Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hivi hali ya kupanda gharama za maisha huko kwenye vikao vyenu huwa hamjadili kabisa?

Naona LATRA wameamua kuwatengea penalty wapinzani.
 
Attachments

  • Screenshot_2023-08-17-16-20-08-01.jpg
    Screenshot_2023-08-17-16-20-08-01.jpg
    34.9 KB · Views: 1
km ni kweli ndio mwanzo wa kuanza kumdharau huyu rais Samia, sintamfuatilia tena, atakuwa ameiuza nchi yetu kwa wahuni. Nilishasemaga Makonda ana akili ndogo sana, km kweli tunaongozwa na akili km za mtu km Makonda bora tuhame nchi, maana imekuwa nchi ya mazezeta. Hivi Samia amejikwaa wapi? Tayari ameshauza chama, juzi anaenda kumsalimia Mabeyo, kwani ndio mkuu wa majeshi mstaafu pekee? Je kina Mboma, Waitara na Mwamunyange siyo wakuu wa majeshi wastaafu? Ni mambo ya sukuma gang, ni ukabila wa wazi. Kwani Makonda kuwa mwenezi ana tofauti gani na wenzake waliokuwa na hiyo nafasi? Bwana mdogo amekuwa zaidi ya Katibu mkuu wa chama na mama anafurahia, mzanzibari kweli mdebwedo. Asubiri atakapotaka uenyekiti wa chama kwamba cheo cha urais kitenganishwe na uenyekiti wa chama ndio atajua yuko na joka
Ndugu saigilomagema, umepanga kuhamia Nchi Gani?

Uhai wa chama chakavu, Si zaidi ya 2026.
 
Ujinga tu...kwani mlikuwa wapi kutafuta mtu kipindi chama kinayumba....utazuia ili umlete nani...mkiulizwa makonda kawakosea nn...? Hamsemi..ila hamtaki Ateuliwe... si mseme kawakosea nn?
Huyo mtu hafai hata kidogo. Hukumbuki enzi ni mkuu wa mkoa ujinga aliokuwa anafanya. Bashite, wewe na Jiwe ni kitu kimoja
 
Ile tu kwamba Makonda ni muenezi wa chama, wakati wewe ulikuwa unamsagia sumu siku nyingi, inaonesha kabisa wewe ni kidagaa tu hapo ccm na huna la kufanya wakubwa wakiamua.
Mama alikosea sana kumleta Bashite. Huyu ilitakiwa awe jera
 
Nasikia polepole ana rudi .....kosa kubwa na lakipumbavu alilofanya samia ni kuwasikiliza wahuni wa msoga kwa kumuondoa polepole chamani ...polepole alikuwa anajua nini maana ya chama tawala na nini maana ya chama cha siasa...kwa sasa samia anajaribu kucheza karata zake za mwisho baada ya za mwanzo kuzikosea ..samia yupo kwenye karata za kufa na kupona sasa hivi ana maadui kila pande.
Uko sahihi kabisa mkuu, hata sisi wachache tuliokuwa tunamuunga mkono kwa sasa hatumtaki tena. Unamleta Bashite, kweli [emoji848]
 
Kuna mkubwa zaidi ya mwenyekiti kwenye chama na serikalini kuna mkubwa zaidi ya Rais?
Angekuwa Rais ndio mkubwa mno, Jiwe asingeondoka huku anapenda kuishi!
Msidanganyike na hizi power za kuchonga, kuna mizizi imeota zaidi na haionekani.
Hata dada mkuu aache kujidanganya au kudanganywa na hao Wakolomide, wanavimbisha makalio na kutembea kwa mbwembwe na bado wakituhumiwa kuhusu mauaji wanaishia kujibu "kamuulize mama yako"
 
Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
(Paraphrase) Tumepokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wetu, Ndugu Daniel Chongolo. Tumeridhia. Tunafanya uchunguzi na jambo hili linaweza likachukua muda kukamilika, kwa sababu hiyo Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara) utakaimu hadi hapo taarifa ya uchunguzi itakapokamilika…. (Haya ni maneno ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kikao cha NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 
Back
Top Bottom