Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Mwanamke yupi sahihi kati ya hawa wawili? USHAURI WAKO NI MUHIMU

Mkuu maelezo niliyoweka hapo nadhani yapo very clear. Imagine ndio wewe sasa na yakupasa ufanye maamuzi kwa kuzingatia hiyo scenario, utafanyaje mkuu. ushauri wako ni muhimu sana
Inabidi tujue na wewe upoje ili tukushauri
 
Naomba ushauri wako kati ya hawa wanawake wawili yupi anaweza kuwa sahihi kwangu?

MWANAMKE WA KWANZA
Ana elimu ya darasa la saba lakini ni mjanja sana maana hata text za kiingereza anajua kusoma na kuandika baadhi ya maneno, amezaliwa 1988 (miaka 36), ana watoto wawili wote wa kike - sio watoto wangu.

Mrefu, mweupe, ana akili ya maisha, anafanya kazi private sekta, na mjasiria mali (anajishughulisha na ufugaji kuku), amepanga anaishi na mtoto huyo mdogo (2 years) na dada wa kazi. Ni msafi, anajipenda, anajua maisha, anaweza ku-plan maisha yake (so far ana kiwanja, na bati kanunua) kifupi ni hayo. Niliwahi kuwa na mahusiano nae hapo awali, baadae nilipotezana nae, nilipokuja kukutana nae ndio akawa na huyo mtoto. Wazazi wake wote wamefariki.

MWANAMKE WA PILI
Ana elimu ya form 4 (division 3 point 25), ni wa mwaka 2000, ana mtoto wa miaka 4 (mtoto wa kike), anaishi na babu na bibi yake - (kwa upande wa mama yake) kwa sababu baba na mama yake walishafariki. Mrefu wastani, maji ya kunde, hana akili ya maisha zaidi ya kujua kupika na kufua na yale mengine ya chumbani (chumbani ni wa moto), ni tegemezi kwa asilimia 100% hata ukimueleza kuhusu kufanya biashara au kumtafutia shughuli ya kufanya anasema yeye kwasasa anataka tu ku-enjoy maisha na kikubwa azae alee familia.

Kwa jinsi alivyo hana matumizi mazuri ya fedha kwa kile apewacho, sijui kama ni akili ya utoto au laaa.

Huyu wa 1988 na huyu wa 2000 tofauti yao ni miaka 12, kwa maana mmoja ni 36 years, na mmoja ni 24 years.

Naomba toa ushauri wako kuhusu mwelekeo wa nani kati ya hawa wawili anaweza kuwa mama bora wa familia.

Akina dada na wamama wa hapa JF, na nyie wanaume kulingana na uzoefu wenu wa maisha , TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.
1. Tofauti ya umri kati ya kila mmoja na wewe ni miaka mingapi?

2. Kwa mtazamo wangu, wa kwanza ni kama umemfagilia sana kiasi cha mimi kuona huyo ndo anakufaa. Lakini, ana watoto wawili. Swali, hao watoto amezaa na mwanaume mmoja wote wawili au kila mmoja ana baba yake?

3. Kuhusu huyu wa pili ambaye ameamua yeye ni wa kuzaa tu na kufurahia maisha, tena kwa 100% ya utegemezi toka kwako, naamini mtasumbuana sana huko mbeleni.

Concl.
HAKUNA ANAYEKUFAA HAPO, SABABU ZANGU NI HIZI;

1.
Mwenye watoto utakuja kusumbuana na wazazi/mzazi wa watoto wake. At least mtoto angekuwa mmoja, angalau. Wawili ni risk. Na nakuambia, yeye hatakuwa tayari kuwatenga watoto wake kisa wewe.

2. Mwenye kutaka kufurahia maisha, siku ukiishiwa utajuta kumfahamu. Hasa ukizingatia yeye hataki kujihusisha na namna yoyote ya utafutaji hela.

3. Mwenye watoto, anajiweza kiuchumi kwa 100%, hiyo itakutia inferiority complex in a way. Hakunaga mwanaume mwenye ujasili wa kupambana na mke mwenye pesa, elimu, madaraka au vyote vitatu huku mwanaume huna hata kimoja katika hivyo. Kifupi ukipitwa na mwanamke, utakuwa ni mtu wa kutafakari kila neno linalomtoka mdomoni mwake. Na kila neno utalihusisha na uwezo wake au wako kifedha.
 
Naomba ushauri wako kati ya hawa wanawake wawili yupi anaweza kuwa sahihi kwangu?

MWANAMKE WA KWANZA
Ana elimu ya darasa la saba lakini ni mjanja sana maana hata text za kiingereza anajua kusoma na kuandika baadhi ya maneno, amezaliwa 1988 (miaka 36), ana watoto wawili wote wa kike - sio watoto wangu.

