Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

well ! ukaribu si mdogo kiivo kwa maana mimi ndo namlea tangu 2019 had leo
 
Kumsaidia mtoto ni vizuri kwanza umuelewe. Unaweza kua wewe unamuona hivyo ila yeye anajiona tofauti. Kwa kua wewe ndio mzazi na unataka kumsaidia tafuta kumjua bila judgements zozote kwanza.

Kama hamna urafiki kiasi cha yeye kujiamini around you. Jaribu haya yafuatayo
1. Chunguza marafiki zake wa karibu, tabia unayoiona kwa rafiki zake ndio tabia halisi ya mwanao (tofauti hua ndogo sana)

2. Chunguza mda wake mwingi anatumia kufanya nini, chunguza interest zake bila kumuuliza direct.

3. Ili kujua vizuri nini anawaza siku mpe karatasi aandike anajionaje baada ya ten years from now, them utaweka 5 years an mwisho utamalizia the next day.
NB. Usimpe hii peke yake hata kama lengo ni kutaka kujua ya huyu mtoto pekee wape watoto wote waliopo hapo nyumbani. Na kila mtu aandike kivyake. kisichukue dakika nyingi ila akishindwa mpe hata siku nzima.
Atakachokiandika utaangalia consistency na kama kina maana. From there unaweza ukapata kumjua kidogo ili ujue pa kuanzia.

Common Sense is not Common 😂
 
Mzee baba,


1. Mchukulie mwanao jinsi alivyo.

2. Epuka sana kufananisha werevu wake na watoto wengine au wewe.

3. Muonyeshe upendo ajue kwamba unampenda bila kujalisha werevu wake.

4. Kumuelewa mtoto wako ni muhimu zaidi kuliko hayo masomo unayongangania aelewe.

5. Pia watoto huwa wanatofautiana vipaji, talanta na vipawa mbalimbali. Tambua kipawa au kipaji chake

6.Epuka kumfokea na kumsema sema mara kwa mara au kumpiga kwa mambo ambayo yapo nje ya uwezo wake.

7. Hakikisha unampa muda wa kuwasiliana au kumtembelea mama yake mzazi kama yupo hai angalau kipindi cha likizo kubwa.

8. Akifanya vizuri hata kama ni kidogo onyesha kumsifia na kumpongeza, itamuongezea kujiamini.

9. Kama mtoto ni slow learner na uwezo wake wa kuelewa ni taratibu nenda nae taratibu pia, ikiwezekana apate remedial class au masomo ya ziada kwa ajili yake tu.

10. Thamani ya mtoto au mtu haiko katika werevu au akili tu, Kuna watoto wamezaliwa na utindio wa ubongo au changamoto mbalimbali ila ni jukumu lako kama mzazi au jamii kuwapenda na kuwachukilia jinsi walivyo.
 
Nina mtoto wa dada yani toka std 1 akifaulu sana ni wa pili kutoka mwisho hata form 4 ni kuungaunga hadi kamaliza, mama ake kachapa, fundisha sana yani unaweza fundisha 1+1=2 dk2 ukimuuliza tena kasahau ila sasa mpe asimamie biashara hapo hapotezi hata 100 na anajua kutengeneza faida ikabidi amsapoti na biashara tu ndipo alipo vizuri
 
View attachment 2987076mambo upendayo haya😂 shule 24/7
😂😂😂apana mkuu,,, furaha yangu ni kuona mtoto akirudi anaelewa nn amejifunza siku hiyo!!
Na vimaswali au vimitihan vidogo vidogo havimsumbui….
sasa mkuu mtoto anakula asubuhi, anapewa hela ya shule, hapangiwi kazi anarudi matokeo marksi ni 27% F Kweli we usiumie?
 
Atleast sasa huyo biashara anaijua
 
Shukuru sana, wa hivyo ndo hutoboa hapa bongo ila wale vipanga, smart, faster, akili sharp huwa wanakuwa target na wanabaniwa ngumu kutoboa ila slow ka huyo wanga hawahangaiki nae maana sio tishio kimafanikio mwishowe anatoboa kiulaini, hii ndo bongo
 
Inaonekana ulimlea kwa sheria kali sana na ulikuwa unamuadhibu kwa kiboko mara kwa mara. Hiyo ilimjengea hofu,uoga na kutokujiamini. Kwa pamoja vitu hivyo vilitawala akili yake kiasi cha akili kukosa fursa ya kujifunza zaidi ya kuwaza adhabu na bakora kutoka kwako. Malezi ya kufoka foka huleta matoto yenye tabia kama za mwanao
 
Ndio mkuu sikatai kwa upande mwingine lakini kiasiri mtoto ni mwoga sana !!
nadhan pia kuna mahusiano ya utoto wake na kipindi cha mimba
 
Nyinyi ndo nyie wazazi mlio amini mtoto akicheza na watoto wenzake atafundishwa tabia mbaya mkaamua kumfungia ndani Aishi.
Anyway wadau watakuja na best solution kuwa mpole ndugu
 
Ndio mkuu sikatai kwa upande mwingine lakini kiasiri mtoto ni mwoga sana !!
nadhan pia kuna mahusiano ya utoto wake na kipindi cha mimba
Hapana kabisa. Tatizo umemlea ukiwa na matokeo yako mfukoni. Ulitaka awe kama unavyotaka kwa kutumia Fimbo na vitisho. Huo unaoona ujinga au kutokuwa na uwezo wa kufikiri! Ndicho kitu ubongo wake umeona afanye ukidhani ndicho unachotaka ili bakora na ukali wako umuepuke. Kumbe ndio nakosea zaidi na kuzidi kwenda tofauti na matokeo yako uliyonayo mfukoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…