Mwanaume asiye na uwezo wa kupata mtoto anahitajika

Mwanaume asiye na uwezo wa kupata mtoto anahitajika

Ahsante kwa tahadhari, najua wapo wengi, nitakuwa makini kuwachuja, nahitaji ninayemlenga ajue this post is not for child support au nimeshindwa kulea, tunahitaji upendo kama ambavyo yeye anahitaji upendo
Huyo/Hao waliokuzalisha watoto watatu wameshatangulia mbele ya haki?
 
I am open for both but yupo mtu ambaye hilo ni hitaji lake, anahitaji upendo wa watoto na heshima.
Upo sahihi.
Sema nini yakishaingia mapenzi usiwaingize watoto hapo kati.
Siku mapenzi yakiisha upweke ukiisha unaweza kujilaumu kuwatumia watoto wako kwenye mahusiano yako na mtu mgeni au mtu mbaki kwao.
Huwezi kumjua mwezio kwa hakika hadi muishi pamoja miaka 5 mpaka 10.
Hapo tabia zake zote za asili atazionesha ambazo alizificha.
 
Wewe uko Afrika hii hii hasa Tanzania , au uko ughaibuni? Naona unaongea mambo ya Kwa wenzetu zaidi kuliko hapa bara la Giza.

Watoto hao ni wa baba Mmoja? Hii inaweza kutupa picha tunaingia maji ya kina Gani.

Pia nashauri huko mbele toa Uzi wenye somo, hili ili wangine wasije ingia mtego uliokunasa.
 
Dunia haiishiwi vitukoo wallah!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kila la kherii kwenu wahitaji. Woiiiiiih
 
Kuna comment zinakatisha watu tamaa, hata mtu akiwa na jambo lake anawaza sana kuja kubezwa na baadhi ya comment, kila kitu kinawezekana ukimuomba Mungu, JF kuna watu wengi mpaka hao anaowahitaji mtoa mada wapo.
Mkuu zidisha maombi Mungu ni mwema sana utapata hitaji lako hapa hapa usirudishwe nyuma na comment chache za kukubeza.
 
Habari

Najitokeza kwenu wana jukwaa kutafuta mwanaume matured kuanzia miaka 38-45 na mwenye hofu ya Mungu ambaye anatamani kuwa na mtoto/watoto lakini kwa namna moja au nyingine imeshindikana kwa njia ya kawaida lakini anauwezo wa kusex.

Mimi ni single mother mwenye watoto 3 natamani kuunganisha familia na mtu wa aina hiyo na tukifanikiwa kufunga ndoa tutafuata taratibu za kisheria kabisa ili kukamilisha hilo na watatumia Sir Name yako na utawamiliki kihalali.

Wasifu wangu
Miaka 35, Mkristo, Mwajiliwa sekta binafsi nina stable economy na watoto nawamudu na kuwalea vzr tu but nimekosa furaha ya mume na wao wanakosa furaha ya baba kutokana na sababu zilizojuu ya uwezo wetu. Naamini katika complete family japo kwa sasa haikuwa riziki yangu na natamani kurekebisha kwa mtu mwenye uhitaji wa kupata furaha ya watoto. (Win- Win Situation).

Hili swala zito haliitaji utani naomba only serious people waje DM.

Ahsante
Pole kwa heka heka na changamoto za maisha Bi rosita.

Sina jibu hata moja la kujibu hitajj la moyo wako, hata hivyo niruhusu nikuulize swali la kuudhi japo ni muhimu. Katika changamoto ulizo\unazo pitia, umewahi kufikiria kufanya counselling na ima Sociologist ama Clinical Psychologist ama wote kwa pamoja? Counselling sessions hizi ulishirikisha watoto?
Just food for thought.

Zaidi Mungu akujalie ufanikishe hitaji la moyo wako
 
Huu unabii mnaubadilisha
Ulikuwa hauhusu wanawake Bali makanisa. Kwamba siku za mwisho makanisa yataibuka mengi kila moja likitaka liitwe kwa jina la Yesu lakini likiwa na Mafundisho ambayo sio ya Yesu. Yani ki kubwa litajwe tu kwa jina la Yesu.
Maipotoshe tafsiri
Umewasilisha elimu ya uzamivu kabisa. Wasio kuelewa usichoke kuwaelimisha
 
Back
Top Bottom