Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Mi naona yuko sahihi dogo, sababu Referee=Mwamuzi/Msuluhishi


Mfuate mwalimu, huenda amepitiwa....
 
Nafikiria dogo kwelie janja mingi ila ili jibu liwe refarii, hapa watu wa kiswahili inabidi waconfirm kama hilo neno limetoholewa rasm kwenye lugha yetu, vinginevyo tafsiri ya referee ni mwamuzi, dogo kapatia.

yes kapata kabisa refarii haipo kwenye kiswahili ukisha sema refarii thats referee moja kwa moja kudos kwa huyo dogo atakuwa ana akili mingi sana sababu inawezakuwa kapata hilo swali moja kwa moja
 
Kwa elimu yetu ya ukasuku ambayo siku ya mtihani mtoto anatakiwa kwenda kuyatapika yale aliyomezeshwa na mwalimu, na sio mawanda na mapana ya uelewa wake. Hapa mtoto wako anakuwa amekosea. Hakufundishwa hivyo.

Andika definition ya kitabuni kama unataka kufaulu mtihani- alisema professa wa Ranchodadas Chanchad!!
 
Mwamuzi tayari ipo kwenye swali, sasa angejiongeza fasta..
 
So kwako Mwalimu kutukanwa ni sawa na haikuumi...hii ni hekima kweli ??

Mkuu daaah basi bwana I am sorry kama hii inakuofend moja kwa moja mzee, ila unachukulia vitu too personal
 
Rejea kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu uone. Huenda tamko "Referee" limetoholewa na likawa "Refa" kwa Kisawahili.

Ila huko google uliporejea jibu lao lina ukakasi sababu hatujui huyo aliyeweka maana ya hiyo kwa Kiswahili amerejea wapi.

Almuhimu kama rejea inasema ni Muamuzi,basi mwalimu amekosea a atakiwa kusahihishwa na aambiwe.

Ni hayo tu.
 
Uwanja wa kuchora mti, mwlm kambania kwakweli.
 
Uwanja wa kuchora mti, mwlm kambania kwakweli.
 
Niko form two tukagewa mtihani ambao ulikua na section ya Question Tags.

Sikumbuki swali ila lilikua la 'I am ...' so naassume..

I am a doctor, ... ?

Mi nikajibu ' ain't I?' nikakosa.

Nikaenda kwa mwalimu kulalamika akanijibu siyo kwamba haupo sahihi lakini sahihi zaidi ni 'aren't I?'

Nafikiri inaapply kwenye swala la hili swali. Mahakamani kuna watu wanafanya maamuzi, bungeni, mpaka kwenye maswala ya ndoa. Plus kutokana na kiswahili kukosa misamiati mingi tunakopa sana maneno hivyo mwalimu kuweka hiyo nyanjo siyo kwamba mtoto hayupo sahihi ila sahihi zaidi ingekua 'refarii'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…