Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Hapa wanachotakiwa kufanya mwananchi ni kuondoa jina la JPM kwenye poll kama wakirudia hii poll lakini pia hili linaweza lisisaidie na wasithubutu kurudia hii kitu maana itakuwa mbaya zaidi cha msingi ni kuandaa ya Mama peke yake nayo inaweza isidaidie aiseeee….
 
Tafuteni slogan ya kuvutia kama "ukweli na uwazi", "maisha bora kwa kila Mtanzania"
Kazi zinaonekana na zinajieleza hakuna haja ya mazingaombwe na propaganda.

You know Samia is a leader of issues not mazingaombwe ya punda ,sijui kujifanya mchana Mungu sana and the likes
 
Gazeti la mwananchi lilianzisha kura za mtandaoni ama poll ya kuuliza wadau ni sera za kiongozi yupi wa Tanzania kati ya Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia wanazozikubali.

Matokeo ya kura yakaonesha Kikwete kupata 17% sawa na Samia, Mkapa kupata 7% na Magufuli kupata 57%.

Baada ya matokeo hayo kutoka, Mwananchi wameamua kuomba radhi kwamba uchaguzi ama vigezo vilivyotumika havikuwa sahihi wanaomba radhi😂.

View attachment 2973698View attachment 2973699
Wameshakoromewa hawa.
Ila yote ya yote ukweli usemwe MAGUFULI NI RAIS PEKEE KUWAHI KUTOKEA TANZANIA.
Shida ilikua utumiaji mabavu tu na kutokupenda kushaurika.
Ila Samia ni KIONGOZI WA HOVYO KUWAHI KUTOKEA.
 
Kazi zinaonekana na zinajieleza hakuna haja ya mazingaombwe na propaganda.

You know Samia is a leader of issues not mazingaombwe ya punda ,sijui kujifanya mchana Mungu sana and the likes
Kazi gani wewe!?
Sema muendelezo wa kazi zilizokwishaanza awamu za nyuma.
Hakuna jipya na la maana Samia anafanya,zaidi amekwamisha mambo mengine.
 
Ukweli upi Sasa? 🤣🤣 Mbona mnalazimisha mliyoshindwa? 😁😁😁😁

Nimekueleza Samia kawapelekea umeme,kawanunulia mtambo wa Utafiti,kawajengea soko la Madini na kawapelekea Huduma za ugani wa Madini za GST kule Chunya.

On top of that kawapa eneo na amewarihusu wachimbe Hadi kwenye vitalu ambavyo Watu wa mazingira walizuia.

Samia anajua kutafuta hela ndio maana anafaulu usilinganishe na wajamaa unaowatetea ni waharibifu na watumiaji wa vya wengine
Chawa wa mama umebaki pekeako unapambana hatari
 
Gazeti la mwananchi lilianzisha kura za mtandaoni ama poll ya kuuliza wadau ni sera za kiongozi yupi wa Tanzania kati ya Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia wanazozikubali.

Matokeo ya kura yakaonesha Kikwete kupata 17% sawa na Samia, Mkapa kupata 7% na Magufuli kupata 57%.

Baada ya matokeo hayo kutoka, Mwananchi wameamua kuomba radhi kwamba uchaguzi ama vigezo vilivyotumika havikuwa sahihi wanaomba
Jamaa wa mtama hapo maelekezo yake yamehusika
 
Kwani wajinga kuwa wengi kunazuia polling? Wewe hapo niambie Magufuli amemzidi Samia lipi hasa na Mimi nikueleze Samia aliyomzidi Magufuli,hata ukitaka leta sekta Moja baada ya nyingine tulinganishe.

Narudia kukuuliza tena,wewe unadhani aliyekuza Mapato kutoka 1.5T Hadi 2.2T Kwa miaka 3 nani amefanya kazi kubwa?
Utajua mwenyewe, mie nnachojua JPM hakuwa babu kubwa sana hasa kwenye utawala bora, ila huyu mamako ni hamna kitu...kuna kakikundi fulani tu kadogo kenye maslahi ndio kanatumia nguvu kubwa kumpamba mf Nape ili waendelea kula kwa urefu wa kamba zao!
 
Hapa wanachotakiwa kufanya mwananchi ni kuondoa jina la JPM kwenye poll kama wakirudia hii poll lakini pia hili linaweza lisisaidie na wasithubutu kurudia hii kitu maana itakuwa mbaya zaidi cha msingi ni kuandaa ya Mama peke yake nayo inaweza isidaidie aiseeee….

Wakiandaa nyingine lazima watu wao wa IT wawe stand by kufanya uchakachuaji .
Kwa sisi watu wa tafiti hiyo ya kwanza ndio ukweli mwenyewe itakayofata itakuwa ya kutengeneza watu wa research tunafahamu
 
Unaniambia mimi mkuu 'Mbaga, Jr'. Ni kipi hasa ulichoona nimeandika kilichokufanya univunjie heshima ya kunihusisha na mambo nisiyo husika nayo?
Au wewe ni mmoja wa vihio wengi tulionao humu, wanaojuwa kusoma lakini hawaelewi wanachokisoma!

Umenishangaza sana kuandika hayo uliyoandika kunijibu mimi na kunihusisha bila hata kuona ushahidi wowote kuwa nami ni hao unaowasema wewe.
Nadhani una matatizo ya uelewa wa ulichosoma. Umebwatuka tu, kujibu kama mtu aliyekuwa usingizini akiota jambo lisilokuwepo.

Usinihusishe na ujinga huo tena.
Kwahy gazeti la mwananchi limekuwa la hovyo baada ya kuweka hy poll ila kabla ya hapo lilikuwa lizuri.?
 
Kazi zinaonekana na zinajieleza hakuna haja ya mazingaombwe na propaganda.

You know Samia is a leader of issues not mazingaombwe ya punda ,sijui kujifanya mchana Mungu sana and the likes
Kazi zingeonekana marehemu asingeshinda hapo inaonekana bibi kizee hamna alilofanya miaka 3 yote katoka Kapa na mwakani anaenda kutoka pale kwenye hicho cheo chake machawaa tumewashtukia 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jambo lingine nililoona kwa hapa JF ni upande wa comments, zinazomsifia JPM zina reactions nzuri zenye kupendeza ila Comments zenye kumpinga JPM utakuta zina dislike na like kidogo 😂 hii inaonyesha n kwa namna gn JPM anavokubalika.

Hata hapa JF, kuna uzi wa poll wa rais yupi unamkubali na JPM ndie aliyepata kura nyingi.
 
Back
Top Bottom