TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

Ifike hatua wananchi wawe wanatumia busara kumdhibiti kwanza mtu halfu wajiridhishe kama kweli ni mwizi kuliko kuanza kumshushia kipigo tu.

Tulishawahi kumuokoa mwana na hii hatari kupigwa na wananchi baada ya kugombana na demu na uyo demu kupiga kelele za mwizi wakati ni ugomvi wa kawaida tu kati yao.

Nina mshkaji wangu alishawahi kufa baada ya kupigiwa kelele za mwizi, alirudi kwake usiku amelewa sasa nyumba za kota zimefanana kinoma kufungua mlango haufunguki akapiga teke kumbe sio kwake dada wa kazi akapiga kelele za mwizi watu wakafika bila kuuliza wakapiga wakaua.

Wananchi waelimishwe kutumia busara wanaposikia makelele ya mwizi
Juzi niliona clip ya mwizi anachomwa moto wakati walishampiga na hawezi hata kukimbia. Nikakemea sana sana kile kitendo lakini kuna watu wengi wengi sana walikuwa wanafurahia na kuhoji, ''umeshawahi kuibiwa wewe?''. Ni masikitiko sana kuona dunia ya yale mtu anaweza kuuawa katika mazingira kama haya. Kna watu wengi tu wameshawahi kuuawa kwa kudhaniwa ni wezi kumbe siyo.
 
#TANZIA Msanii wa Bongofleva Mandojo amefariki dunia leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Msanii mwenzake aliyefanya naye kazi kwa ukaribu Domokaya na Soggdoggyanter wamethibitisha taarifa hiyo ya kifo cha Mandojo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu mmoja ambaye alimuitia mwizi.

#RIPMandojo

Kwani waliokuwa wanahalalisha panya road kuuwawa kwa kuhisiwa tu, hadi hapa wanasema je?
 
Inavosemekana jamaa kumbe alikuwa na afya ya akili na waliompiga
Kwanza jeshi la polisi, libebe lawama, inakuwaje mtu kapigwa, hali mbaya na anavuja damu nyie mnakaa nae tu ndani? Hili ni kosa, ni uzembe.

Ndugu walijua ndugu anapiga maji anakuwa miyeyusho walichukua hatua yoyote msela aache pombe.

Mchizi alikuwa na bahati mbaya, miaka kadhaa nyuma niliona kabomolewa nyumba yake na mtu aliekuwa anagombea nae eneo, kitu kama hicho.
 
View attachment 3066818

Mungu ailaze mahali pema peponi nafsi yake Bwana alitoa Bwana ametwaa.

===

Msanii wa Bongo fleva Mandojo amefariki dunia asubuhi ya leo August 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa habari za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu ambae ndio aliemuitia mwizi.

"Nimeongea na Domokaya analia tu hawezi hata kuongea vizuri, anasema tu Mandojo, Mandojo Soggy Doggy Anter ambae nimeongea nae na kuthibitisha kutokea kwa msiba huu. Innalillahi wa inna ilayhi rajiun

Tunaendelea kufatilia taarifa zaidi

DJ FETTY
Ushimen again brother,

Ushimen sorry brother, classmate wanapukutika tu.
 
Back
Top Bottom