Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Nnakumbana na changamoto hii kwa binti yangu. Yaani unachoeleza ndicho ninachokumbana nacho ila ni mdogo yuko la nne ila yani maswali ya common sense madogo tu kwake changamoto hata katika maisha. Sema mzazi mwenzangu kumbe alimwachishaga ziwa akiwa na miezi mitatu sijui ndio effect hiyo
pole sana !!
Atleast we unajua chanzo mi huyu kanyonyeshwa vizuri tu sema labda n matatzo ya upande wa mama ake labda
 
Tuanze na lishe unayompatia nyumbani, je ni mlo kamilii?.

Twende kwenye malezi unayompa hapo nyumbani, je ni malezi ya kumfanya aweze kujitegemeaa?

Tuelekee kwenye lugha ya mawasiliano kati yenu, je huwa unamkaripia/kumgombeza mara kwa mara?

Je, kwa wastani mwili wake upoje, je ni mnene, mkakamavu au lege lege?

Vipi anashiriki michezo yoyote shuleni kwao au hata hapo mtaani?.

Ni mwanao wangapi kuzaliwq kwenye hiyo familia yako?.

Graph yake ya makuzi kadi ya clinic ilikuwaje au ipoje kama bado upo nayo? (Ni muhimu sana kutunza hiyo kadi)

Ukimaliza hayo yote, vipi mwanao huyo ana mpenzi? Kama hana wewe kama baba yake umemsaidiaje hilo swala?. (Usishangae ni jukumu lako mshua)

Ukiona mwanao hawezi kucheka mbele yako inabidi ujitafakari upya kiongozi, kuna kitu kikubwa hakipo sawa kati yenu.

Tafakari hayo machache Mkuu mwenzetu, kila la heri.
Noted
 
mapenzi no hana hizo mambo hata kubalehe vizuri bado!!

zamani alikua muongo muongo vikatembea viboko had akaacha ila hilo la shule shida ipo tangu zamani !!
Ukikagua daftari lake lazima upate hasira

Mfano; kwene daftar amepata ila swali lile lile umpe afanye hawezi! hapo ndipo fimbo zilipoanza kuhusika
Atakuwa anakuogopa wakati mwingine wazazi ndio wanaharibu Watt ..kila kitu umkaripie, umchape, umpe maneno mia..unafikiri huyo mtoto atakuwaje?

Saikolojia ya mtt inaharibika na kitu kidogo sana ..kuwa makini pia ,kubwa kuwa rafiki yake...anza sasa, sasahvi
 
Kukaa na mwanangu kupiga naye stori kulimjenga sana. Hata sometimes kauli anazotoa kwa wenzie unajua kabisa kaiga kwangu au kufuata nachomfundisha

Akiwa Grade 3 tu nikaanza kumpa majukumu ya kujitegemea. Ana time table ya majukumu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Aamke kufagia uwanja, asafishe choo, amsaidie dada kuosha vyombo na ahudumie bustani. Jioni tunakaa kwenye kibweta kula stori za maisha na kumsikiliza mitazamo yake na kuiweka sawa.

Pale home kuna PS. Huwa nimewaruhusu madogo jirani walio bright wanakuja pale kucheza naye. Hata likizo huwa naangalia ndugu mwenye dogo bright basi namuomba aje kwangu likizo Anajifunza vingi sana.
Leo yupo grade 4 anajitambua sana na anajiamini.

Usimkatie tamaa, bado anaweza kubadilika huyo
Hayo ndio malezi mtoto anatakiwa apewe. Nakumbuka kabla hatujaanza shule mzee tulikuwa tunakaa naye njie jioni anatueleza mambo ya angani comets, meteors, stars. Ni vitu ambavyo siwezi kuvisahau mpaka nakufa. Ile bond aliotujengea ndio naijenga kwa watoto wangu pia.
 
Nnakumbana na changamoto hii kwa binti yangu. Yaani unachoeleza ndicho ninachokumbana nacho ila ni mdogo yuko la nne ila yani maswali ya common sense madogo tu kwake changamoto hata katika maisha. Sema mzazi mwenzangu kumbe alimwachishaga ziwa akiwa na miezi mitatu sijui ndio effect hiyo


Ultimation of parenting is to make ur daughter to be productive to herself even in her society.

Endelea kujifunza zaidi ili uamishie huo ufahamu to ur daughter is possible
 
Amesema shule ya msingi boarding au day? Na o level vipi boarding au day?

Watoto wa dada yangu wamesoma boarding kuanzia shule ya msingi, mmoja ana division 1 na mwingine ana 2,

Kwa hiyo darasani wako vizuri ila akili za mtaani ndo changamoto, kuna malezi wanakosa.

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Sasa kwa ulimwengu wa sasa akili za mtaani ndio zinatakiwa ziwe nyingi kuliko za darasani otherwise utawalea watoto hadi umri wao wa kustaafu. Kama usipowapa kazi😁!!!
 
Sasa kwa ulimwengu wa sasa akili za mtaani ndio zinatakiwa ziwe nyingi kuliko za darasani otherwise utawalea watoto hadi umri wao wa kustaafu. Kama usipowapa kazi😁!!!
kwaiyo bro saizi ww ni nani au unafanya nn!?

maana umenitisha na yale matokeo yako!!
nipe kaushuhuda atleast nilegeze kamba kwa kijana wangu
 
Sasa kwa ulimwengu wa sasa akili za mtaani ndio zinatakiwa ziwe nyingi kuliko za darasani otherwise utawalea watoto hadi umri wao wa kustaafu. Kama usipowapa kazi😁!!!


Azingatie kumfanya mtoto kuwa na tija tu

Akiwa na tija tayari atakuwa na potential na akiwa na potential atakuwa marketable to his her career

Then ajitahidi kuulewa mtaa ili ajilinde dhidi ya uraibu , Kama ,drugs, alcohol ,sex ,gambling and so on .

Kumlea mtoto kuwa productive ni vita kati ya intangible stuffs vs tangible stuffs

Aendelee kuwa patience hata mawaziri , na matajiri tunaona
huwa wanakwama Sana , mfano nyerere watoto wake .nk.
 
Back
Top Bottom