Makusanyo ya JPM yalikua na faida gani? Maana miradi yote ilijengwa kwa mikopo, hakutoa ajira, hakupandisha mishahara, sasa hizo pesa alizobania matumizi alizitumia wapi? Mbona Mama anaspend kuliko JPM na bado anaajiri, kuongeza mishahara, miradi analipa madeni n.k!! Amewezaje?
Kuhusu ufisadi tokea enzi za JPM CCM walikua wanaiba na hakuna hatua zilichukuliwa. Mfano ACACIA walitupa loss ya Trillion 400+ ila bado walipewa hisa 84%, waliruhusiwa kusafirisha makinikia na kesi zote tulizowafungulia tulifuta.
Mwanyika yule VP wa ACACIA alikua na kesi ya uhujumu uchumi ya zaidi ya 2B ila sio tu aliachiwa ila alipewa ubunge na JPM!! same to Nchambi alikamatwa na nyara za serikali na bunduki za ujangili ila aliachiwa na aliendelea na ubunge.
Bashiru naye alikagua mali za CCM akagundua ufisadi wa kutisha ila JPM na ubabe wote ule hakuwahi mchukulia hatua hata mmoja!! Zaidi alibembeleza walioba warudishe kwa hiari.
Ripoti ya CAG tokea 2015/16 zimekua zikitaja mafisadi kila mwaka cha ajabu CAG alipotaka kukagua manunuzi ya ndege na SGR akaondolewa kazini!! Sasa kama JPM alikua na nia ya kuzuia wizi why azuie CAG asikague TGFA?
Haya kuelekea uchaguzi wa 2020, JPM alituma TAKUKURU kuchunguza watoa rushwa kura za maoni. Cha ajabu ile ripoti sio tu ilifanywa siri ila waliotoa rushwa hawakupelekwa mahakamani zaidi ya kukatwa tu kinyume na sheria iliyoanzisha TAKUKURU. Yaani mtu anatoa rushwa adhabu yake ni kunyima tiketi ya kugombea na sio jela tena?
So kama issue ni kuchukua hatua JPM alikua anatumia makamera tu kufoka ila kiuhalisia majizi kibao aliyachekea. Hata wale waliokamatwa kwa kesi za uhujumu uchumi kuanzia Seth, Ruge sijui hakuna aliyekutwa na hatia mpaka leo. So huwa nashangaa wafuasi wake mnavyompamba kuwa alikua na maamuzi magumu sijui anachukua hatua.