Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
141102225115_warioba_vurugu_304x171_bbc_nocredit.jpeg
 
Kazi imeanza!!
Mama anataka mtu strong mwenye uwezo na asiyekuwa na uoga wa kuwadhibiti wahuni aliowaainisha Polepole kuwa wapo Chamani wanaojifanya wao ndio Alfa and Omega ndani ya Chama !!

Ngoja Tusubiri tuone !! 🙏🙏
 
Jamaa akipewa hiko cheo basi ntaamini kwa namna moja bibi kaamua kugawana chaga maana huu muungano huwezi uendea direct watakuzima ..ila unatumia indirect way ili bara wachukue chaga zao na visiwani like wise.. ni mchakato ila utafanyika bila watu kujua mpk kishindo kikisikika.

Unafanya matumizi sahihi ya ubongo wako… umewaza nje kabisa, safi.
 
Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hajatulia. Apoze matako yake kwanza ndo aungwe.
Nasikitikia teuzi. Zuhura Yunus please mshauri dada vyema. Naita dada maana mimi ni dada yake ila kicheo simkuti.
 
Kwa vilaza kama wewe ataponzwa kweli ila kwa wenye akili Makonda ni kijana safi na mchapakazi
Shida yako wewe ni uchawa unakusumbua na unashidwa kufikiri kwa kutumia akili. Kazi hipi Makonda anaifanya na alishaifanya? Kinachokuvutia wewe ni ubabe wake, majibu ya hovyo, siasa za kukomoana na usanii sanii anaoufanya.
 
km ni kweli ndio mwanzo wa kuanza kumdharau huyu rais Samia, sintamfuatilia tena, atakuwa ameiuza nchi yetu kwa wahuni. Nilishasemaga Makonda ana akili ndogo sana, km kweli tunaongozwa na akili km za mtu km Makonda bora tuhame nchi, maana imekuwa nchi ya mazezeta. Hivi Samia amejikwaa wapi? Tayari ameshauza chama, juzi anaenda kumsalimia Mabeyo, kwani ndio mkuu wa majeshi mstaafu pekee? Je kina Mboma, Waitara na Mwamunyange siyo wakuu wa majeshi wastaafu? Ni mambo ya sukuma gang, ni ukabila wa wazi. Kwani Makonda kuwa mwenezi ana tofauti gani na wenzake waliokuwa na hiyo nafasi? Bwana mdogo amekuwa zaidi ya Katibu mkuu wa chama na mama anafurahia, mzanzibari kweli mdebwedo. Asubiri atakapotaka uenyekiti wa chama kwamba cheo cha urais kitenganishwe na uenyekiti wa chama ndio atajua yuko na joka

Yaani unajipinda kuandika kiasi hiki ili tu umuambukize Rais uoga wako?

Kwamba wewe unajua sana kuliko Rais wa nchi?!

Kuhusu Mobeyo, tuliza ubongo halafu itafute hotuba yake wakati wa maziko ya Rais aliyepita.

Acha ukabila.
 
Shida yako wewe ni uchawa unakusumbua na unashidwa kufikiri kwa kutumia akili. Kazi hipi Makonda anaifanya na alishaifanya? Kinachokuvutia wewe ni ubabe wake, majibu ya hovyo, siasa za kukomoana na usanii sanii anaoufanya.
Kuna wakati watu wa namna hiyo wanahitajika sana ili kuwadhibiti wahuni !!
 
Hajatulia. Apoze matako yake kwanza ndo aungwe.
Nasikitikia teuzi. Zuhura Yunus please mshauri dada vyema. Naita dada maana mimi ni dada yake ila kicheo simkuti.
Ni kweli, mama asipotulia hawa power mongers na machawa wao watamwangusha. Shida yao si kumusaidia bali ni vyeo na ulaji, wengi ni wanafiki.
 
Ndio hapo sasa. Kwa Sasa ccm imefika mahali atakacho mwenyekiti kwakuwa ana kofia ya urais lazima kitimie. Kura ni kutimiza taratibu lakini hazina madhara yoyote. Magufuli alipanda mbegu ya ushindi wa 100% bila hata kura Moja kukataa au kuharibika.

Waasisi wa kupita bila ‘kupingwa’ tumewasahau mara hii mpaka kumbebesha lawama marehemu?

Ile team ya campaign CCM 2014-2015 itadumu katika history ya nchi hii kwa karne nyingi sana. Pengine ikaibuka tena 2024-2025?
 
Ni kweli, mama asipotulia hawa power mongers na machawa wao watamwangusha. Shida yao si kumusaidia bali ni vyeo na ulaji, wengi ni wanafiki.
Nchi ni yetu wote lakini CCM inainadi kama yao wakati tunautafuta uhuru na ujamaa walikuwa hawajazaliwa au wapo kimya. Sasa tunakaa tunaangalia nchi wanaikorofisha na tunakaa kimya, kisha kufirisiwa mali, kunyanganywa vuwanja na zaidi kuambiwa wewe siyo raia kisa umetoka pembezoni.
 
Hivi hali ya kupanda gharama za maisha huko kwenye vikao vyenu huwa hamjadili kabisa?

Naona LATRA wameamua kuwatengea penalty wapinzani.

Mtu ananunuliwa hadi socks na malapa atayajuaje ya gharama za maisha kupanda?

Mtu ambae hajui Bei ya lita moja ya gas zaidi ya kusoma taarifa za EWURA kwenye makaratasi hawezi kuelewa kupanda kwa gharama za maisha.
 
Waasisi wa kupita bila ‘kupingwa’ tumewasahau mara hii mpaka kumbebesha lawama marehemu?

Ile team ya campaign CCM 2014-2015 itadumu katika history ya nchi hii kwa karne nyingi sana. Pengine ikaibuka tena 2024-2025?
Hakuna mwenye ubavu huo. Waliotangulia mbele ya haki walikuwa na ubavu hasa.
 
Back
Top Bottom