King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Inasikitisha Sana yaani hadi Gwajima naye anatoa maagizo badala ya kufatilia yeye kama yeye maana case imefika kwake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DED alifuatwa kuulizwa na mwandishi wa habari anajibu simple tu. " mtoto amekufa kwasababu ya cancer" pumbafu kabisa yaani hii nchi Ina viongozi wa ovyo mpaka unashangaa Huwa wanateuliwa kwa vigezo Gani?Pole mama.
Umasikini ni aghari, mama kitu cha kwanza haukutakiwa kuipokea hiyo shs. 20,000/=, kwa kifupi shule ilitumia udhaifu huo kukusukumia mzigo wewe mzazi, mzazi ulitakiwa ukaripoti polisi kwa hatua za kisheria badala ya kujadiliana na shule, pia shule ilitakiwa ichukue jukumu la matibabu ya mwanao wewe ukiwa msindikizaji tu.
Udhaifu wa kupokea ile pesa ili umpeleke hospitali ndiko kulikoifanya shule ikuambie gharamis upasuaji watakurudishia pesa zako, kwa kifupi walijitoa kwenye tatizo hilo.
Mama hapo Moshi ipo mamlaka ya wizara ya elimu inayosimamia shule zote, pia yupo mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ambao ulitakiwa uende ofisini kwao kuwajulisha kuhusu tatizo hilo.
Mwisho ulitakiwa upate ripoti ya kina mobiTuki yaani postmortem ya maiti. Hii postmortem inakuwezesha kufungua kesi ya jinai dhidi ya shule na mwalimu.
Mwisho, kabla ya kupeleka tatizo lako kwa Waziri anza na viongozi wa mkoani mwako, vinginevyo utadhani unakosa msaada kumbe ni njia ambazo si sahihi unazotumia.
Mkuu vijana wanaoenda kufanya field mashuleni wengi wao ni wadogo sana kiumri tofauti na miaka ya nyuma, japo haimaanishi ni halali kwa hilo tukio ila kiukweli wahitimu wengi wa ualimu elimu hawajakomaa kiumri, kimaadili na hata kiutendaji kaziPoleni sana Kwa Msiba huo...
Hivi inaingia akilini kabisa wewe Mwalimu mtu mzima uanze kumchapa mtoto hadi kumpiga na ngumi kabisa?
Angekuwa mtoto wako ungemfanyia hivyo?
Tuweni na kiasi jamani, it's unfair kumfanyia mtoto mdogo ukatili Mkubwa hivyo hadi kupelekea apoteze maisha🥲
Kuna wakati nilisoma mahali kwamba Viboko vimepigwa marufuku mashuleni hadi Kwa Kibali maalumu cha Mkuu wa Shule n.k na mwisho ilikuwa Viboko kama sikosei 2 ama 3, Je huyo Mwalimu alipewa kibali cha kumchapa huyo mtoto.
Basi Kuna haja waanze kupewa seminar ya maadili yao ya kazi.Mkuu vijana wanaoenda kufanya field mashuleni wengi wao ni wadogo sana kiumri tofauti na miaka ya nyuma, japo haimaanishi ni halali kwa hilo tukio ila kiukweli wahitimu wengi wa ualimu elimu hawajakomaa kiumri, kimaadili na hata kiutendaji kazi
Na Injinia Masaunidorothy Gwajima
Bila shaka utakuwa unaishi nje ya Tanzania maana haiwezekani ushangae mwananchi wa Hali ya chini kupuuzwa na viongozi wa serikali pale anapokuwa na shida.Mnabidi kusikiliza pande zote mbili
Ukiona huyo Dada anarushwa Amini something wrong to her
Ivi unayajua maticha yalivyo mapuuz mkuu ?Hivi Kuna mwalimu anaweza kukapiga ngumi katoto ka miaka 7
NAKAZIA KWA HERUFI KUBWAMwambie huyo mkuu wa shule asipokuonyesha huyo mwalimu basi yeye ndie utakaeshughulika naye,na ufanye kweli.