TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

TANZIA Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia

Kwanza jeshi la polisi, libebe lawama, inakuwaje mtu kapigwa, hali mbaya na anavuja damu nyie mnakaa nae tu ndani? Hili ni kosa, ni uzembe.

Ndugu walijua ndugu anapiga maji anakuwa miyeyusho walichukua hatua yoyote msela aache pombe.

Mchizi alikuwa na bahati mbaya, miaka kadhaa nyuma niliona kabomolewa nyumba yake na mtu aliekuwa anagombea nae eneo, kitu kama hicho.
Uzembe wa polisi kivipi kwani Polisi walimchukua akiwa anavuja damu wakaenda kumuweka lockup akafia kituo cha polisi?
 
Juzi niliona clip ya mwizi anachomwa moto wakati walishampiga na hawezi hata kukimbia. Nikakemea sana sana kile kitendo lakini kuna watu wengi wengi sana walikuwa wanafurahia na kuhoji, ''umeshawahi kuibiwa wewe?''. Ni masikitiko sana kuona dunia ya yale mtu anaweza kuuawa katika mazingira kama haya. Kna watu wengi tu wameshawahi kuuawa kwa kudhaniwa ni wezi kumbe siyo.
Hata kama una machungu ya kuibiwa ni kotu gani hicho ulichoibiwa mpaka uone sawa mwenzako kuchomwa mtoto.! Vyombo husika vianze kuchukulia siriaz kuwashughulikia wanaofanya haya matukio,
 
Uzembe wa polisi kivipi kwani Polisi walimchukua akiwa anavuja damu wakaenda kumuweka lockup akafia kituo cha polisi?
Umesikia hiyo clip? UMESIKILIZA, jamaa wamemkuta kesho yake kitu cha polisi hali mbaya saana, mguu wake wa kulia ukivuja damu, na hapo kituo cha polisi alipelekwa toka jana usiku.. Sasa hapo kwanini wasilaumiwe wanakaaje na mtu anavuja damu na hali yake ni mbaya?
 
.
 
Attachments

  • Screenshot_20240811_152042_Chrome.jpg
    Screenshot_20240811_152042_Chrome.jpg
    264.3 KB · Views: 2
Umesikia hiyo clip? UMESIKILIZA, jamaa wamemkuta kesho yake kitu cha polisi hali mbaya saana, mguu wake wa kulia ukivuja damu, na hapo kituo cha polisi alipelekwa toka jana usiku.. Sasa hapo kwanini wasilaumiwe wanakaaje na mtu anavuja damu na hali yake ni mbaya?
Tatizo kila mtu anatoa taarifa zake , mandojo amepigwa asubuhi ya leo, jana hajalala kwake leo asubuhi kuna kanisa aliingia akafanya fujo, Mandojo huwa hanywi pombe akinywa huwa anakua kama amedata sasa inasemekana alikunywa pombe ikamletea shida ndo akaanza kuzingua ndo sababu iliyopelekea akapigiwa kelele za mwizi, kapigwa leo asubuhi polisi alipitishwa kuchukua pf3 tu
 
Back
Top Bottom