Mwanamke unawezaje kuishi kwenye ndoa na mwanaume ambae hauna hisia nae?

Kwanza mwanamke anapaswa kujenga hisia kwa mwanaume aliyemfuata na kumtongoza, wewe unaanzaje kuwa na hisia na mwanaume ambaye hana hata mpango na wewe, mtoa post kanishangaza sana. Sasa îtabidi utamaduni mpya wa wanawake kutongoza wanaume na kuwalipia mahali uanze ili mpate mliokuwa na hisia nao. Vuta subra ipo siku utampata mtu sahihi
Dah DUNIA kweli haina usawa watu wanakesha kuomba kupata mme kama wako aisee wanakosa wanapata vivuruge ..nawe Mungu kakupa alie sahihi kwako lakini huna hisia nae ..Mungu ni mwema ipo siku atanipa kama huyo .
 
Mapenzi ni hisia, huwezi mfundisha mtu kuwa na hisia na mtu..kama hana hana tuuuu na ameshaingia ndoani hana budi kulinywa tu na kusubiria kifo..
 
Yani unatakiwa uwe kisutu kwa kesi ya uhujumu uchumi,yani unachukua hela zake tu hakuna return,au jamaa dogo zege
Mimi nifanye nini sasa na njaa inaniuma hahaa ila kiukweli najitahidi sana kukaa mbali nae tatizo huwa tunajikuta tu automaticay tumekutana
 

Alikudanganya nani?

Wangekuwa wanamkubali kila mwanaume
 
wewe si umekataa kumpa ......... .... wakati unajua kabisa .............!! leo ndio ilikua nafasi nzuri kabisa kwa ............. .....!!

Ngoja nikuitie babu Asprin

Utakoma leo, chapachapa denguuu leeeloooo..... aahahahahhaaa
 

Daaah,umenipa hasira sana.....!

Nakiandika yaliyo moyoni mwangu,baada ya kusoma uzi huu,itakuwaje sijui...?!
 
Mnhhh uifurahie ndoa yako?? mwambie mumeo aongeze mke mwingine😂😂😂😂,kama hautataka tena akuguse?😂😂😂...sipati picha utakavyojituma😂😊
 
@manengelo Ahahhahha namfanyia kweli.

Pesa ya matumizi kwa mwezi mzima nampa yeye ashike na apange kuhusu chakula.

Siku akiniuliza tule nini mume wangu huwa nacheza na saikolojia yake namuambia "wife sitakiii utata nilisha kuambia mambo ya chakula wewe ndo msimamizi unapanga tule nini nini upike sasa unaniuliza mimi nina utaalamu gani?"

Basi hapo anaondoka kwenda jikoni akiwa anatabasamu kufurahia kuona nimempa cheo katika sekta yake na ataenda kupika menyu ya kufa mtu kwa sababu kashaona ameaminiwa so hataki kuniangusha.

Au kama ishu za pesa ya akiba basi namuambia mfano wife laki tano hizi apa tuziweke mie siwezi kutunza pesa hasa ziweke wewe,mimi mara nimenunua hiki na hiki,aaaaah hapo wife nikimpa hawazi upuuzi wa kununua nguo au kitu kingineee baali atajihaidi aitunze hyo hela ili kulinda ule uaminifu niliompa.

Katika ishu za kawaida huwa namtania sana yaani mpaka anavunjika mbavu kwa kucheka,some time akiniona tu hata kama sijaongea anachekaa ,nikimuuliza ananiambia nakumbuka kituko chako cha siku fulani.

Yaani nina mengi ya kuandika kuwafunza wanaume wenzangu ila kiufupi hata niwe mbali nae bado ataendelea kunikumbuka tu.

Namshukuru Mungu kunipa kipaji cha kumhendo mke wangu.
 


safi sana sana kakake.. mwee! niishie hapa
 
Hapa ndipo uvumilivu unavyoingia kwenye ndoa.
 
Shida hii kuwakuta wanawake wengi, unakuta ana boyfriend wake wa miaka 4-5 sema jamaa hana nia ya kumuoa ila wote wanapendana sasa picha inaharibika anatokea jamaa mwingine pembeni ndani ya miezi 3-6 jamaa anatangaza ndoa mdada akiangalia umri unaenda na jamaa anaempenda hafanyi maamuzi hivyo mwanamke anakubali kuolewa na jamaa aliejuana nae miezi michache matokeo yake wanakuja kuleta uzi kama mleta mada hapa
 
Kwa hiyo kwa nini ukubali kuolewa na mtu usiyempenda??
Hujielewi... .... ..
Mwambie halafu uone atakubali kuishi nawe au atasanda!
Ila ujuwe tu kuwa ni bora kuishi na anayekupenda kuliko kuishi na unayempenda bila kuwa na uhakika wa wewe kupendwa!
 
Hahaha ungeolewa tu tukule mpunga we ukateseke peke yako
 
hata kama humpendi kimapenz kwa nn unawaza kumsukumaa..?kwani we ni rihana?..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…