Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Na
Safi Sana. Nijibu tu yote hapa. Umesema uko Mbeya na Mwani ni zao la Baharini. Inapatikana Sana DSM Yale maduka ya Kisuna na wanautoa Zanzibar. Binafsi ninautumia kama kirutibisho na tiba kwa mambo mengi hasa mifupa na misuli. Mwani au Seaweed iko ya Unga imesagwa na nzima. Ya Unga unakoroga kijiko kidogo cha chai kwa kikombe cha maji ya Moto unakunywa. Mtoto mpe nusu kijiko cha chai. Ulio mzima unachukua vipande viwili au vitatu unaloweka saa nzima(ni ngumu Sana) halafu unatafuna au unablend hata na matunda upate juice unakunywa). Itasaidia Sana. Kama Una ndugu mtume aende Kariakoo akutafutie akutumie. Ni maduka machache yanayouza Mwani hapo Kariakoo. Siku hizi mi ninaagiza Zanzibar maana bei pia iko chini kidogo Kwa 15,000 packet badala ya 20,000 Kariakoo. Naagiza za kunitosha hata 6 months. Ni food supplement nzuri Sana Kwa Sisi watu wazima umri umesogea mifupa na nerves zinachoka hivyo tuna boost.
Nashukuru mkuu nitajaribu kuulizia kwa Tanga kama nitaweza kupata nina ndugu wengi huko
 
MPELEKE KWENYE MAOMBI KWENYE MAKANISA YA KIROHO..ANZIA KWA NABII ROLINGA MBEZI BEACH AFRICANA..MUNGU ATAMFUNGUA
Hap Sasa ndio umuhimu wa kina mwamposa inaonekana
Nashauri tu kuwa ukiwa unaendekea pia na tiba za hospital maombi pia kazania mkuu
 
Nibinti wa miaka 10 ijumaa trh 11mar,2022 amerudi toka shuleni sa11 jioni akasema ameanguka akiwa anacheza mpira wamiguu nawavulana shuleni tukamuuliza umeumia? Akasema kidogo nikweli alikua anatembea kama anavuta mguu kwa mbali sana mamaake akamuangalia miguu ipo sawa haina uvimbe wala nini.

Jumamosi ameamka vzr akajiandaa kwenda shuleni(wanafanya mitihani kila jmos)kuulizwa maumivu akasema nikidogo akapewa dawa yamaumu akameza akaondoka.

Huku nyuma tukanunua dawa yakuchua alivyorudi tukamchua bas akaendelea kupumzika pamoja na root ndogo ndogo zadukani,

Lkn jumapili tukaona anazidi kuburuza miguu anatembea kwa shida bas muda mwingi akawa ndani tu.

Jumatatu akaamka akawa anashindwa kabisa kutembea yn anatembea kwa kujishikilia ukutani anasema anapata maumivu makali sana kwene nyonga tukampeleka hsptl akapigwa exray yamiguu yote pamoja na nyonga lkn majibu yakaja kuwa hakunamvunjiko wamoja kwa moja unnaonekana wakamchukua damu kwa vipimo vingine lkn pia hawajaona shida wakatupatia vidonge vyamaumivu tu kua aendelee kutumia pamoja naile dawa yakuchua atakuwa sawa,

Hadi Jumatano mtoto hali inazidi kuwa nbaya sasa miguu yote hawezi kusimama,kutembea wala kuitikisa yan hata kuisogeza mpaka aisapoti kwa mikono, ikabidi twende hsptl nyingine nayo wakampiga exray zamiguu na nyonga wakasema hivyo hivyo kuwa hawaoni mvunjiko wowote labda ninyama tu kikubwa apumzike muda mwingi wakatupatia vidonge vya maumivu na dawa ya kuchua lkn hadi leo mtoto bado hakuna unafuu wowote na usiku akilala huwa analalamika maumivu makali juzi ilibidi tuite nesi akamchoma sindano yamaumivu akalala vzr najana akashinda vzr bila maumivu ila miguu ndo ipo totaly disable niwakubeba nakusogeza kwakila alitendalo kufika usiku muda wakulala maumivu yakaanza upya nesi akaja akamchoma sindano lkn jana pamoja nakuchomwa sindano yamaumivu aliendelea kugugumia maumivu usiku kucha usingizi niwamang'amng'am yn akisinzia kidogo anaamka anagugumia maumivu,

Amekuja kuupata usingizi mzuri sa10 hapo ndo amelala hadi sambili bila kushtuka na ameamka bila maumivu lkn bado miguu haifanyi chochote naukijaribu hata kumsimamisha anapiga yowe kwa maumivu makali anayoyapata kwene nyonga.

