Hao madaktari ni wazembe sana, especially uliowafata baada ya mwanao kushindwa kutembea, wajinga kama hao ndo hufanya mauaji hospital bila kujijua, nimesoma nao wengi, wengine wanafaulu ila mtu unajua kabisa huyu hafai na hana maamuzi sahihi
Anyways, ningependa kujua au ungemuuliza mwanao aliangukaje na akielezee kiufasaha kabisa bila kupindisha neno(every small detail matter), kuna possibilities nyingi za ugonjwa wake ila the most ovious sitaki kuikimbilia uku sijamuona mgonjwa kabisa,
Ukimshika mguu wake bila hizo dawa za maumivu inakuaje, na ukimbinya kidogo kwenye nyama za mapajani au kwenye kigimbi inakuaje??
Na je anaweza kuhamisha mguu wake ata kidogo kwa sasa??
Nijibu please, maana uku Jf ni kusaidiana
Ila kikubwa umeelezwa vizuri na baadhi ya watu humu, nenda muhimbili tafta daktari mzoefu na alieona mengi, uzuri matatizo ya binadam hujirudia, ukipata mzoefu yawezekana ashaona mengi ya ugonjwa huo na pia ashafanya makosa mpaka akajirekebisa
Kuna vipimo inabidi wavifanye kama MRI na kupima fluid iliyoko kwenye vertabral colum, ni maumivu ila hey, bora maumivu ya maramoja na diagnosis ikapatikana
Kibaya cha magonjwa mengi ni kuchelewa kufika hospitalini, hao madaktari wa mwanzo ilibidi wajiulize kwann mtoto anaumia na anachechemea wakati hakuna palipoumia, ilibid wajue situation iliyomkuta, ila myb myb nao wanapata wagonjwa wengi ambao matatizo yao sio serious ndo maana wakaja na hizo judgement
So please nenda muhimbili pia tafta madaktari wazoefu ata kama wamestaaf wafate kwenye hospital zao