Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Alisikika kijana mmoja wa hovyo akisema "mwanaume usiwe mnyonge kama huna pesa hakikisha ni shababi na mtwangio ipo." Hii technically inaitwa GG.
 
Alisikika kijana mmoja wa hovyo akisema "mwanaume usiwe mnyonge kama huna pesa hakikisha ni shababi na mtwangio ipo." Hii technically inaitwa GG.
Mtwangio bila pesa haunogi 😅
 
  • Kicheko
Reactions: al1
Jamii yetu imetufundisha kuona thamani ya mwanaume kupitia mfukoni mwake.

Ndio maana mwanaume asiye na pesa mara nyingi anaonekana hana mvuto, kwa sababu pesa imetafsiriwa kama usalama,uwezo na uongozi.

Mwanaume asiye na pesa hukosa uwezo hata wa kutoa maamuzi ndani ya familia yake mwenyewe na wakati mwingine hushindwa hata kujiamini.

Mwanaume asiye na pesa huweza hata kudharauliwa na kunyimwa nafasi aliyopaswa kuwa nayo ndani ya familia na Jamii kwa ujumla.

Watu wanataka kujua kesho itakuwaje, na kwa bahati mbaya pesa imekuwa ndio jibu la haraka.

Kwa hiyo kama huna pesa sasa, usikate tamaa. Jenga akili yako, jenga tabia yako,jifunze kutoka kwa wengine waliofanikiwa Ili nawe ufanikiwe
hivi kwa wanaume kama vile Vladimir Putin, Elon Musk, Aliko Dangote na ndugu yangu sana Bill Gates wanaweza kua wamepitia changamoto hiyo?

Mi nadhani mvuto wa mwanaume katika jamii yoyote ile huchochewa zaidi na boldness yake katika kuonyesha njia, kuchukua hatua kwa maneno na matendo. Pesa inaweza tu kutumika kuestablish hiyo boldness ya mwanaume huyo kamili katika kuchukua hatua zaidi.

Tofauti na hapo huenda ndio changamoto uliyoitaja inaweza kujionyesha.🐒
 
Back
Top Bottom