Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Una lolote la kusema kwa Nchimbi tunayemjua? Tuliyewahi kumjadiri kwa tabia yake tangu Umoja wa Vijana na hatimaye waziri wa mambo ya Ndani, na wote waliouwawa akiwa waziri?
 
Huna lolote wewe. Si Makonda wala CCM yenyewe ambayo imefikiria kumuweka Makonda kwenye Ukatibu Mkuu. CCM imedhamiria kumuweka mtu mwenye nasaba ya utu uzima. Akina Makonda wanalelewa kwa ajili ya CCM ya kesho.
 
Una lolote la kusema kwa Nchimbi tunayemjua? Tuliyewahi kumjadiri kwa tabia yake tangu Umoja wa Vijana na hatimaye waziri wa mambo ya Ndani, na wote waliouwawa akiwa waziri?
Wewe umeshasema na umeanzisha takataka yako thread, unataka kumlisha mtu Maneno kwa ajenda zako binafsi?

Huwa nawaambia watu hapa kila siku Ccm ni laana kwa Taifa letu.
 
km ni kweli ndio mwanzo wa kuanza kumdharau huyu rais Samia, sintamfuatilia tena, atakuwa ameiuza nchi yetu kwa wahuni. Nilishasemaga Makonda ana akili ndogo sana, km kweli tunaongozwa na akili km za mtu km Makonda bora tuhame nchi, maana imekuwa nchi ya mazezeta. Hivi Samia amejikwaa wapi? Tayari ameshauza chama, juzi anaenda kumsalimia Mabeyo, kwani ndio mkuu wa majeshi mstaafu pekee? Je kina Mboma, Waitara na Mwamunyange siyo wakuu wa majeshi wastaafu? Ni mambo ya sukuma gang, ni ukabila wa wazi. Kwani Makonda kuwa mwenezi ana tofauti gani na wenzake waliokuwa na hiyo nafasi? Bwana mdogo amekuwa zaidi ya Katibu mkuu wa chama na mama anafurahia, mzanzibari kweli mdebwedo. Asubiri atakapotaka uenyekiti wa chama kwamba cheo cha urais kitenganishwe na uenyekiti wa chama ndio atajua yuko na joka

Na hakuna kitu cha namna hiyo cha kutenganisha chama na serikali kitatokea. Wewe kwa hilo endelea na kilio cha samaki! Kuhusu rais kusalimia majenerali mimi nafikiri atawasalimia tu atakapokuwa amefika maeneo yao wanakoishi! Hata Msuguri aliyezaliwa 1920 na ana zaidi ya miaka 103 hadi sasa ataenda kumsalimia tu. Msuguri ndiye mkuu wa majeshi mstaafu mwenye umri mkubwa kuliko wote uliowataja, kwa hiyo poa tu. Nyerere alizaliwa 1922 lakini Msuguri 1920.
 
Tupatupa mwaga vitu
FB_IMG_1697694483207.jpg
 
Makonda kupewa ukatibu mkuu.... Either kupendekezwa...

... Itakuwa ni dharau kuu kupita yoyote Ile iliyowahi kutendeka ndani ya CCM tangu kuundwa kwake!

Hata huyo atakaempendekeza MAKONDA... ...naye Atakuwa (hamnazo!) Hana akili vilevile!...

Ccm inapita katika kikaango.....katika kipindi hiki cha mpito... Kuelekea 2024/25

Kosa likifanyika muda HUU... Kurekebisha ni vigumu sana!...

Nawaona wabunge wengi wa CCM kutokurudi bungeni...
Either Kwà kutopitishwa majina yao... ama kukatwa wazi wazi!...(juu kwa juu)

Yule mwenezi ana roho mbaya sana ya kisasi ... Hata kama mlikwazana Jf tu!
 
Makonda kibinafsi napenda sana
Uwezo wa uwajibikaji wako,
Uwezo wa kutetea na kutoa hoja,
Uweza wa kuisemea Serikali yetu,
Uwezo kukisemea chama chetu,
Uwezo wa kumsemea Rais wetu,
Uwezo wa kuwasemea viongozi
Chapa kazi!! Tunaimani na wewe
CCM iendeleee kuwa imara
 
Kama kweli alikuwa anaongea hayo maneno basi huyo Jamaa atakuwa ana tamaa sana aisee.

Pili ingependeza sana Said Mtanda RC wa Mara awe Katibu Mkuu ila naona haitaweza kutokana na mambo yenu ya udini maana itaonekana safu nzima ni Waislamu.
Huyu aliyekuwa Dc Nkasi kajitwalia open space na kujenga jengo kiaina na kuwalazimisha crdb wapange kwake? Kweli ccm hakuna msafi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani u KM,huko ccm unaombwa na muhusika ama mwenyekiiti ndio anaamua.

Wewe ukiwepo utazuia asiteuliwe kwani mnapigakura?.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Ndio hapo sasa. Kwa Sasa ccm imefika mahali atakacho mwenyekiti kwakuwa ana kofia ya urais lazima kitimie. Kura ni kutimiza taratibu lakini hazina madhara yoyote. Magufuli alipanda mbegu ya ushindi wa 100% bila hata kura Moja kukataa au kuharibika.
 
Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Nimekumis mzee wangu... Ila nashukuru kumbe nawe upo hapo kutujuza, nakuaminia Sana... Mpigeni stop dogo sifa haja acha bado,!
 
Back
Top Bottom