Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

Pungunza mihemko ya kishabiki pasipo hoja.. unapiga Kelele kushabikia uchafu kama wale nzi WA KIJANI chooni [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Alafu aliyekwambia Mimi Ni chadema Nani?.. Mimi Ni CCM kitambo sana
Ccm hatuna watu wa ovyo
 
Watanzania wanaswagwa kama mifugo kila mtu katika mafungu yao iwe wanafunzi wa vyuo vikuu, kada ya ualimu, mkata mkonge, wanasheria nguli, madaktari, wakulima, wafugaji n.k hawana umoja wakiona mmoja wa watu ktk kundi lao au katika wingi wao wakidhulumiwa wote hubaki kufukiria kulia mayowe au kuombea atokee mwokozi mmoja awatetee.

Ukisoma historia ya Tanganyika ya mkoloni wafanyakazi wa reli waligoma, makuli bandarini waligoma, wakata mkonge mashambani waligoma, wafanyakazi wa serikali waligoma ila zama hizi serikali ya CCM inauliza unamgomea nani wakati sisi (wakoloni weusi) tunatalawa hamuoni mkosa uzalendo !

Mtindo huu watanzania wa zama hii kuchangua kukaa kimya pale mtu au kikundi fulani kinapodhulumiwa haki yake unawapa kiburi wakoloni weusi waliochukua uhuru wa bendera kutoka kwa wakoloni weupe wawe wakandamizaji kuliko mkoloni mwingireza ambaye aliruhusu vyama huru vya wafanyakazi, vyama huru vya kitaaluma, vyama huru vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama huru vya wanafunzi n.k

N.B

MGOMO WA MAKULI WA BANDARI TANGANYIKA MWAKA 1939

National Library of Australia
https://trove.nla.gov.au › article
11 Aug 1939 - STRIKE IN TANGANYIKA - Trove


Police and troops were called out at Dares-Salaam, the capital of Tanganyika (British East Africa), to-day to deal with native dock workers

SIKU 82 MFULULIZO BILA KIKOMO ZA MGOMO WA WAFANYAKAZI TANGANYIKA

The East African Railway Strike, 1959-60: labour's challenge of ...

21 Jan 2018 — By May 1959 events were taking a sharp turn in Tanganyika as some long service higher grade African workers...

The History of the EAR&H Tanganyika Road Services

The Strike In 1960 the Tanganyika Railway African Union called it members out on strike, over a pay dispute, for 82 days from Tuesday
 

Attachments

  • 1690896333928.png
    1690896333928.png
    384 bytes · Views: 1
  • 1690896334053.png
    1690896334053.png
    784 bytes · Views: 1
Watanzania wanaswagwa kama mifugo kila mtu katika mafungu yao iwe wanafunzi wa vyuo vikuu, kada ya ualimu, mkata mkonge, wanasheria nguli, madaktari, wakulima, wafugaji n.k hawana umoja wakiona mmoja wa watu ktk kundi lao au katika wingi wao wakidhulumiwa wote hubaki kufukiria kulia mayowe au kuombea atokee mwokozi mmoja awatetee.
Wakina mwijaku steve nyerere babalevel kumbuka eti ndiyo wanathaminiwa [emoji1]

Ova
 
Zama za kutisha watu kisa vyeti ziliisha miaka mingi iliopita
 
Nasisitiza Tena naTena

Wakati tulipo fiwa na Raisi tulisikia fununu katiba ilitaka kupindishwa Makamu wake asishike Uraisi kama katiba inavyo elekeza

Tuliambiwa Mkuu wa JWTZ aliokoa jahazi

Nasasa katiba inavunjwa kumilikisha Mali bila kufuata katiba

Hivyo ni wakati wa Mkuu wa JWTZ Tena kuingilia jambo hili

Hivi hao wajanja wakifanikiwa kutupora sehemu ya Ardhi huyo Mkuu wa JWTZ atakuwa na mamlaka ya kulinda sehemu hiyo Tena

Jamàni tuwe siriasi na nchi yetu au kwavile tuliipata Kwa amani

Mnataka wajukuu wake kukomboa Kwa vitaaa!!
Ni kweli
Ila hakuna mkuu wa JWTZ kuna
mkuu wa majeshi anatoka
Au Chief of Defense Forces (CDF)

Huyu ni mkuu wa majeshi yote combined.
 
