NGUO ZAO KATIKA DAMU YA MWANA KONDOO WAPATE KUUENDEA ULE MJI. hata wewe uliyekuwa umeokoka ukarudi nyuma, ungalipo mzima ni neema ya Mungu, anataka ubadilike urudi tena, mrudie Mungu wako kwa machozi kama mwana mpotevu, tubu dhambi zako, atakusamehe na utakuwa mpya tena, usipoteze hii nafasi, inaweza isiwepo tena, wengi walipanga mipango mingi, wakaamka asubuhi wakagongwa na gari hata kabla hawajatubu, wameenda na dhambi zao, Yesu alisema kesheni basi kwa kuwa hamjui siku wala saa (ya aidh akuja kwake au kufa kwako).

kwenu ninyi ambao hamjaokoka, hivyo hivyo ulivyo Mungu atakupokea na atabeba mizigo yako yote, sali sala hii pamoja na mimi:

Eee Mungu wangu, mbele zako mimi ni mwenye dhambi, ninaamini ulimtoa Yesu Kristo alikufa kama kafara kwa ajili ya ukombozi wangu, naomba unisamehe, uniokoe kuanzia leo, mimi niwe mali yako, futa jina langu katika Kitabu cha hukumu, andika jina langu katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo Yesu Kristo, Katika Jina la Yesu! Amen.

hivihivi kimchaezo mchezo umeshaokoka, acha dhambi, kimbia dhambi na jiunge na wale waliookoka ili mmwabudu Mungu pamoja. Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom