Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Ni mazungumzo ya mtu na kaka yake, mdogo mtu kamuuliza bro wake,vipi mipango ya kuoa imefikia wapi?
Bro akajibu Mwanamke mwenyewe kama nataka nimpotezee maana vitu anavyopost mitandaoni na jinsi anavyojibu comments zake ni mtihani sana.
Naam huo ni mfano wa kweli kabisa ambao mfanyakazi mwenzangu alikuwa anaongea na bro wake,na haya mambo yapo sana,ladies huenda ukasahau ulicho post lakini mitandaoni huwa haisahau,wakati mwingine mnakosa mambo fulani fulani kwenye maisha yenu kwa kutaka kupata likes za muda mchache tu.
Kuwa makini na maisha yako ya mitandaoni,kile unachoona kinafurahisha nafsi yako leo huenda kesho kikawa adui mkubwa wa maendeleo na mustakabali mzima wa maisha yako.
Ni hayo tu!