Hapa ingetakiwa wananchi tuwe wakali hasa. Hawa wameshaona sisi huwa hatuna cha kufanya zaidi ya kulalamikia mitandaoni.
 
Hapa ingetakiwa wananchi tuwe wakali hasa. Hawa wameshaona sisi huwa hatuna cha kufanya zaidi ya kulalamikia mitandaoni.
Samia kashawasifia, kasema "Watanzania warahimu sana".

Tafsiri, anasema hamuwezi kumfanya chochote. Hata kwenye kura alisema mkimpigia kura au msipompigia kura, ana uhakika wa kushinda.
 
Yuleyule aliyefanya figisu hadi kumfutia Leseni mwanadada Fatuma Karume, Mwanasheria mkuu wa Serikali bwana Feleshi amempeleka Wakili msomi ndugu Mwabukusi kwenye Kamati ya maadili ya Mawakili.

Katika malalamiko yake Mwanasheria wa Serikali anasema eti:

1. Mwabukuzi ni mchochezi.

2. Mwabukusi kavunja maadili ya uwakili kwa kuongea na vyombo vya habari baada ya ya kesi na kutoa matamshi ya kutaka Spika, Mbarawa na Waziri mkuu waachie ngazi.

3. Kwamba Mwabukuzi kaivunjia heshima mahakama.

Namkumbusha Mwanasheria mkuu kuwa asitafute diversion, kashindwa kuitetea serikali kwenye suala hili la mkataba sasa asianze witchhunt ili kuwatoa wananchi katika reli.

Pia Mwabukusi naye kama Mtanzania analindwa na katiba kwenye haki ya kutoa maoni. Kama hizo kanuni zenu za uwakili vinavunja haki hii ya Wakili kutoa maoni yasiyovunja sheria basi hivyo vitu na NULL and VOID ABNITIO.

Kitu kingine, Kamati ya mawakili siyo mahakama. Kama Mwabukusi kavunja sheria, Mpeleke mahakamani. Katiba inasema Mahakama ndiyo chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki nchini.

Kwa hiyo ndugu Feleshi, unajidhihirisha tu kuwa Umeshindwa kuitetea serikali kwenye mkataba mbovu, sasa unafanya Witchhunt. Yote hii ili mnyamazishe wananchi ili mfanikiwe azma yenu ya Kugawa Bandari zetu na kuuza nchi!

Wananchi hatutokubali!

Barua yenyewe ya mwanasheria mkuu wa serikali hii hapa.

View attachment 2704399
View attachment 2704644
Afutiwe
 
Hakuna haki ya matusi wala kuvunjiana heshima kwa kivuli cha uhuru wa maoni, demokrasia wala uanaharakati. Mbona Wakili msomi Peter Kibatata kwenye kesi ya Mbowe na wenzake hajawahi kuwa na matusi haya! Kwanini hoja zake pekee zisitoshe badala ya kuongezea na matusi. Hakuna taaluma isiyokuwa na miiko.
 
Wameshindwa kujibu hoja sasa wanatarget watu wanaopinga mkataba.

Wamemuweka ndani wakili Madeleka.

Wanataka kumnyamazisha wakili Mwabukusi.

Wapo wanakula njama namna ya kumdhibiti Lissu.
Madelela na Mwanukuzi na Lissu ni akili fyatu.
 
Watu wanaoongea sana, fahamu kuwa hawana uwezo wa kufikiri mbali, muono wao upeo wake ni mwisho wa pua zao.
Tunataka uwekezaji katika bandari ili ule mkataba ni ovyo.
Jaribuni kuusoma ulemkataba.
 
Back
Top Bottom