Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Next King

Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
32
Reaction score
70
Naomba ushauri wako kati ya hawa wanawake wawili yupi anaweza kuwa sahihi kwangu?

MWANAMKE WA KWANZA
Ana elimu ya darasa la saba lakini ni mjanja sana maana hata text za kiingereza anajua kusoma na kuandika baadhi ya maneno, amezaliwa 1988 (miaka 36), ana watoto wawili wote wa kike - sio watoto wangu.

Mrefu, mweupe, ana akili ya maisha, anafanya kazi private sekta, na mjasiria mali (anajishughulisha na ufugaji kuku), amepanga anaishi na mtoto huyo mdogo (2 years) na dada wa kazi. Ni msafi, anajipenda, anajua maisha, anaweza ku-plan maisha yake (so far ana kiwanja, na bati kanunua) kifupi ni hayo. Niliwahi kuwa na mahusiano nae hapo awali, baadae nilipotezana nae, nilipokuja kukutana nae ndio akawa na huyo mtoto. Wazazi wake wote wamefariki.

MWANAMKE WA PILI
Ana elimu ya form 4 (division 3 point 25), ni wa mwaka 2000, ana mtoto wa miaka 4 (mtoto wa kike), anaishi na babu na bibi yake - (kwa upande wa mama yake) kwa sababu baba na mama yake walishafariki. Mrefu wastani, maji ya kunde, hana akili ya maisha zaidi ya kujua kupika na kufua na yale mengine ya chumbani (chumbani ni wa moto), ni tegemezi kwa asilimia 100% hata ukimueleza kuhusu kufanya biashara au kumtafutia shughuli ya kufanya anasema yeye kwasasa anataka tu ku-enjoy maisha na kikubwa azae alee familia.

Kwa jinsi alivyo hana matumizi mazuri ya fedha kwa kile apewacho, sijui kama ni akili ya utoto au laaa.

Huyu wa 1988 na huyu wa 2000 tofauti yao ni miaka 12, kwa maana mmoja ni 36 years, na mmoja ni 24 years.

Naomba toa ushauri wako kuhusu mwelekeo wa nani kati ya hawa wawili anaweza kuwa mama bora wa familia.

Akina dada na wamama wa hapa JF, na nyie wanaume kulingana na uzoefu wenu wa maisha , TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.
 
Hakuna mke hapo,tafuta ambaye hajazaa,kuhusu akili na hela mtatumia za kwako

Narudia usioe singo maza
mimi nimekiwasha kwa single mother wa watoto sita, mara 2 tu kaanza kulia eti ana ujauzito😭😭😭
Screenshot_20241128-161946.jpg
 
Back
Top Bottom