TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

Huyu jamaa sijui ni kwamba alikua na bahati mbaya au vp, Coz kuna Nyumba yake alijenga kule Mbweni ikaja kuvunjwa sikujua sababu hasa ni nini, Lakini pia jamaa alikua mpambanaji sana, Alikua na goli lake pale K.koo mtaa wa kongo, alikua anauza viatu vya wadada, na ukimkuta pale usanii na ustar anauweka pembeni anapiga kazi kweli kweli

Anyway Amepumzike kwa Amani kifo chake kinasikitisha sana, Inanikumbusha kifo cha Steve 2K aliyekufa kwa kuchomwa kisu na Producer Casto ponela, na Kifo cha john walker aliyekufa akiwa Gereji
 
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mandojo amefariki Dunia jijini Dodoma leo.

Taarifa ya kifo cha Msanii huyo imethibitishwa na rafiki yake wa karibu Msafiri L pamoja na msanii mkongwe Soggy Doggy

Kwa mujibu wa Msafiri L anasema marehemu Mandojo amefariki baada ya kupigwa na watu akidhaniwa kuwa ni mwizi usiku wa kuamkia Leo.

Tunaendelea kufuatilia Taarifa hii kwa undani Endelea kufuatilia kurasa zetu.

#MYDSwahili
 

Attachments

  • FB_IMG_1723375484259.jpg
    FB_IMG_1723375484259.jpg
    49.1 KB · Views: 1
#TANZIA Msanii wa Bongofleva Mandojo amefariki dunia leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Msanii mwenzake aliyefanya naye kazi kwa ukaribu Domokaya na Soggdoggyanter wamethibitisha taarifa hiyo ya kifo cha Mandojo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu mmoja ambaye alimuitia mwizi.

#RIPMandojo
 

Attachments

  • FB_IMG_17233756880051572.jpg
    FB_IMG_17233756880051572.jpg
    309.5 KB · Views: 2
Kifo hichi jamani,last time nawaona hawa ni kwenye duka lao la viatu kariakoo,Mbona ni mtu poa kaka why mob justice inakatisha maisha ya watu hivi pasipo sababu😪
Pole sana kwa Domokaya na familia yake kiujumla..Pumzika salama Mandojo😪😪
 
Kifo hichi jamani,last time nawaona hawa ni kwenye duka lao la viatu kariakoo,Mbona ni mtu poa kaka why mob justice inakatisha maisha ya watu hivi pasipo sababu😪
Pole sana kwa Domokaya na familia yake kiujumla..Pumzika salama Mandojo😪😪
Huyu Mwamba ndio ana soko Mbande-Kisewe, mradi ambao alisema utamuingizia zaidi ya Laki 1 na 20 kila siku.
 
Back
Top Bottom