Mwanaume asiye na uwezo wa kupata mtoto anahitajika

Ahsante kwa tahadhari, najua wapo wengi, nitakuwa makini kuwachuja, nahitaji ninayemlenga ajue this post is not for child support au nimeshindwa kulea, tunahitaji upendo kama ambavyo yeye anahitaji upendo
Huyo/Hao waliokuzalisha watoto watatu wameshatangulia mbele ya haki?
 
I am open for both but yupo mtu ambaye hilo ni hitaji lake, anahitaji upendo wa watoto na heshima.
Upo sahihi.
Sema nini yakishaingia mapenzi usiwaingize watoto hapo kati.
Siku mapenzi yakiisha upweke ukiisha unaweza kujilaumu kuwatumia watoto wako kwenye mahusiano yako na mtu mgeni au mtu mbaki kwao.
Huwezi kumjua mwezio kwa hakika hadi muishi pamoja miaka 5 mpaka 10.
Hapo tabia zake zote za asili atazionesha ambazo alizificha.
 
Wewe uko Afrika hii hii hasa Tanzania , au uko ughaibuni? Naona unaongea mambo ya Kwa wenzetu zaidi kuliko hapa bara la Giza.

Watoto hao ni wa baba Mmoja? Hii inaweza kutupa picha tunaingia maji ya kina Gani.

Pia nashauri huko mbele toa Uzi wenye somo, hili ili wangine wasije ingia mtego uliokunasa.
 
Dunia haiishiwi vitukoo wallah!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kila la kherii kwenu wahitaji. Woiiiiiih
 
Kuna comment zinakatisha watu tamaa, hata mtu akiwa na jambo lake anawaza sana kuja kubezwa na baadhi ya comment, kila kitu kinawezekana ukimuomba Mungu, JF kuna watu wengi mpaka hao anaowahitaji mtoa mada wapo.
Mkuu zidisha maombi Mungu ni mwema sana utapata hitaji lako hapa hapa usirudishwe nyuma na comment chache za kukubeza.
 
Pole kwa heka heka na changamoto za maisha Bi rosita.

Sina jibu hata moja la kujibu hitajj la moyo wako, hata hivyo niruhusu nikuulize swali la kuudhi japo ni muhimu. Katika changamoto ulizo\unazo pitia, umewahi kufikiria kufanya counselling na ima Sociologist ama Clinical Psychologist ama wote kwa pamoja? Counselling sessions hizi ulishirikisha watoto?
Just food for thought.

Zaidi Mungu akujalie ufanikishe hitaji la moyo wako
 
Umewasilisha elimu ya uzamivu kabisa. Wasio kuelewa usichoke kuwaelimisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…