Mwanamke uliyeolewa, usifanye makosa haya

Kuazima nguo kwa mashosti zake
 
Angalau nimeweza hiyo namba 5. Nahitaji Tuzo.
 
Acheni kujificha kwenye mwamvuli wa "kuwachukia wanaume" mimi siwachukii wanaume bali nachukia mitazamo ya ajabu dhidi ya wanawake, lazima niseme ukweli tu hata kama hamtaki kuusikia tofautisha kati ya asili na mfumo kandamizi uliotengenezwa na wanaume, kiuhalisia misogynists ndio wako wengi na ndio wabaya na wa kuogopwa zaidi kuliko feminists tofauti na mnavyosema humu

Hata wazungu nao huwa wanaaminisha dunia kwamba ni asili mtu mweupe kumtawala mtu mweusi kwa sababu tu mtu mweupe ni tajiri na mtu mweusi ni masikini, na siku zote tajiri humtawala masikini lakini kiuhalisia hiyo siyo asili bali ni mfumo tu ambao wameutengeneza wao wenyewe, na kuupandikiza vichwani mwa watu weusi ili wajione inferior na wakubali kutawaliwa kirahisi bila ubishi

Hata pale ambapo watu weusi walianza kudai uhuru wa kujitawala wenyewe bado watu weupe wakaleta propaganda kuwa "tuliwaambia hawawezi kujitawala wenyewe ona sasa nchi zao bado ni masikini na viongozi wao ni mafisadi", ukiniambia kuwa utawala wa mwanaume kwa mwanamke uko kibiblia basi bila shaka utakuwa hujasoma kuhusu habari ya kina Shem, Ham, na Jafet na maneno waliyotamkiwa na baba yao Nuhu, sasa hayo wanayofanya watu weupe dhidi ya watu weusi yana tofauti gani na wanayofanya wanaume kwa wanawake
 
Kwann uyafanye sasa wakati mmeo anakutosheleza huoni una mpa shetani nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…