Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Kama una imani mpeleke kanisani!! Kwa MWAMPOSA, au kanisa jingine unakopaamini.
 
Pole sana nenda kwa daktari wa misuli
 
Mkuu usihangaike namwanao popote ispokua hospital. Mambo yamatibabu yanachangamoto nyingi Sana hasa kiuchunguzi navipimo lakin usichoke kuhangaika naukajitikomeza kwnye njia zisizo kitaalam,

Nimuhimu kubalance mambo ya imani najitihada zako kama mzazi. Weka Imani yote mungu atamponya ilajitihada 100% weka kwenye tiba zakisayansi. Wengi wanapotea kwenye hilo nakuwaumiza Zaid wapendwa wao

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Usifanye makosa ya kuchelewa. Mpeleke hospitali kubwa kama Muhimbili etc. Mimi naamini hiyo itakuwa ni hitilafu kwenye moja ya pingili za Uti wa Mgongo, hali inayopelekea kubanwa kwa mishipa ya fahamu inayosambaa kwenda maeneo ya chini ya mwili.

Hakuna muujiza zaidi ya kuwahi haraka sana Muhimbili.

Pia, Nitaangalia kama ninayo Namba ya daktari yeyote pale MOI akupe ushauri zaidi wa kitaalamu.
 

Pole mzazi kwa kuuguliwa.

Zingatia sana hapa na yaliyotolewa hapo juu.

1: Inawezekana uumiaji wa mtoto haukuwa mkubwa kuleta athari ya ghafla, ila matokeo ya kuumia ndo yameleta shida (kututumka kwa mwili/inflammation) au kadri ya tiba za kuchua zimeongeza tatizo pia.

2: Hii inahusisha athari kwenye mfumo wa uti wa mgongo ndo maana athari zinaonekana pande zote mbili za miguu (mfumo wa umeme na taarifa kutofika miguuni vizuri).

3: Baada ya Xray, CT scan ya uti wa mgongo kutegemea na level ya panapoanzia maumivu au ganzi ni muhimu.

4: Mpeleke mgonjwa kwenye hospitali ya juu zaidi yenye madaktari wa mifupa na mishipa ya fahamu pia yenye uwezo wa kufanya vipimo tajwa kulingana na ulipo.

5: Kama unatumia bima, hakikisha unapata referral note kukuondolea usumbufu.

6: Naomba msimkande au kumchua maeneo ya mgongo kwa sasa/tena. Bali aendelee na dawa za kumeza/sindano au hiyo ya kupaka ni APAKWE TU BILA KUCHUA AU KUMKANDA.

7: Msimbebe kwa kukunja uti wa mgongo bali awekwe kwenye kitu kigumu ambacho mgongo haujikunji.
 
Umemaliza kila kitu ..
Hiyo case 2 toka kwa mdau bagamoyo na maelezo yako yana mwanga wa moja kwa moja.

USISAHAU MAOMBI..
PINDI UTAKAPOPATA SULUHU.. USISITE KUTUPA MREJESHO.
 
Ukiambiwa hosipitalini kuwa nenda kajaribu kwenye maombi unabidi ujiongeze hawawezi kukuambia jaribu na dawa za wanganga wa kienyeji.Wanakuambia mpeleke kwenye maombi.​
 
Kuhusu haja kubwa mwisho amejisaidia jumapili nakula anakula vzr tu nimemuuliza inamaana husikii haja kabisa au unajibana anasema toka j3 hajahisi haja kubwa kabisa,haja ndogo anapata vzr na anacontrol(hajikojolei) huwa anasema nasikia mkojo ndo tunamuweka sehemu yakukojoa anakojoa kisha tunamtoa.
Vipimo zaidi nitampeleka hosptal yarufaa juma3 kuhusu uti wa mgongo apo sijui zaidi ila anakaa nakujisomea vitabu vyake ama kuangalia Tv vizuri tu bila kujiegemeza sehemu yoyote
 
Usifanye makosa ya kuchelewa. Mpeleke hospitali kubwa kama Muhimbili etc. Mimi naamini hiyo itakuwa ni hitilafu kwenye moja ya pingili za Uti wa Mgongo, hali inayopelekea kubanwa kwa mishipa ya fahamu inayosambaa kwenda maeneo ya chini ya mwili.
Kwa comment yako hii imenifanya nimuambie achezeshe vidole vya miguu lkn ameshindwa
 
Pole sana, tunamuombea afya
Mpeleke Hospitali kama Dar ni MOI.

Usisikilize upuuzi wa kwenda kwa mganga wala maombi,
sijawahi maisha mwangu kujua, kuona wala kushuduhudia mtu yeyeto aliye na critical illness kutibiwa na kupona na mganga wala makelele ya maombi.
 
Onana na Neurologist kama yupo pale MOI,

Inawezekana kuna tatizo katika mfumo mzima wa nyonga au katika mfumo wake wa kichwa....


PDX sciatica
 
Mkuu kwa mujibu ya maelezo yako huyo binti wako amekumbwa na upepo wa pepo mchafu Shetani ndio anaye msumbuwa utamaliza vipimo vyote vya hospitali na maradhi hayawezi kuyaona na hata ukimpeleka kwa wachungaji sio rahisi huyo pepo mchafu kumtowa. Nitafute mimi kwa wakati wako nipate kumtoa pepo mchafu aliye mkumba binti yako ili aweze kupona maradhi yake.
 
Kwa comment yako hii imenifanya nimuambie achezeshe vidole vya miguu lkn ameshindwa
Pole sana mkuu, naungana na wote wanaoshauri utafiti wa kisayansi, sikatai kuwa kuwa kuna mambo ya kienyeji lakini kwa case yako tafadhali zingatia sana sana vipimo vya kisayansi na tiba yake.
Fanya hivyo huku ukimwomba mwenyeezi mungu amponye binti yako inshaallah.

Sent from my D6616 using JamiiForums mobile app
 
Ni tatizo la moyo watoto huwa wanapata stroke.... Mpeleke hospital kubwa mwanangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…