Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,450
Reaction score
19,184
Jamii yetu imetufundisha kuona thamani ya mwanaume kupitia mfukoni mwake.

Ndio maana mwanaume asiye na pesa mara nyingi anaonekana hana mvuto, kwa sababu pesa imetafsiriwa kama usalama,uwezo na uongozi.

Mwanaume asiye na pesa hukosa uwezo hata wa kutoa maamuzi ndani ya familia yake mwenyewe na wakati mwingine hushindwa hata kujiamini.

Mwanaume asiye na pesa huweza hata kudharauliwa na kunyimwa nafasi aliyopaswa kuwa nayo ndani ya familia na Jamii kwa ujumla.

Watu wanataka kujua kesho itakuwaje, na kwa bahati mbaya pesa imekuwa ndio jibu la haraka.

Kwa hiyo kama huna pesa sasa, usikate tamaa. Jenga akili yako, jenga tabia yako,jifunze kutoka kwa wengine waliofanikiwa Ili nawe ufanikiwe
 
Sio lazima niwe mvuto katika jamii

Sishindani na fala yoyote

Sibabaishwi na urembo wa mwanamke yoyote, wapo wa kununua hata aftano

Hata kama mnanidharau , nikifa lazima mtaokota tu mwili wangu maana harufu yake itawakera😁
 
Jamii yetu imetufundisha kuona thamani ya mwanaume kupitia mfukoni mwake.

Ndio maana mwanaume asiye na pesa mara nyingi anaonekana hana mvuto, kwa sababu pesa imetafsiriwa kama usalama,uwezo na uongozi.

Mwanaume asiye na pesa hukosa uwezo hata wa kutoa maamuzi ndani ya familia yake mwenyewe na wakati mwingine hushindwa hata kujiamini.

Mwanaume asiye na pesa huweza hata kudharauliwa na kunyimwa nafasi aliyopaswa kuwa nayo ndani ya familia na Jamii kwa ujumla.

Watu wanataka kujua kesho itakuwaje, na kwa bahati mbaya pesa imekuwa ndio jibu la haraka.

Kwa hiyo kama huna pesa sasa, usikate tamaa. Jenga akili yako, jenga tabia yako,jifunze kutoka kwa wengine waliofanikiwa Ili nawe ufanikiwe
Screenshot_20260723-205918~2.png
 
Back
Top Bottom