Mrefu, mweupe, ana akili ya maisha, anafanya kazi private sekta, na mjasiria mali (anajishughulisha na ufugaji kuku), amepanga anaishi na mtoto huyo mdogo (2 years) na dada wa kazi. Ni msafi, anajipenda, anajua maisha, anaweza ku-plan maisha yake (so far ana kiwanja, na bati kanunua) kifupi ni hayo. Niliwahi kuwa na mahusiano nae hapo awali, baadae nilipotezana nae, nilipokuja kukutana nae ndio akawa na huyo mtoto. Wazazi wake wote wamefariki.

MWANAMKE WA PILI
Ana elimu ya form 4 (division 3 point 25), ni wa mwaka 2000, ana mtoto wa miaka 4 (mtoto wa kike), anaishi na babu na bibi yake - (kwa upande wa mama yake) kwa sababu baba na mama yake walishafariki. Mrefu wastani, maji ya kunde, hana akili ya maisha zaidi ya kujua kupika na kufua na yale mengine ya chumbani (chumbani ni wa moto), ni tegemezi kwa asilimia 100% hata ukimueleza kuhusu kufanya biashara au kumtafutia shughuli ya kufanya anasema yeye kwasasa anataka tu ku-enjoy maisha na kikubwa azae alee familia.

Kwa jinsi alivyo hana matumizi mazuri ya fedha kwa kile apewacho, sijui kama ni akili ya utoto au laaa.

Huyu wa 1988 na huyu wa 2000 tofauti yao ni miaka 12, kwa maana mmoja ni 36 years, na mmoja ni 24 years.

Naomba toa ushauri wako kuhusu mwelekeo wa nani kati ya hawa wawili anaweza kuwa mama bora wa familia.

Akina dada na wamama wa hapa JF, na nyie wanaume kulingana na uzoefu wenu wa maisha , TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.

Kuna tusi nilitaka kukutukana lakini nimejizuia
 
1. Tofauti ya umri kati ya kila mmoja na wewe ni miaka mingapi?

2. Kwa mtazamo wangu, wa kwanza ni kama umemfagilia sana kiasi mimi kuona huyo ndo anakufaa. Lakini, ana watotot wawili, swali, amezaa na mwanaume mmoja watoto wote wawili au kila mmoja ana baba yake?

3. Kuhusu huyu wa pili ambaye ameamua yeye ni wa kuzaa tu na kufurahia maisha tena kwa 100% ya utegemezi toka kwako, naamini mtasumbuana sana.

Concl.
HAKUNA ANAYEKUFAA HAPO, SABABU ZANGU NI HIZI;

1.
Mwenye watoto utakuja kusumbuana na wazazi/mzazi wa watoto wake. At least mtoto angekuwa mmoja, angalau. Wawili ni risk. Na nikuambia hatakuwa tayari kuwatenga watoto wake kisa wewe.

2. Mwenye kutaka kufurahia maisha, siku ukiishiwa utajuta kumfahamu. Hasa ukizingatia yeye hataki kujihusisha na namna yoyote ya utafutaji hela.

3. Mwenye watoto, anajiweza kiuchumi kwa 100%, hiyo itakutia inferiority complex in a way. Hakunaga mwanaume mwenye ujasili wa kupambana na mke mwenye pesa, elimu, madaraka au vyote vitatu huku mwanaume huna hata kimoja. Kifupi ukipitwa na mwanamke, utakuwa ni mtu wa kutafakali kila neno linalomtoka mdomoni. Na kila neno utalihusisha na uwezo wako kifedha.
Asante sana bro kwa mchango wako na muda wako. Umenifanyia analysis ambayo inatakiwa nitulie nayo kichwani
 
Wanawake wote ni sawa awe na PhD awe ni darasa la 7B. Ww cha kushukuru tu mwanamke awe msafi,asiwe mvivu, awe na heshima ajue kupika na ajue kuzungusha kiuno. Tofauti na hapo ww unachotafuta ni kitonga na kwaharaka haraka nikufahamishe hao viumbe hela zao zinabajet sana na ukiila utasimangwa hatare.

Bwana mdogo toka usingizini katafute hela uache upuuzi wa kuwaza kusaidiwa majukumu na mwanamke.
Mwanaume hutakiwi hata kuchukua ushauri kwa mwanamke,mwanamke ndo anatakiwa achukue ushauri kwako hapo utaiona heshima.

Huyo SINGO MAZA kakuzidi akili ndomaana anakuzuzua.Toka kimbia mbio katafute uliyemzidi akili, acha ujinga.
 
Back
Top Bottom