Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Sikiliza moyo wako mzee. Mwanamke kikubwa anakuheshimu,anakusikiliza,anaridhika na hali yako kiuchumi uliyo nayo kwa wakati husika, kikubwa kulivyo vyote HAKUSALITI NJE lakini pia kama sio mchoyo kwako.
 
Mkuu maelezo niliyoweka hapo nadhani yapo very clear. Imagine ndio wewe sasa na yakupasa ufanye maamuzi kwa kuzingatia hiyo scenario, utafanyaje mkuu. ushauri wako ni muhimu sana
Yawezekana hata wewe hawakuelewi hata kidogo, jichunguze mzee, mpaka sasa hakuna aliyekubali kukubebea mimba?
 
Sikiliza moyo wako mzee. Mwanamke kikubwa anakuheshimu,anakusikiliza,anaridhika na hali yako kiuchumi uliyo nayo kwa wakati husika, kikubwa kulivyo vyote HAKUSALITI NJE lakini pia kama sio mchoyo kwako.
mkuu naheshimu sana mawazo yako kama GT mwandamizi wa JF lakini naomba uthibitishe kwenye hili swala moyo unahusika?

njoo na ushahidi

Kazi za moyo ni hizi
Screenshot_20241129-121937.jpg
 
mkuu naheshimu sana mawazo yako kama GT mwandamizi wa JF lakini naomba uthibitishe kwenye hili swala moyo unahusika?

njoo na ushahidi

Kazi za moyo ni hiziView attachment 3165117
Moyo
mkuu naheshimu sana mawazo yako kama GT mwandamizi wa JF lakini naomba uthibitishe kwenye hili swala moyo unahusika?

njoo na ushahidi

Kazi za moyo ni hiziView attachment 3165117
Jibu langu si la kisayansi lakini; moyo hubeba tafsiri ya hisia,upendo,hasira,huzuni,furaha n.k. Tafsiri hiyo inakuja kuonekana katika matokeo kwa nje,utaonekana au utajihisi kumpenda zaidi fulani kuliko fulani,yawezekana wote wakawa na sifa na vigezo sawa ila ukahisi kuwa unampenda zaidi fulani kuliko fulani au unamchukia zaidi fulani kuliko fulani na ni katika muktadha huo na mimi nimesema ausikilize moyo wake.
 
Wanawake wote ni sawa awe na PhD awe ni darasa la 7B. Ww cha kushukuru tu mwanamke awe msafi,asiwe mvivu, awe na heshima ajue kupika na ajue kuzungusha kiuno. Tofauti na hapo ww unachotafuta ni kitonga na kwaharaka haraka nikufahamishe hao viumbe hela zao zinabajet sana na ukiila utasimangwa hatare.

Bwana mdogo toka usingizini katafute hela uache upuuzi wa kuwaza kusaidiwa majukumu na mwanamke.
Mwanaume hutakiwi hata kuchukua ushauri kwa mwanamke,mwanamke ndo anatakiwa achukue ushauri kwako hapo utaiona heshima.

Huyo SINGO MAZA kakuzidi akili ndomaana anakuzuzua.Toka kimbia mbio katafute uliyemzidi akili, acha ujinga.
Kama ashapenda huwezi kumshauri akaelewa
 
Aisee duh.
Pole kwa kuwa njia panda. Ndoa ni kipindi Cha mwisho Cha maishabya mtu. Ufanye uamuzi wa busara sana. Aidha, kwa kukufahamisha tu kama shida yako ni watoto. Humu ndani kuna mabinti ambao wako tayari kuolewa na hawana watoto. Pia, kama shida yako ni kuwa na mahusiano ya nyuma humu ndani na hata nje ya hapa wapo mabinti ambao hawajatumika kabisa. Fata moyo wako unataka nini.
 
Naomba ushauri wako kati ya hawa wanawake wawili yupi anaweza kuwa sahihi kwangu?

MWANAMKE WA KWANZA
Ana elimu ya darasa la saba lakini ni mjanja sana maana hata text za kiingereza anajua kusoma na kuandika baadhi ya maneno, amezaliwa 1988 (miaka 36), ana watoto wawili wote wa kike - sio watoto wangu.

Mrefu, mweupe, ana akili ya maisha, anafanya kazi private sekta, na mjasiria mali (anajishughulisha na ufugaji kuku), amepanga anaishi na mtoto huyo mdogo (2 years) na dada wa kazi. Ni msafi, anajipenda, anajua maisha, anaweza ku-plan maisha yake (so far ana kiwanja, na bati kanunua) kifupi ni hayo. Niliwahi kuwa na mahusiano nae hapo awali, baadae nilipotezana nae, nilipokuja kukutana nae ndio akawa na huyo mtoto. Wazazi wake wote wamefariki.

MWANAMKE WA PILI
Ana elimu ya form 4 (division 3 point 25), ni wa mwaka 2000, ana mtoto wa miaka 4 (mtoto wa kike), anaishi na babu na bibi yake - (kwa upande wa mama yake) kwa sababu baba na mama yake walishafariki. Mrefu wastani, maji ya kunde, hana akili ya maisha zaidi ya kujua kupika na kufua na yale mengine ya chumbani (chumbani ni wa moto), ni tegemezi kwa asilimia 100% hata ukimueleza kuhusu kufanya biashara au kumtafutia shughuli ya kufanya anasema yeye kwasasa anataka tu ku-enjoy maisha na kikubwa azae alee familia.

Kwa jinsi alivyo hana matumizi mazuri ya fedha kwa kile apewacho, sijui kama ni akili ya utoto au laaa.

Huyu wa 1988 na huyu wa 2000 tofauti yao ni miaka 12, kwa maana mmoja ni 36 years, na mmoja ni 24 years.

Naomba toa ushauri wako kuhusu ot wa kati ya hawa wawili anaweza kuwa mama bora wa familia.

Akina dada na wamama wa hapa JF, na nyie wanaume kulingana na uzoefu wenu wa maisha , TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.
Wote ni single mother hawafai. Wewe una umri gani na unajishughulisha na nini?
 
Usioe Ila wasaidie wape mtaji ili waendelee na maisha yao
 
Kuna jamaa yangu alimpeleka ''single maza'' wake kwa wazazi. Baba yake akamwonya kwa kumwambia ''unayoaje mwanamke aliyezaa, huyo aliyemzalisha kwa nini hakumuoa?''. Jamaa akakaidi na kuoa. Walija achana kwani iligundulika baadae kuwa hakuwa ''single maza'' tu bali alikuwa ''double maza'' kwani alikuwa na mtoto mwingine akamficha na alikuwa jeuri kweli kweli ndiyo maana hakuweza kuishi na baba wa watoto aliozaa.
 
Mkuu kwamba nyota yako imewaka kwa wanawake walozalishwa pekee?

Usitake kuanza mechi huku agrigeti inakubana namna hiyo utaumia sana
 
Tupe na CV yako ili tukiwashe vizuri kwa Pande zote...
Yeah aweke wazi pia cv yake tusije tukamshauri kuishi na mshangazi wakati yeye binafsi pengine ni mtoto wa 2000 wa kunyoa viduku na kucheza amapiano hapo ushauri wetu hautafanya kazi vizuri
 
Back
Top Bottom