Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Sasa mkitaka wanawake wafanye majukumu yenu vipi na majukumu yao atafanya nani, hapa siongelei yale ya kimaumbile naongelea yale ya nyumbani, ambayo mnaweza kuyafanya ila hamtaki tuWanaume wanacholalamika ni wanawake wengi siku hizi wanajiuza kwa kigezo cha kuhudumiwa, kumbe ni prostitution in disguise, married and unmarried, ukihitaji ngono ni hela yako tu. Katika tamaduni zetu bibi na mama zetu walienda shambani kulima na waume zao na wanachozalisha kinatumika na familia nzima , hili la wa kisasa kutaka kuhudumiwa kama walemavu ni nothing but prostitution in disguise, mume na mke wote wanatakiwa kuzalisha chakula, mavazi na shelter for the family.
Usiniambie eti watafanya wadada wa kazi hiyo kauli huwa mnaisema tu ila hamuimaanishi, maana baada ya muda mnaanza kulalamika kwamba wake zenu wamejisahau, kazi zote wamewaachia wadada wa kazi na wengine wanaenda mbali zaidi hadi kutembea na hao wadada
Halafu namshangaa sana mtu anayetolea mifano bibi zetu kana kwamba bibi zetu walikuwa wanafurahia kutwishwa mizigo yote hiyo, kumbe walikubali kwa vile tu tamaduni zote zilitungwa na wanaume, hivyo wao hawakuwa na sauti ya kupinga hayo