Tuanze na lishe unayompatia nyumbani, je ni mlo kamilii?.
Twende kwenye malezi unayompa hapo nyumbani, je ni malezi ya kumfanya aweze kujitegemeaa?
Tuelekee kwenye lugha ya mawasiliano kati yenu, je huwa unamkaripia/kumgombeza mara kwa mara?
Je, kwa wastani mwili wake upoje, je ni mnene, mkakamavu au lege lege?
Vipi anashiriki michezo yoyote shuleni kwao au hata hapo mtaani?.
Ni mwanao wangapi kuzaliwq kwenye hiyo familia yako?.
Graph yake ya makuzi kadi ya clinic ilikuwaje au ipoje kama bado upo nayo? (Ni muhimu sana kutunza hiyo kadi)
Ukimaliza hayo yote, vipi mwanao huyo ana mpenzi? Kama hana wewe kama baba yake umemsaidiaje hilo swala?. (Usishangae ni jukumu lako mshua)
Ukiona mwanao hawezi kucheka mbele yako inabidi ujitafakari upya kiongozi, kuna kitu kikubwa hakipo sawa kati yenu.
Tafakari hayo machache Mkuu mwenzetu, kila la heri.