Rais Samia ameanza kufoka ati "stupid"?
Huu ni mwanzo tu wa ripoti za CAG kuumbua zaidi utawala wako , ufisadi uliuasisi mwenyewe mwanzoni kabisa ya utawala wako.
Wakati anaingia madarakani, kwa kutumia hekima zake na uungwana wake, alianza kuyafungulia majizi na mafisadi yaliyofungwa jela.
Tukaona wazalendo wote wanafukuzwa kazi na kurudishwa majizi kama akina Nape, Kinana, Makamba! Majizi yakaanza kurudishiwa hela zao, symbion wakalipwa billion 360 chapchap bila kufuata utaratibu wa bunge.
Akatuambia kuwafunga majizi jela ni udikteta, na kwamba majizi wanatakiwa kuachiwa huru na kupewa kongole. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.
Na baada ya hapo, tukaambiwa kwamba majizi wanatakiwa kulipwa fidia na ruzuku. Hatupaswi kuwasumbua kwa namna yoyote ili kulinda misingi ya utawala wa sheri.
Akina Makamba wakawa wanaleta makampuni kutoka nje Kwa mikataba ya hovyo Kwa mabilioni ya pesa..