TANZIA Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyechomwa moto na mpenzi wake kutoka Kenya afariki dunia

TANZIA Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyechomwa moto na mpenzi wake kutoka Kenya afariki dunia

Mwanariadha wa Uganda wa mbio za Marathon, Rebecca Cheptegei amefariki dunia leo hii Septemba 5, 2024 wakati akipatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa petroli kisha kuchomwa moto na mpenzi wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Nation ya nchini Kenya, umauti umemkuta katika Hospitali ya Rufaa ya Moi huko Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya ikiwa ni siku mbili tangu kudaiwa kuchomwa moto na mpenzi wake Dickson Marangach, huku sababu ikitajwa ugomvi uliosababishwa na mgogoro wa kiwanja pamoja na nyumba.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk Owen Menach ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki na Upasuaji, amesema Cheptegei, aliyelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), amefariki dunia saa 11 alfajiri ya leo.

“Inasikitisha kwamba tumempoteza mgonjwa mapema leo asubuhi baada ya viungo vyake vyote kuharibika saa kumi na moja asubuhi tulipokuwa tukijitahidi kuokoa maisha yake Dk Menach amesema

Snapinsta.app_458391606_942489817643127_3145154513902031263_n_1080.jpg
 
Kwani mwanaume inakuwaje mpaka uchomwe mke wako moto? Ni kweli wanawake wana maudhi mengi lakini ukiona mambo ni magumu na huwezi vumilia si mwanaume unaondoka kwa amani na kwenda kuanza maisha upya na ikiwezekana utafute mwananmke mwingine? Utagombaniaje mali na mwanamke? Huyo mwanaume sheria zichukue mkondo wake ikiwezekana anyongwe hafai kuishi kabisa ili kesho asiue wanawake wengine.
 
Kwenye hizi posts, wanaume huwaoni. Ingekua mwanamke ndo amemchoma moto mwanaume wangesimamisha mishipa hapa.

Saizi dunia inaharibiwa na hao hao wanaume. Baba mzazi anabaka mtoto wake alafu yanakaa kuteteana. What a gender
Kwanza habari ililetwa juzi wakabadilisha jinsia za wahusika, wanaume ni mashetani sio mbwa tu
 
Unamchoma mtu moto na wewe moto unakushika.

unayemchoma anaungua sana wewe unaungua kidogo,wote mnapelekwa hospital
anhaa hapo sawa, kwahiyo Bwana Dickson ngumi aliona hazitoshi, sasa akishauguza majeraha anakutana na gereza linamuita
 
Back
Top Bottom