DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pole mama.

Umasikini ni aghari, mama kitu cha kwanza haukutakiwa kuipokea hiyo shs. 20,000/=, kwa kifupi shule ilitumia udhaifu huo kukusukumia mzigo wewe mzazi, mzazi ulitakiwa ukaripoti polisi kwa hatua za kisheria badala ya kujadiliana na shule, pia shule ilitakiwa ichukue jukumu la matibabu ya mwanao wewe ukiwa msindikizaji tu.

Udhaifu wa kupokea ile pesa ili umpeleke hospitali ndiko kulikoifanya shule ikuambie gharamis upasuaji watakurudishia pesa zako, kwa kifupi walijitoa kwenye tatizo hilo.

Mama hapo Moshi ipo mamlaka ya wizara ya elimu inayosimamia shule zote, pia yupo mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ambao ulitakiwa uende ofisini kwao kuwajulisha kuhusu tatizo hilo.

Mwisho ulitakiwa upate ripoti ya kina mobiTuki yaani postmortem ya maiti. Hii postmortem inakuwezesha kufungua kesi ya jinai dhidi ya shule na mwalimu.

Mwisho, kabla ya kupeleka tatizo lako kwa Waziri anza na viongozi wa mkoani mwako, vinginevyo utadhani unakosa msaada kumbe ni njia ambazo si sahihi unazotumia.
DED alifuatwa kuulizwa na mwandishi wa habari anajibu simple tu. " mtoto amekufa kwasababu ya cancer" pumbafu kabisa yaani hii nchi Ina viongozi wa ovyo mpaka unashangaa Huwa wanateuliwa kwa vigezo Gani?
 
Poleni sana Kwa Msiba huo...

Hivi inaingia akilini kabisa wewe Mwalimu mtu mzima uanze kumchapa mtoto hadi kumpiga na ngumi kabisa?

Angekuwa mtoto wako ungemfanyia hivyo?

Tuweni na kiasi jamani, it's unfair kumfanyia mtoto mdogo ukatili Mkubwa hivyo hadi kupelekea apoteze maisha🥲

Kuna wakati nilisoma mahali kwamba Viboko vimepigwa marufuku mashuleni hadi Kwa Kibali maalumu cha Mkuu wa Shule n.k na mwisho ilikuwa Viboko kama sikosei 2 ama 3, Je huyo Mwalimu alipewa kibali cha kumchapa huyo mtoto.
Mkuu vijana wanaoenda kufanya field mashuleni wengi wao ni wadogo sana kiumri tofauti na miaka ya nyuma, japo haimaanishi ni halali kwa hilo tukio ila kiukweli wahitimu wengi wa ualimu elimu hawajakomaa kiumri, kimaadili na hata kiutendaji kazi
 
Ina maana wiki hio au siku hio mtoto kachelewa aliyemuadhibu alikuwa ni mwalimu wa zamu kwa wakati huo, hapo cha kufanya angeuliza mtoto yeyote pale shuleni mwalimu wa zamu ni yupi, lakini pia kipindi ameadhibiwa wanafunzi wenzie walishuhudia naamini bado kuna nafasi ya kumtambua mwalimu alisababisha kifo cha mtoto.

Inasikitisha na kutia hasira, pole sana.
 
Mkuu vijana wanaoenda kufanya field mashuleni wengi wao ni wadogo sana kiumri tofauti na miaka ya nyuma, japo haimaanishi ni halali kwa hilo tukio ila kiukweli wahitimu wengi wa ualimu elimu hawajakomaa kiumri, kimaadili na hata kiutendaji kazi
Basi Kuna haja waanze kupewa seminar ya maadili yao ya kazi.

Kama wataendelea kufanya kazi Kwa mazingira hayo, hivyo vifo vitaendelea kuwa vingi Kwa Wanafunzi wetu.

Pia kama hawatapewa seminar, itapelekea wengine kuanza kutembea na wanafunzi wao wa kike, maana Kwa mazingira ya Vijijini ni kawaida kumkuta Mwanafunzi wa darasa la 5 ameota maziwa, kwahiyo wanaweza kujikuta wakaanza kuwaharibu mabinti zetu
 
Back
Top Bottom