Mwananchi amwaga Machozi akimtaka Rais Samia kufuta Mkataba wa DP World

Mwananchi amwaga Machozi akimtaka Rais Samia kufuta Mkataba wa DP World

Nimeona msigwa anaambiwa huo mjadara angepeleka redioni ambako wasikilizaji ni wengi ila kakaza fuvu.
Msigwa ni mjinga,analeta mjadala halafu anachagulia watu maswali ya kuuliza.
 
Wanasambaza meseji kweny magroup ya kanisa wakipewa hofu eti wakristo watakosa ajira ,mara sijui nchi itageuka kuwa ya kiislamu ,mara watabaguliwa .

Zipo wapi hoja za kiuchumi zenye mantiki ?

Tibaijuka huyu aliyekula pesa za Escrow na kusema hadharani na wale maaskofu waliohongwa ila kumsafisha na walikuwa na kesi huko mahakamani?

Je watu fulani wakiibua mjadala wa uendeshaji wa hospital ya KCMC na Bungando kwa kupewa ruzuku na serikali naw waliosaini na kutoa wazo hilo wote wa dini ,si watu wa dini fulani wataanza kuitwa magaidi?

Kwa nn hamna hoja za kiuchumi zaidi ya watu kuleta hofu tu mara waliosaini ni wazanzibar mara waislamu hii ni hoja kweli kama sio wapumbavu ndo wanakuwa na ujinga huo.
apo sasa umetusanua labda upande wa pili mnatumiana msg kuunga huu mkataba mbovu alafu hizo hospitali zinatoa huduma kwa jamii nzima sio dini fulani yani hazina tofauti na hospitali za serikali .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdada wa watu ameamua kutoa machozi baada ya kuona anaenda kugeuzwa mtumwa ndani ya mipaka ya nchi yake, moyo wake umeshindwa kuvumilia maumivu ya kuona watoto, wajukuu, vitukuu vyake vitakaposhindwa kufaidi rasilimali watanganyika tulizopewa na Mungu.

Samia aendelee kunyamaza, aendelee kuacha vifua vya wengi viendelee kujaa kwa maumivu, na hasira, atambue wapo wengi wasiotoa machozi ili kutuliza maumivu ndani ya mioyo yao kama alivyofanya Edna, hawa hasira zao wataenda kuzitolea sehemu nyingine kwa njia nyingine.

Sasa muache akae asubiri mjinga aliyeamua kuziba masikio akijitapa kufanya kazi asizojua anamfanyia nani.
Acha upotoshaji
 
Mjadala unaendelea, maswali na majibu now... huyo dada alisema neno moja tu kwa sauti ya kilio "Msigwa, mwambie dada Rais Samia afute huo mkataba, sisi hatuutaki"
Sasa apo aliongea nini ni drama tu

Angetoa sababu kweli alipoteza muda
 
Rais Samia ameanza kufoka ati "stupid"?

Huu ni mwanzo tu wa ripoti za CAG kuumbua zaidi utawala wako , ufisadi uliuasisi mwenyewe mwanzoni kabisa ya utawala wako.

Wakati anaingia madarakani, kwa kutumia hekima zake na uungwana wake, alianza kuyafungulia majizi na mafisadi yaliyofungwa jela.

Tukaona wazalendo wote wanafukuzwa kazi na kurudishwa majizi kama akina Nape, Kinana, Makamba! Majizi yakaanza kurudishiwa hela zao, symbion wakalipwa billion 360 chapchap bila kufuata utaratibu wa bunge.

Akatuambia kuwafunga majizi jela ni udikteta, na kwamba majizi wanatakiwa kuachiwa huru na kupewa kongole. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.

Na baada ya hapo, tukaambiwa kwamba majizi wanatakiwa kulipwa fidia na ruzuku. Hatupaswi kuwasumbua kwa namna yoyote ili kulinda misingi ya utawala wa sheri.

Akina Makamba wakawa wanaleta makampuni kutoka nje Kwa mikataba ya hovyo Kwa mabilioni ya pesa..
 
Hiyo ni lazima, uwezi kuzaa watoto kakosa wajukuu. Mateso ni mjukuu
 
Back
Top Bottom