Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Mkuu shida Nini kwenye hiyo kauli? Unaniniita zuzu kisa kusema tutafuteni Hela Mzee. Well ubarikiwe.
Wewe una shida mbili: kwanza umeshindwa kujua kwamba kila siku serikali inasema, tena bungeni ni marufuku mwili wa marehemu kuzuiwa kwa kisingizio cha deni, lakini wewe hiki kinachofanyika umeona ni sawa tuuu. Pili unapomwambia atafute pesa ni wewe uliyemsaidia kutafuta pesa ya kumuuguza mgonjwa wake hospittalini mpaka akafariki? Je unajua mpaka mgonjwa anafariki ametumia sh ngapi hospitalini kabla ya wewe kuja na kejeli zako za kijinga??

Mwisho ukiona mtanzania anamwambia mwenzake tafuta pesa jua ni zuzu kwa sababu hujui maisha ya huyo unayemwambia tafuta pesa zaidi ya kumuona akiposti mtandaoni. Siyo kila mtu anayepata pesa huwa anapita nazo mtaani kuwaonyesha kama anazo.
 
Nimesema tutafuteni Hela, Sasa mjomba kuwa serious ni wapi Sheria imetamka maiti isizuiwe?. Chief kuwa serious achana na maneno ya wanasiasa tupambane kujiimarisha kiuchumi tuepukane na adha hizi. Jioni njema.
 
Nimesema tutafuteni Hela, Sasa mjomba kuwa serious ni wapi Sheria imetamka maiti isizuiwe?. Chief kuwa serious achana na maneno ya wanasiasa tupambane kujiimarisha kiuchumi tuepukane na adha hizi. Jioni njema.
Na mimi nimekujibu kwamba watu wote hapa Tanzania wanaofanya maisha yao ni wewe uliwaambia watafute pesa?? Achana ha hizi kauli za reja reja za mtaani ndugu yangu kwani mwenye pesa hawezi kuja inbox kukuambia tayari nimejipata.

Wewew kuniambia mimi niachane na wanasiasa ndiye unapaswa uwe seriuos, hivi unajuaje kama mimi siyo mwanasiasa? Unanifahamu kwani?
 
Shida ni kwamba waweza kuta utaratibu upo ila hauwekwi wazi kwakua wanaojua utaratibu upo wanalenga kuipiga pesa ikitolewa nzima.

Pili, ni sahihi zaidi wakimpa mgonjwa options za huduma ili ajue nini kinafuata kwa mgonjwa ama akipona ama akifariki. Nimeona kuna mtu kaandika kitanda 50K per day. Why? Ilikua ni private ward au vipi? Kama ni ndiyo kwanini mzazi asingeambiwa?
 
Umesoma thread hadi mwisho? Umeelewa?

Tunajadili sera ya afya na huduma za afya ya serikali ya CCM kwa kutumia scenario ya ndugu huyu na maiti yake kuzuiliwa.

Umeipata point yangu? Umeelewa sasa?

Haya twende kazi. Leta hoja yako wajumbe wakusome
Point yako ni ipi? Kwamba kwakuwa alifariki usilipe?
 
Tukate bima za afya kuliko kuanza ilaumu Serikali
 
Kwa hichi ulichokiandika, hakuna sababu ya kuendelea kujadiliana na wewe. Tayari una perception yako iliyojaa judgement ndani yake. Ila in humanity, hospitali walijali utu kabla ya pesa. Kama bill ya matibabu imewashinda, fuateni utaratibu wa kulimaliza swala hilo kwa kufata taratibu husika.
 
Hiyo 10m ni pesa ya kununua goli Moja cc Sa100.
 
Zuzu mwingine huyu hapa...
Jambo jema ungetueleza ni vipi aliyefariki hadaiwi anadaiwa asiyefariki kwa huduma ambayo hospitali haikumpa! Je, ambao hawana ndugu nani anadaiwa? Na unadaiwa nini wakati mgonjwa alilipia gharama za tiba! Kosa ni kufia hospitalini! Hiyo kwa kifupi ni kodi ya kifo.
 
Mimi ningewaachia hiyo maiti wanisaidie kuzika, na hata mimi nikifa wakakaza niacheni tu haiwezekani Engineer aangushe ghorofa kisha adai malipo tena makubwa kiasi iko.
Kifo ni kifo na Maziko ni maziko tu, Ukoo urelax.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…