NIMEKUJA KWENU WAKUU MNISHAURI NIFANYE NINI KUMUOKOA MWANANGU nahofia mwanangu asije akapata ulemavu wakudumu(Eeh Mungu aepushie mbali)
Kuna mmoja alikuwa shemeji yangu, yeye alianza kuumwa mkono, aisee kimchezo mchezo akapelekwa mloganzila, kakaa pale karibu mwaka mmoja akiugulia maumivu lakini vipimo vinaonyesha hakuna kitu. Ikachukuliwa sample kwenda India ila majibu yakarudi yale yale. 11th March mwaka huu amefariki. Huwezi amani kama mtu anaweza umwa mkono mwaka mzima mpaka akafariki. Sina nia ya kukutisha ila kukuambia usichukulie masihara kwani unaweza mpoteza binti yako. Angaika kadiri uwezavyo.
 
Mkuu usihangaike namwanao popote ispokua hospital. Mambo yamatibabu yanachangamoto nyingi Sana hasa kiuchunguzi navipimo lakin usichoke kuhangaika naukajitikomeza kwnye njia zisizo kitaalam,

Nimuhimu kubalance mambo ya imani najitihada zako kama mzazi. Weka Imani yote mungu atamponya ilajitihada 100% weka kwenye tiba zakisayansi. Wengi wanapotea kwenye hilo nakuwaumiza Zaid wapendwa wao

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Unachokisema kilimfanya mtu akapoteza binti yake(shemeji yangu) kwa kujua mtoto wake ana tatizo linaloweza tibika kisayansi.
 
Pole kwake, halafu pole Sana kwako! Ninaamini Ana shida zaidi ya mpira aliocheza, nashauri aende kwa daktary specially wa mifupa.

Ikishindikana huko pambana a na maombi, na sio Hawa manabii kama Mwamposa, hapana, watu wa kueleweka.
Ila babu usimidharau mwamposa mnk hata huyu wako Ni mtu tu Kama mwamposa

Muhimu Ni maombi
 
Pole mkuu nawasiwasi isijekua rare diseas kama ya mtoto wa masoud kipanya yule malcom au yule kijana wa Tanga jitahidi kuwaona wataalamu
 
Ila babu usimidharau mwamposa mnk hata huyu wako Ni mtu tu Kama mwamposa

Muhimu Ni maombi
Mwamposa binafsi huwa namwona kama tapeli au wakala wa shetani na hata KKKT aliwahi kufukuzwa. Japo inaweza kuwa kinyume chake.
 
Pole sana, tunamuombea afya
Mpeleke Hospitali kama Dar ni MOI.

Usisikilize upuuzi wa kwenda kwa mganga wala maombi,
sijawahi maisha mwangu kujua, kuona wala kushuduhudia mtu yeyeto aliye na critical illness kutibiwa na kupona na mganga wala makelele ya maombi.
Mm nilishashuhudia kabisa kijiji kwetu baba mmoja alipooza miguu ghafla walipeleka hosipital kupima hawaoni kitu ila alipoteza uwezo wa kutembea. Walileta mganga wa kienyeji ndani ya wiki yule baba alianza kuendesha mbaiskeli wanakijiji walikuwa wanashangaa na kushangilia miujiza. Haya mambo ushuhudie.Dunia Ina mengi yamejificha.
 
Kama wewe ni mkristo piga maombi
Kama wewe ni Muslim piga swala mkuu
Maombi maombi, acha upotoshaji ndugu. Nani alipona ugonjwa kwa kuombewa , toka lini kuongea kukatibu mwili wa mwanadamu
 
Mpeleke mhimbili haraka kwa madaktari wa neurosurgeon wakamwangalie, mtoto hajavunjika ila inaelekea kuna misuli imebanwa sehem
 
Zogwale, kama hutojali hebu leta faida kamili za mwani au seaweed, utakuwa umetufaidisha wengi, japo uzi hausiani na seaweed.

Sent from my D6616 using JamiiForums mobile app
Just Google Seaweed benefits also Seamoss benefits. Utaziona nyingi Sana. Ka packet nilicho nacho nacho kina benefits lukuki sema ndiyo hivyo Lugha gongana Sana.
 
Just Google Seaweed benefits also Seamoss benefits. Utaziona nyingi Sana. Ka packet nilicho nacho nacho kina benefits lukuki sema ndiyo hivyo Lugha gongana Sana.
Mwani nimeupata Jijini Tanga ambao haujasagwa wanapima kuanzia elf mbili,kilo moja 15000 sasa nimeambiwa kuna mwembamba na mnene sasa sijui best ni upi hapo mkuu
 
Mwani nimeupata Jijini Tanga ambao haujasagwa wanapima kuanzia elf mbili,kilo moja 15000 sasa nimeambiwa kuna mwembamba na mnene sasa sijui best ni upi hapo mkuu
Kaka, tujuze hali ya mtoto tafadhali.

Ulikwenda hospitali?

Vipimo vimeonesha nini?

Ana nafuu yeyote mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom